Chid Benz: Tupac yupo Cuba na tunawasiliana naye!

Chid Benz: Tupac yupo Cuba na tunawasiliana naye!

The Businessman

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
7,397
Reaction score
9,255
21150171_2066719276675813_7638136228373570851_n.jpg

Chidi Benz azua jipya mjini, adai 2Pac yuko hai na anaishi nchini Cuba, na wanaongea kila siku na tayari ameshafanya naye ngoma itakayotoka hivi karibuni.

Chidi Benz ambaye kwa sasa anazungumzwa sana kwa skendo za utumiaji wa madawa ya kulevya, akiongea na eNewz alisema kuwa "Maneno yanayoongelewa kwamba 2Pac amefariki siyo kweli, Kila siku ninaongea na 2pac na hata sasa hivi nimetoka kuongea naye"

Mimi na 2Pac tumekutana Cuba, na tumefanya nyimbo ya pamoja na Mungu akisaidia hivi karibuni tataachia nyimbo hiyo".

"2Pac ana mpango wa kurudi kwenye muziki, na wimbo wetu tuliorekodi ndiyo utamrudisha. Na hivi karibuni 2Pac atakuja bongo, ila atakuja kimya kimya kama alivyokuja Beckam" Aliongeza Chidi Benz.

Pia Chid aliendelea kwa kusema "Baada ya kukutana na 2Pac tuliamua kurekodi baadhi ya vipande vya video ambavyo tutaanza kuvisambaza kwanza ili kuweza kuwajulisha watu kuwa 2Pac bado yupo hai na kuwaondoa watu fikra za kuwa 2Pac ni marehemu".

Hata hivyo kitu cha kushangaza zaidi ni baada ya Chid kuendelea kusema kwamba anamdai 2Pac kipini chake cha puuani ambacho alimuazima walipokuwa wote nchini Cuba.

Kama ilivyokuwa kwa Young Dee, Chid Benz naye ameonekana kuwa na hali ya kujichanganya sana katika maelezo yake kila aanapoongea.

Hivi karibuni Ali Kiba akiongea na eNewz alishauri serikali iingilie kati suala la Chid Benz na kumpatia matibabu. Na hata kama akibainika anajihusisha na madawa Alikiba alishauri "Chid asifungwe bali apelekwe 'rehab' akatibiwe kwani kumfunga mtu anayetumia madawa ni kumtesa tu".
 
Nimetoka kuangalia hapa, hyu jamaa anachanganyikiwa aisee.
 
Nimeona Interview yake kwenye matangazo ya E-News EATV anasema Tupac yupo hai nchini Cuba na tunawasiliana naye na kipini alichovaa puani ni cha kwake. Na anafanya mpango amlete Tanzania.

Huyu jamaa karibu anakuwa 'chizi fresh'.
Arudishwe Sober house
 
Ngada haijawai kumuacha mtu salama sasa huyo ni wakuonewa huruma tu
 
Back
Top Bottom