Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hilo gazeti linaripoti .kiJUHA sana, hiyo habari haijulikani kama ni ya mwaka huu au miaka mitatu iliyopita kwa vile haina tarehe. Hakuna background ya kazi ya Ray C kama ni ofisi ya muziki, utangazaji, ofisi ya kubwia unga au danguro....Kwa uandishi huu acheni tuendelee kuwadharau
Mambo binamu
Naona hufuatilii yanayojiri hivi sasa.
Ray C ana ofisi yake ya taasisi yake inayoitwa Ray C Foundation. Hii ni asasi inayowasaidia waathirika wa madawa ya kulevya kuachana nayo kwa msaada wa kitabibu. Inasaidia kuwapa wathirika hao dawa za kuondoa sumu mwilini itokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, yaani, "narcotics rehabilitation medicine" na kwa namna nyingine "narcotics detoxification". Ni sumu hizi ndizo zinazoleta "utegemezi" (soma "uteja") kwani zinapoingia mwilini husababisha mtumiaji awe anahitaji kutumia dawa hizo za kulevya, kimsingi huwa HAPONI mpaka ziondolewe.
Ni tatizo ambalo limewakumba vijana wengi wa Kitanzania, haswa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambako Ray C alipitia, mzazi mwenziwe na "Chidi Benz", Mariam alipitia, na pia hata hao wengine wanaodaiwa kuhusika na matumizi ya dawa hizo, kama vile "Chidi Benz".
Binafsi niliwahi kuongea kwa simu na "Chidi Benz". Nilichokiona kwake ni kwamba si mtu anayejiheshimu kwani majibu yake ni ya "ovyo". Nadhani hata hao "mapromota" wa muziki huu wa kizazi kipya wamemkacha kutokana na tabia zake za ajabu ajabu, kuwa na kesi lukuki. Ninachoshangaa ni kwamba Mahakama zetu hazijampa hukumu inayostahili. Je, ni pesa zake anazowahonga makarani na mahakimu ndizo zinazomkwepesha kwenda jela? Hivi akiwekwa ndani MWAKA MMOJA TU, hatabadilika?
Wenye kuwajua wanasheria watoe hoja hiyo - haswa kuhusu kesi ya Mwanaisha - ili Mahakama ichukue hatua ya kuyanusuru maisha yake. Iko siku "Chidi Benz" atakanyaga pabaya na atagombana na mtu ambaye atajihami kwa silaha! Akila "shaba" nani atafaidika na kifo chake?
Mimi ni mjumbe tu na mjumbe hauwawi. Fikisheni ujumbe kwa wahusika. Maisha ya "Chidi Benz" yapo hatarini!
Nimemaliza.
Umeona eeeh, hadi nimeuliza ndio nimepata background, je ni wasomaji wote wa hicho chanzo cha habari wana fursa ya kuuliza? Kwa hiyo mwandishi angeweka sentensi moja tu kuhusu Ray C foundation. Then kuripoti alhamisi, au jumatano bila tarehe halisi inaacha maswali maana kila wiki kuna hizo siku. Anyway inategemeana na wasomaji na upeo wao.
Hilo gazeti linaripoti .kiJUHA sana, hiyo habari haijulikani kama ni ya mwaka huu au miaka mitatu iliyopita kwa vile haina tarehe. Hakuna background ya kazi ya Ray C kama ni ofisi ya muziki, utangazaji, ofisi ya kubwia unga au danguro....Kwa uandishi huu acheni tuendelee kuwadharau
hii habari haipo balance kabisa kwanini wameshindwa kumtafuta Chid Beenz nae asikike anasemaje!
tutaamini vipi kama asingiziwi kwa tabia zake za nyuma!?