GE2025 Chief Justice George Masaju's Speech Towards the 2025 General Election in Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
Lushoto, Tanzania

Alhamisi, 18 Septemba 2025​

MAFUNZO YA UENDESHAJI MASHAURI YA UCHAGUZI KWA MAJAJI, MAHAKIMU YAHITIMISHWA​

View: https://m.youtube.com/watch?v=WAAaVOMqZkM
· Jaji Mkuu asema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Kanuni za uchaguzi
· Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman ashiriki kutoa uzoefu kuhusu mashauri ya uchaguzi
· Jumla ya washiriki 381 wanufaika na mafunzo hayo
Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma

Mafunzo ya Namna Bora ya Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa kwa Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya nchini yamehitimishwa leo, huku Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akishauri kwamba Kanuni za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho (electoral laws) ili kuwawezesha Majaji na Mahakimu kusikiliza ipasavyo mashauri hayo.

Akizungumza leo tarehe 18 Septemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo hayo yaliyohusisha washiriki wa kundi la mwisho la Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Masaju amesema majadiliano mbalimbali pamoja na changamoto zilizowasilishwa na washiriki wa Mafunzo yameonesha kuwa, kanuni hizo zina mapungufu na hivyo kuwa na haja ya kuzifanyia mabadiliko.

“Niwashukuru kwa kukubali kufanya mabadiliko ya kanuni hizi zinazotungwa na Jaji Mkuu, tumepata ushauri mzuri hapa na Jaji Mkuu Mstaafu ametushauri maeneo ya kuangalia , tuna pa kuanzia na wawezeshaji wetu ni mahiri na ninyi wenyewe ni mahiri mna ustadi mkubwa kwenye maeneo haya na hili tutalifanya kabla ya tarehe ya uchaguzi wenyewe na litakuwa zoezi shirikishi lakini maboresho ya mwisho yatakayotolewa lazima yapate kibali cha Mahakama maana sisi ndio wenye ile sheria na mwenye mamlaka ya kuitunga ile sheria ni Jaji Mkuu,” amesema Mhe. Masaju.

Jaji Mkuu ameeleza kuwa, lengo la kufanyia marekebisho kanuni hizo ni kwa sababu ni sheria za uchaguzi zimekusudia kufikia lengo la wananchi la kupata Serikali ambayo itawajibika kwao kwa ajili ya ustawi wao wananchi kama inavyotajwa kwenye Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine inasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na inayofuata haki ya kijamii na kwamba mamlaka ya Serikali hiyo yatapatikana kutoka kwa wananchi.

‘.... Na kwamba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii na lengo kuu la Serikali ikiwa ni ustawi wa wananchi na Serikali ikiwajibika kwa wananchi,’ amenukuu Mhe. Masaju akirejea Ibara ya 8 ya Katiba.

Ameongeza kuwa, lengo lingine la kufanya maboresho kwenye kanuni hizo ni kuleta uwazi zaidi katika kupata tafsiri sahihi ya migogoro ya uchaguzi inayoletwa mahakamani na kujua kama uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema kuwa, katika mazingira kama hayo, Mahakama ambayo ina jukumu la kutunga kanuni za kusimamia mashauri ya uchaguzi lazima ijiridhishe kama kanuni hizo zinakidhi matarajio ya wananchi ili watu wanaokuwa na mashauri ya uchaguzi mahakamani yaamuliwe kwa namna ambayo wanaridhika kwamba maamuzi hayo yamefanyika kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.

Ameeleza kuwa, baadhi ya changamoto zilizoonekana katika Kanuni hizo ni pamoja na kukosekana kwa uwazi na uhakika pamoja na mapungufu mengine yatakayobainika baada ya kuzipitia kanuni hizo.
Kufuatia maelekezo ya Jaji Mkuu kuhusu mabadiliko ya kanuni za uchaguzi, Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa pamoja wamepanga kukutana Jumatatu tarehe 22 Septemba, 2025 ili kupitia kanuni hizo za uchaguzi na kutoa mapendekezo ya maboresho yake.

Aidha, Mhe. Masaju ameeleza kwamba, mashauri yanayotokana na migogoro ya uchaguzi yatasikilizwa katika Mahakama zilizopo nchini na kuwataka watu wanaohitaji kufuatilia mashauri hayo kufika katika Mahakama husika wasikilize kwa amani na kwa kufuata na kuheshimu taratibu za Mahakama.

Jaji mkuu ametoa rai kwa mtu ambaye hataridhika na uamuzi wa Mahakama ya ngazi fulani ana haki ya kukata rufaa kwa kuwa ni haki ya kikatiba.

Mhe. Masaju amesisitiza kuwa, Mahakama inalo jukumu la kudumisha utawala wa sheria katika nchi kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ambapo amethibitisha kwamba Mahakama itahakikisha inaendelea kufanya hivyo.
“Pamoja na mamlaka tuliyo nayo ya kikatiba na kisheria, mamlaka yetu pia yapo katika uwezo wetu wa kufanya maamuzi ya Mahakama kwa maslahi ya sheria, amesema Jaji.

Kadhalika, Jaji Mkuu ameeleza kwamba hakutakuwa na urushaji mubashara (live streaming) ya mashauri hayo na kusisitiza kuwa, “hakutakuwa na ‘live streaming’ ya mashauri hayo huku akirejea kinachozungumziwa kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa; ni haki ya kupata taarifa sio haki ya kutangazwa wakati wote.

Katika hatua nyingine amewashukuru waandaaji wa mafunzo hayo Mahakama na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, wawezeshaji pamoja na washiriki wote wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu.

“Nawashukuru washiriki wote, waandaaji na Wawezeshaji wa Mafunzo haya ambayo niliyafungua tarehe 28 Agosti, 2025 lakini katika ngazi mbalimbali, tulianza na Mahakama Kuu kwa pamoja, Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya, zoezi ambalo limefanyika kwa ustadi mkubwa sana,” amesema Mhe. Masaju.

Kwa upande wake Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman ametoa uzoefu wake kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani juu ya mashauri yatokanayo na migogoro ya uchaguzi ambapo ameshauri juu ya menejimenti fasaha ya mashauri ya uchaguzi kwa kuwa yanagusa Taifa, kuwa na matumizi fasaha ya lugha na mengine.

“Tuwajibike ipasavyo na tutumie uchaguzi huu kujiimarisha kama Mahakama kupitia maamuzi yetu kujenga ‘integrity’ ya Mahakama,” amesema Mhe. Chande.

Jaji Mkuu huyo Mstaafu amesisitiza mambo ya kuzingatia kuwa ni pamoja na Mahakama kuangalia Sheria na wajibu wake kwenye masuala ya uchaguzi, usikilizwaji wa mashauri ya uchaguzi mapema ipasavyo na Mahakama iwe na uwazi na yenye kufikika kwa kuwa mashauri hayo yana maslahi ya umma.

Mhe. Chande amesema, mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa uchaguzi na migogoro ya uchaguzi kwa kiasi kikubwa ni muingiliano kati ya siasa na sheria.

Majaji wengine walioshiriki kutoa uzoefu wao kuhusu mashauri ya migogoro ya uchaguzi ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Ferdinand Wambali na Mhe. Issa Maige.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto yalifunguliwa na Jaji Mkuu tarehe 28 Agosti, 2025 lengo likiwa ni kuimarisha uwezo wa Maofisa Mahakama, yaani Majaji na Mahakimu katika namna bora ya kuendesha mashauri ya uchaguzi ili kuwaweka tayari kushughulikia mashauri hayo kwa weledi na mapema ipasavyo pale ambapo wadaawa watakuwa wamegonga milango ya Mahakama kutafuta haki.

Kwa mujibu wa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo mafunzo hayo yametolewa kwa jumla ya washiriki 381 wakiwemo Majaji wa Mahakama Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya.

Source: TanzaniaJudiciary.blogspot
 
Ijumaa, 19 Septemba 2025​

TLS YAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA​

Matukio katika picha wakati Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipokutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiwa na sehemu ya Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo na sehemu ya Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025
Source : tanzaniajudiciary.blogspot
 
Lushoto, Tanzania

Alhamisi, 18 Septemba 2025​

MAFUNZO YA UENDESHAJI MASHAURI YA UCHAGUZI KWA MAJAJI, MAHAKIMU YAHITIMISHWA​

View: https://m.youtube.com/watch?v=WAAaVOMqZkM
· Jaji Mkuu asema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Kanuni za uchaguzi
· Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman ashiriki kutoa uzoefu kuhusu mashauri ya uchaguzi
· Jumla ya washiriki 381 wanufaika na mafunzo hayo
Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma

Mafunzo ya Namna Bora ya Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa kwa Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya nchini yamehitimishwa leo, huku Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akishauri kwamba Kanuni za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho (electoral laws) ili kuwawezesha Majaji na Mahakimu kusikiliza ipasavyo mashauri hayo.

Akizungumza leo tarehe 18 Septemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo hayo yaliyohusisha washiriki wa kundi la mwisho la Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Masaju amesema majadiliano mbalimbali pamoja na changamoto zilizowasilishwa na washiriki wa Mafunzo yameonesha kuwa, kanuni hizo zina mapungufu na hivyo kuwa na haja ya kuzifanyia mabadiliko.

“Niwashukuru kwa kukubali kufanya mabadiliko ya kanuni hizi zinazotungwa na Jaji Mkuu, tumepata ushauri mzuri hapa na Jaji Mkuu Mstaafu ametushauri maeneo ya kuangalia , tuna pa kuanzia na wawezeshaji wetu ni mahiri na ninyi wenyewe ni mahiri mna ustadi mkubwa kwenye maeneo haya na hili tutalifanya kabla ya tarehe ya uchaguzi wenyewe na litakuwa zoezi shirikishi lakini maboresho ya mwisho yatakayotolewa lazima yapate kibali cha Mahakama maana sisi ndio wenye ile sheria na mwenye mamlaka ya kuitunga ile sheria ni Jaji Mkuu,” amesema Mhe. Masaju.

Jaji Mkuu ameeleza kuwa, lengo la kufanyia marekebisho kanuni hizo ni kwa sababu ni sheria za uchaguzi zimekusudia kufikia lengo la wananchi la kupata Serikali ambayo itawajibika kwao kwa ajili ya ustawi wao wananchi kama inavyotajwa kwenye Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine inasema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na inayofuata haki ya kijamii na kwamba mamlaka ya Serikali hiyo yatapatikana kutoka kwa wananchi.

‘.... Na kwamba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii na lengo kuu la Serikali ikiwa ni ustawi wa wananchi na Serikali ikiwajibika kwa wananchi,’ amenukuu Mhe. Masaju akirejea Ibara ya 8 ya Katiba.

Ameongeza kuwa, lengo lingine la kufanya maboresho kwenye kanuni hizo ni kuleta uwazi zaidi katika kupata tafsiri sahihi ya migogoro ya uchaguzi inayoletwa mahakamani na kujua kama uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema kuwa, katika mazingira kama hayo, Mahakama ambayo ina jukumu la kutunga kanuni za kusimamia mashauri ya uchaguzi lazima ijiridhishe kama kanuni hizo zinakidhi matarajio ya wananchi ili watu wanaokuwa na mashauri ya uchaguzi mahakamani yaamuliwe kwa namna ambayo wanaridhika kwamba maamuzi hayo yamefanyika kwa kuzingatia Katiba na Sheria za nchi.

Ameeleza kuwa, baadhi ya changamoto zilizoonekana katika Kanuni hizo ni pamoja na kukosekana kwa uwazi na uhakika pamoja na mapungufu mengine yatakayobainika baada ya kuzipitia kanuni hizo.
Kufuatia maelekezo ya Jaji Mkuu kuhusu mabadiliko ya kanuni za uchaguzi, Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa pamoja wamepanga kukutana Jumatatu tarehe 22 Septemba, 2025 ili kupitia kanuni hizo za uchaguzi na kutoa mapendekezo ya maboresho yake.

Aidha, Mhe. Masaju ameeleza kwamba, mashauri yanayotokana na migogoro ya uchaguzi yatasikilizwa katika Mahakama zilizopo nchini na kuwataka watu wanaohitaji kufuatilia mashauri hayo kufika katika Mahakama husika wasikilize kwa amani na kwa kufuata na kuheshimu taratibu za Mahakama.

Jaji mkuu ametoa rai kwa mtu ambaye hataridhika na uamuzi wa Mahakama ya ngazi fulani ana haki ya kukata rufaa kwa kuwa ni haki ya kikatiba.

Mhe. Masaju amesisitiza kuwa, Mahakama inalo jukumu la kudumisha utawala wa sheria katika nchi kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ambapo amethibitisha kwamba Mahakama itahakikisha inaendelea kufanya hivyo.
“Pamoja na mamlaka tuliyo nayo ya kikatiba na kisheria, mamlaka yetu pia yapo katika uwezo wetu wa kufanya maamuzi ya Mahakama kwa maslahi ya sheria, amesema Jaji.

Kadhalika, Jaji Mkuu ameeleza kwamba hakutakuwa na urushaji mubashara (live streaming) ya mashauri hayo na kusisitiza kuwa, “hakutakuwa na ‘live streaming’ ya mashauri hayo huku akirejea kinachozungumziwa kwenye Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa; ni haki ya kupata taarifa sio haki ya kutangazwa wakati wote.

Katika hatua nyingine amewashukuru waandaaji wa mafunzo hayo Mahakama na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, wawezeshaji pamoja na washiriki wote wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu.

“Nawashukuru washiriki wote, waandaaji na Wawezeshaji wa Mafunzo haya ambayo niliyafungua tarehe 28 Agosti, 2025 lakini katika ngazi mbalimbali, tulianza na Mahakama Kuu kwa pamoja, Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya, zoezi ambalo limefanyika kwa ustadi mkubwa sana,” amesema Mhe. Masaju.

Kwa upande wake Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman ametoa uzoefu wake kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani juu ya mashauri yatokanayo na migogoro ya uchaguzi ambapo ameshauri juu ya menejimenti fasaha ya mashauri ya uchaguzi kwa kuwa yanagusa Taifa, kuwa na matumizi fasaha ya lugha na mengine.

“Tuwajibike ipasavyo na tutumie uchaguzi huu kujiimarisha kama Mahakama kupitia maamuzi yetu kujenga ‘integrity’ ya Mahakama,” amesema Mhe. Chande.

Jaji Mkuu huyo Mstaafu amesisitiza mambo ya kuzingatia kuwa ni pamoja na Mahakama kuangalia Sheria na wajibu wake kwenye masuala ya uchaguzi, usikilizwaji wa mashauri ya uchaguzi mapema ipasavyo na Mahakama iwe na uwazi na yenye kufikika kwa kuwa mashauri hayo yana maslahi ya umma.

Mhe. Chande amesema, mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa uchaguzi na migogoro ya uchaguzi kwa kiasi kikubwa ni muingiliano kati ya siasa na sheria.

Majaji wengine walioshiriki kutoa uzoefu wao kuhusu mashauri ya migogoro ya uchaguzi ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Ferdinand Wambali na Mhe. Issa Maige.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto yalifunguliwa na Jaji Mkuu tarehe 28 Agosti, 2025 lengo likiwa ni kuimarisha uwezo wa Maofisa Mahakama, yaani Majaji na Mahakimu katika namna bora ya kuendesha mashauri ya uchaguzi ili kuwaweka tayari kushughulikia mashauri hayo kwa weledi na mapema ipasavyo pale ambapo wadaawa watakuwa wamegonga milango ya Mahakama kutafuta haki.

Kwa mujibu wa Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo mafunzo hayo yametolewa kwa jumla ya washiriki 381 wakiwemo Majaji wa Mahakama Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya.

Source: TanzaniaJudiciary.blogspot

Wananchi watapataje viongozi wanaowataka wakati viongozi wanaotakiwa na wananchi Wana zuiwa kushiriki uchaguzi na kufanya siasa. Wanaoshiriki sasa ni CCM na vivuli vya ccm
 
..Jaji Mkuu anapaswa kujiongeza.

..kuendelea kutoa taarifa za muenendo wa mashauri kupitia magazeti ni kukumbatia ujima.

..Teknolojia ya habari imebadilika na mahakama nayo inapaswa kwenda na wakati.

..Jaji Mkuu hana sababu yoyote ile ya msingi ya kukataa matangazo mubashara ya mahakama zetu.

..Mahakama iruhusu Televisheni binafsi kurusha matangazo ya kesi mbalimbali.

Cc Nguruvi3
 
Mkuu
Jaji mkuu amezungumzia Mahakama kusimamia utawala wa sheria ili mamlaka itoke kwa Wananchi.
Amezungumzia vifungu mbali mbali kana kwamba ndicho Wananchi wanacholalamikia.

Jaji Mkuu antambua malalamiko ya Wananchi si mamlaka ya kimahakama bali Mahakama kutelekeza mamlaka yake na kutumiwa na wanasiasa kufanya maamuzi. Huu ndio ukweli alioukwepa lakini anaujua.

Kuhusu kesi kuendeshwa mubashara, jana Tundu Lissu aliwakumbusha Majaji 3 . Jibu alilopewa ni kwamba wanalifanyia kazi. Leo Jaji mkuu kaenda Lushoto kuwapa maagizo kijanja, kwamba, uhuru wa kupata habari si uhuru wa kurusha mubashara.

Alichokisema Jaji mkuu ni ''hukumu'' ya shauri la Lissu. Wiki ijayo utasikia majaji 3 waki 'echo' kauli ya Jaji mkuu.

Mafunzo yanayoendelea kuhus uchaguzi ni kupoteza fedha za umma, tatizo ni Mahakama kupokwa Uhuru.

Kalamu
 
Mkuu JokaKuu

Suala la mashauri mubashara lipo Mhakama kuu katika kesi ya Tundu Lissu, na majaji 3 hawajalitolea hukumu
Jaji mkuu kulizungumzia ni kuingilia mashauri yaliyoko mahakamani

Wiki ijayo Majaji wa kesi ya Tundu hawatakuwa huru kutoa maamuzi kwasababu lazima waegemea ''hukumu'' iliyotolewa na Jaji mkuu akifunga mafunzo. Suala la Tundu Lissu limehukumumiwa tayari, nje ya Mahakama

Hivi Jaji mkuu hana washauri na hakuona political ramifications ya matamshi yake!
 
WATANZANIA HATULALAMIKI KUHUSU HZO VIFUNGO VYAKE VYA SHERIA.tunalalamika kuhusu mahakama kutokuwa na nguvu imeingiliwa na wanasiasa.maagizo kutoka mzizi uliojichmbia hadi chni ndyo inayoharibu imani ya mahakama.mahakama zetu zinachezewa na wanasiasa.mahakama zpo kwaajili ya vibaka na kuwalinda wanasiasa.
 
Jaji mkuu anapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.sijaona chochote pale.ni kuhadaa watz.amemjibu lisu kuhusu mubashara kijanja agizo toka juu.hakuna jipya kwa huyu bwana.bado yupo kisiasa
In fact hajamjibu Tundu Lissu bali kupitia maelezo yake '' ametoa hukumu'' ya suala la Lissu lililo mahakamani
Yaani '' amewaagiza Majaji'' wa kesi ya Lissu watoe hukumu gani!
 
Mkuu JokaKuu

Suala la mashauri mubashara lipo Mhakama kuu katika kesi ya Tundu Lissu, na majaji 3 hawajalitolea hukumu
Jaji mkuu kulizungumzia ni kuingilia mashauri yaliyoko mahakamani

Wiki ijayo Majaji wa kesi ya Tundu hawatakuwa huru kutoa maamuzi kwasababu lazima waegemea ''hukumu'' iliyotolewa na Jaji mkuu akifunga mafunzo. Suala la Tundu Lissu limehukumumiwa tayari, nje ya Mahakama

Hivi Jaji mkuu hana washauri na hakuona political ramifications ya matamshi yake!

..sidhani kama ni aina ya Jaji Mkuu ambaye taifa linamhitaji kwa wakati huu.

..mahakama haiwezi tena kutegemea taarifa za mashauri zipatikane kupitia magazeti tu.

..hata hiyo hotuba ya Jaji Mkuu imerushwa na vyombo vya habari vya TV, sasa kwanini hataki kesi zionekane kwa mtindo huohuo?
 
WATANZANIA HATULALAMIKI KUHUSU HZO VIFUNGO VYAKE VYA SHERIA.tunalalamika kuhusu mahakama kutokuwa na nguvu imeingiliwa na wanasiasa.maagizo kutoka mzizi uliojichmbia hadi chni ndyo inayoharibu imani ya mahakama.mahakama zetu zinachezewa na wanasiasa.mahakama zpo kwaajili ya vibaka na kuwalinda wanasiasa.

..Jaji Mkuu anataka kuficha uozo katika mahakama anazoziongoza.

..Vyombo vya habari vya televisheni vikiingia mahakamani watu wengi zaidi watashuhudia uozo ulioko huko waziwazi bila kuyumbishwa na propaganda za watu wa kati.
 
In fact hajamjibu Tundu Lissu bali kupitia maelezo yake '' ametoa hukumu'' ya suala la Lissu lililo mahakamani
Yaani '' amewaagiza Majaji'' wa kesi ya Lissu watoe hukumu gani!
Tayari ni agizo toka juu ameingilia kesi inayoendelea kwa kaul yake hyo kaharibu imani ya watu kwa hzi mahakama zetu.imani yetu bdo sana kwa mahakama zetu bado wanatumika kisiasa.kwa kauli yake ile hzo vikao sijui semina waliyokaa tayar totaly rubish ni kupoteza tu kodi ya wananchi bila sababu za maana
 
..sidhani kama ni aina ya Jaji Mkuu ambaye taifa linamhitaji kwa wakati huu.
Huyu si kiwango cha akina Nyalali, Samatta, Lukakingira, Mzavaz, Kisanga etc.
Aliye iingiza Mahakama katika ''siasa'' na kuwa tawi la chama ni Jaji rtd I. Juma. Huyu ndiye aliyeanzisha '' erosion ya trust'' katika mahakama zetu. Kwa Jaji Masaju sikutegemea chochote , tunamjua
..mahakama haiwezi tena kutegemea taarifa za mashauri zipatikane kupitia magazeti tu.
Halafu walipofungua Jengo lao pale Dodoma walisema Mahakama imekuwa modernized katika Afrika na sijui ni ya Tano au Kumi Duniani kwa kwenda digital. Masaju anaturudisha enzi za Mzalendo na Uhuru. Shame
..hata hiyo hotuba ya Jaji Mkuu imerushwa na vyombo vya habari vya TV, sasa kwanini hataki kesi zionekane kwa mtindo huohuo?
Jambo jema wanataka lirushwe waonekane. Kinachowakwaza sasa hivi ni kesi ya Tundu Lissu
Wanaogopa kuwaudhi na kukiuka maagizo kutoka juu. CJ Masaju shame on you
 
Tayari ni agizo toka juu ameingilia kesi inayoendelea kwa kaul yake hyo kaharibu imani ya watu kwa hzi mahakama zetu.imani yetu bdo sana kwa mahakama zetu bado wanatumika kisiasa.kwa kauli yake ile hzo vikao sijui semina waliyokaa tayar totaly rubish ni kupoteza tu kodi ya wananchi bila sababu za maana
Shauri la Tundu Lissu limeamualiwa kwenye mikutano si mahakamani tena akiwa hayupo
Maagizo kutoka juu kwa CJ hayawezi kupingwa na Majaji 3.

Mwambieni TAL akiwa magereza huku nje tunajua hukumu ya shauri lake la TV Mubashara! keshahukumiwa
 
In fact hajamjibu Tundu Lissu bali kupitia maelezo yake '' ametoa hukumu'' ya suala la Lissu lililo mahakamani
Yaani '' amewaagiza Majaji'' wa kesi ya Lissu watoe hukumu gani!
NA HAYO NDO MAAGIZO KUTOKA JUU.
22/9/025 MAJAJI WATATEMBELEA HUMO. MAHAKAMA HAITARUHUSU URUSHWAJI MUBASHARA.
TAYARI KAWAELEKEZA CHAKUFANYA.
 
Back
Top Bottom