Naona hufuatilii yanayojiri hivi sasa.
Ray C ana ofisi yake ya taasisi yake inayoitwa Ray C Foundation. Hii ni asasi inayowasaidia waathirika wa madawa ya kulevya kuachana nayo kwa msaada wa kitabibu. Inasaidia kuwapa wathirika hao dawa za kuondoa sumu mwilini itokanayo na matumizi ya dawa za kulevya, yaani, "narcotics rehabilitation medicine" na kwa namna nyingine "narcotics detoxification". Ni sumu hizi ndizo zinazoleta "utegemezi" (soma "uteja") kwani zinapoingia mwilini husababisha mtumiaji awe anahitaji kutumia dawa hizo za kulevya, kimsingi huwa HAPONI mpaka ziondolewe.
Ni tatizo ambalo limewakumba vijana wengi wa Kitanzania, haswa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambako Ray C alipitia, mzazi mwenziwe na "Chidi Benz", Mariam alipitia, na pia hata hao wengine wanaodaiwa kuhusika na matumizi ya dawa hizo, kama vile "Chidi Benz".
Binafsi niliwahi kuongea kwa simu na "Chidi Benz". Nilichokiona kwake ni kwamba si mtu anayejiheshimu kwani majibu yake ni ya "ovyo". Nadhani hata hao "mapromota" wa muziki huu wa kizazi kipya wamemkacha kutokana na tabia zake za ajabu ajabu, kuwa na kesi lukuki. Ninachoshangaa ni kwamba Mahakama zetu hazijampa hukumu inayostahili. Je, ni pesa zake anazowahonga makarani na mahakimu ndizo zinazomkwepesha kwenda jela? Hivi akiwekwa ndani MWAKA MMOJA TU, hatabadilika?
Wenye kuwajua wanasheria watoe hoja hiyo - haswa kuhusu kesi ya Mwanaisha - ili Mahakama ichukue hatua ya kuyanusuru maisha yake. Iko siku "Chidi Benz" atakanyaga pabaya na atagombana na mtu ambaye atajihami kwa silaha! Akila "shaba" nani atafaidika na kifo chake?
Mimi ni mjumbe tu na mjumbe hauwawi. Fikisheni ujumbe kwa wahusika. Maisha ya "Chidi Benz" yapo hatarini!
Nimemaliza.