Wauza unga wa Bongo ni wajanja sana. Ndio wameamua kuizima issue ya Chid Benz kwa mtindo huu wa kumpeleka kwa Babu Tale? Najua kama issue ya uteja wa Chid ingewaathiri sana Rumi na Nassoro coz ndio wao waliofanya awe teja.
Wamekuwa hawataki kabisa issue ya uteja wa Chid itawale kwenye mazungumzo ya Watanzania kwa usalama wao. Kama mnakumbuka kuna wakati 2014 Chid alitawala mitandaoni kama hivi, kwa haraka wakaizima issue.
Fasta ikatangazwa Diamond na AY watamsimamia kimuziki na fasta ukatolewa wimbo wake wa Mpaka Kuchee aliowashirikisha AY na Diamond, na baada ya hapo stori zikawa Chid kurudi kwenye game sio kukongoroka.
Watanzania walipobadilisha hoja, basi na wao wakanyoosha miguu na kuendelea kuponda raha zao na kumuacha Chid akiendelea kujikongoroa mwili wake kwa kuvuta unga kwa kiasi atakacho. Kazi yake ni kuvuta, kulala, kuamka na kuvuta tena.
Imekuwa ndio mtindo, kila Chid akitokeza kwenye jamii juu ya uteja wake anatajiwa Meneja mpya, ashakuwa chini ya Tunda Man na Shetta. Na sasa wametumia njia ile ile, ila wameongeza kwa kumpeleka sober ambako hata TID alipelekwa na aliporudi gari likawaka tena.
Ifike wakati Watanzania tusihamishwe hoja kwa 'peremende' za hawa wauza unga, ambao wakati wote wametokeza kujitia kumsaidia Chid inapotokea uteja wake kujadiliwa na sehemu kubwa ya jamii. Ndio hawa hawa wauza unga waliomsaidia kwenye kesi ya kukamatwa na unga.
Wanampumbaza Chid kwa kumweka kwenye nyumba nzuri ili kujitia wako naye na kumpa uwezo wa kuvuta unga kwa kiasi atakacho. Wameshamtumia vya kutosha hawamtaki tena, wamebaki kumlinda asizungumze na wala asizungumzwe na Watanzania.
Rumi (a.k.a Rashid Jabu) na mshikaji wako Nassoro (Nasabshort) iko siku Chid atawagharimu tu labda mumtoe pumzi kama Ngwair. acheni leo mjione wajanja ila iko siku.
Ova