Chidi Benz arudia madawa ya kulevya, Babu Tale aapa kutomsaidia tena!


Hata huyo Babu Tale wenu nae namwona ni Mpumbavu tu pia kwani alipashwa kumtumia Msanii Rehema Chalamila ( Ray C ) kama reference yake ndipo ajikite katika kumsaidia Chid Benz. Hivi kama tu Ray C aliweza kusaidiwa tena na Rais Mstaafu Kikwete kwenda rehab huku akipewa first class treatment lakini bado akawa tu anabwia bwimbwi itakuwa kwa Chid Benz aliyepelekwa tu huko madongo kuporomoka Bagamoyo?

Leo huyo Babu Tale anaposema tena hadi kuuapa kuwa hatomsaidia tena Chid Benz kwani kuna Mtu aliyemtuma? Ni sifa zake mwenyewe na kiherehere cha kutaka kujionyesha yeye ni Philanthropist ndicho Kimemponza na sisi Watoto wa mjini tunajua kwanini leo Babu Tale analalamika kwani alitaka kuchuma zaidi kupitia fadhila yake kwa Chid Benz ila bahati mbaya Chizi karudia tena Utahaira wake na sasa kaingia bonge la hasara.

Eti unajitolea kumtibia Chid Benz wakati Wazazi wake, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa pale Ilala flats wameshindwa. Shenzy Taipu kabisa na akome kujipendekeza siku nyingine. Nani aliyekuambia kuwa Chid Benz anatibika? Hivi LAANA huwa INATIBIKA? Huwa sipendi Watu wanaokurupuka na wasiopenda kutumia akili. Muulizeni vizuri huyo Chid Benz wenu Mtu gani aliyemdhalilisha mwaka huu mwezi wa Tatu ( March ) maeneo ya Kinondoni na baadae tena Kigamboni halafu yule Mtu alimtamkia maneno gani Chid Benz na ambayo leo yametimia?
 
Vipi mh rais mstaafu kikwete alipomsaidia ray c naye alikuwa anatafuta kiki.....maana naye baada ya mda alirudia na ukizingatia ukubwa na heshima ya mtu aliyemsaidia
 
Mkuu punguza kwa hasira afu sasa utuelezee huyo mtu aliemtakia maneno chid yakatimia nani.. Tupe ubuyu tumung'unye sie
 
uwe unapiga picha au kurekodi video, kisha unatuletea ubuyu hapa
 
Mkuu punguza kwa hasira afu sasa utuelezee huyo mtu aliemtakia maneno chid yakatimia nani.. Tupe ubuyu tumung'unye sie

Nitamwaribia Mkuu na siwezi kumtaja ila Wasanii wenzie wanalijua sana hili nililolisema hapa na hata huyo Mtu wanamjua mno. Nasisitiza tena kusema kuwa LAANA huwa haina TIBA na naomba niishie hapa tafadhali.
 
Kama mzazi/wazazi wake walimshindwa mwanzo basi ni ngumu kwa mtu baki kuweza kumkanya na akaacha...

Kilichobaki ni kuuacha ulimwengu uumvunze maana ndio mwalimu nambari moja...
mkuu wewe ni legend hapa,
 
ni mtu gani huyo mkuu? na ni maneno gani?
 
ni mtu gani huyo mkuu? na ni maneno gani?

Nakupa tu hint na mengineyo utayafuatilia mwenyewe. Ni hivi watafute Wasanii marafiki sana na Chid Benz amabo ni Watatu ( 3 ) mmoja ni wa Kike anaishi Sinza Mori huku wengine wa Kiume mmoja akiishi Ilala katikati ya Amana na Bungoni huku mwingine akiishi Kinondoni Manyanya watakupa kila kitu na bahati nzuri wanafahamika sana tu hivyo watafute watakupa mkanda mzima ila kwa Mimi naomba sasa niishie tu hapa tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…