Cheti cha NIDA na JKT vinatofautiana majina wakuu, nifanyeje

Cheti cha NIDA na JKT vinatofautiana majina wakuu, nifanyeje

Pain killer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
14,361
Reaction score
21,680
Habari wakuu.

Naomba kuuliza, wakati napita jkt mujibu wa Sheria walitupa vyet vya jkt lakini kwa bahati mbaya wakati wanatupa Mimi jina langu la mwisho katika majina matatu lilikosewa kipindi kilee, kutokana na Mambo mengi wakati natoka kambini nilishindwa kufuata taratibu kurekebisha jina la mwisho nikawa nimetoka hivo hivo jina limekosewa, haya mapuuza leo yananigharimu kwa kweli.

Sasa majina yangu kwenye vyet vyote, nida, form four, Chet cha kuzaliwa, form six viko sawa, hio ya jkt ndio tofauti tu...

Hivi wakuu naweza kufanyaje kurekebisha hiki Chet, Kuna muda nataka kuenda kurekebisha mwenyewe nakumbuka kuwa namba yangu ya jeshi AT 346..! Itakuwa na jina la awali.

Hapo nifanyeje wakuu.
 
Ngoja waje kukupa muongozo.

Nashukuru Alphabet ya mwanzo ya jina langu iliniokoa kwenda huko maana walichukuliwa wenye majina ya alphabet za mwanzo
 
Usipende kutoa details zako, nenda mahakamani wakuandikie kiapo kuwa jina sahihi ni fulani, lililopo kwemye cheti lina makosa, ukipata kiapo cheti unaweza tumia sehem yoyote. Nitafute dm nitakusaidia bure
 
Habari wakuu .

Naomba kuuliza ,wakati napita jkt mujibu wa Sheria walitupa vyet vya jkt lakini kwa bahati mbaya wakati wanatupa Mimi jina langu la mwisho katika majina matatu lilikosewa kipindi kilee...
Nenda nacho makao makuu ya jkt kuna ofisi ya kushughulikia watakurekebishia.
Kwani wakati mnapewa hamkuambiwa kama kuna makosa muende ??
 
Usipende kutoa details zako, nenda mahakamani wakuandikie kiapo kuwa jina sahihi ni fulani, lililopo kwemye cheti lina makosa, ukipata kiapo cheti unaweza tumia sehem yoyote. Nitafute dm nitakusaidia bure
Asante mkuu nakuja inbox unipe maelekezo kidogo
 
Unashukuru tena, huoni kwamba umekosa nafasi za polisi?!
Ndio nashukuru maana sikutaka kwenda huko.

Nilichaguliwa awamu ya pili ila tuliambiwa tuandike barua za kuhairisha ili tuende chuo kwanza, nilifanya hivyo na sasa mambo yashabadilika, ndio ishaisha hivyo
 
Nenda nacho makao makuu ya jkt kuna ofisi ya kushughulikia watakurekebishia.
Kwani wakati mnapewa hamkuambiwa kama kuna makosa muende ??
Sasa mkuu tulipewa utaratibu but Mimi nilitoka mapema kulikuwa na hatua nyingi so nikawa nimepuuzia ...

Any way makao makuu wanaweza nirekebishia ?
 
Nenda mahakamani ujaziwe Deed poll ili usimame na majina yaliyojitokeza kwenye NIDA, cheti cha kuzaliwa na hivyo vyeti vya shule. Baada ya kupata hiyo Deed poll peleka wizara ya ardhi isajiliwe tayari kwa matumizi.
 
Deed pol ni ya kubadili majina, ye anahitaji affidavit au kiapo kuthibitisha majina ni yake na yaliandikwa kimakosa, ambapo hata mwanasheria anaweza fanya hvo. Haina haja ua deed poll
 
Deed pol ni ya kubadili majina, ye anahitaji affidavit au kiapo kuthibitisha majina ni yake na yaliandikwa kimakosa, ambapo hata mwanasheria anaweza fanya hvo. Haina haja ua deed poll

Mkuu nijuavyo mie deed poll sio kubadili majina tu, endapo nyaraka za mtu mmoja zina majina mawili tofauti anatakiwa kulikataa jina moja na kutumia jina aliloamua yeye kutoka moja ya nyaraka zake.

Affidavit unakubali majina yote kuwa ni ya kwako ila kuna baadhi ya huduma huko mbeleni itamsumbua maana watahitaji asimame na jina moja na wala sio kutumia majina yote.
 
Ndio nashukuru maana sikutaka kwenda huko.

Nilichaguliwa awamu ya pili ila tuliambiwa tuandike barua za kuhairisha ili tuende chuo kwanza, nilifanya hivyo na sasa mambo yashabadilika, ndio ishaisha hivyo
Haina kwere..
 
Mkuu nijuavyo mie deed poll sio kubadili majina tu, endapo nyaraka za mtu mmoja zina majina mawili tofauti anatakiwa kulikataa jina moja na kutumia jina aliloamua yeye kutoka moja ya nyaraka zake. Affidavit unakubali majina yote kuwa ni ya kwako ila kuna baadhi ya huduma huko mbeleni itamsumbua maana watahitaji asimame na jina moja na wala sio kutumia majina yote.

Uko sahihi kabisa kama yupo Dar aende pale magogoni kuna kontena la wanasheria akiwa na elfu15 wanamtengenezea Deed poll chap.

Then anaenda wizara ya ardhi ipo pale pale watampa control number akalipie elfu32 then atakuwa huru kutumia majina.
 
Back
Top Bottom