Kila mwanaume ana vigezo maalum au sifa anazozitazamia kwa mwanamke ambaye angependa kuwa naye kwenye ndoa, na mara nyingi tabia hizi zinakuwa ni msingi muhimu kabla ya kuingia kwenye mahusiano. Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashidi Abdallah, maarufu kama Chidi Benz, amefunguka kuhusu aina ya tabia ambazo kwake zinaonyesha mwanamke kuwa siyo "wife material."
Chidi Benz anasema, kuna tabia kadhaa ambazo mwanamke akiwa nazo, zinamfanya mwanaume yeyote kujua kuwa huyo siyo chaguo sahihi kwa ndoa. Hizi ni tabia ambazo kwa mtazamo wake zinaathiri uaminifu, upendo, na maelewano mazuri katika mahusiano ya muda mrefu kama ndoa.