GE2025 Chief Justice George Masaju's Speech Towards the 2025 General Election in Tanzania

GE2025 Chief Justice George Masaju's Speech Towards the 2025 General Election in Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
NA HAYO NDO MAAGIZO KUTOKA JUU.
22/9/025 MAJAJI WATATEMBELEA HUMO. MAHAKAMA HAITARUHUSU URUSHWAJI MUBASHARA.
TAYARI KAWAELEKEZA CHAKUFANYA.
Ni makusudi kabisa kwasababu angeongelea mtu mwingine tungeambiwa anaingilia uhuru wa Mahakama.

CHADEMA, mwelezeni TAL kwamba Jumatatu aondoe shauri lake, hukumu imeshatolewa na Jaji Mkuu

So sad! kama kuna taasisi zilizoingiliwa , Mahakama imegeuzwa ''Jumuiya'' . Lakini ndiyo iliyopo!

Kitu cha kwanza cha kudai si Tume ya Uchaguzi, ni uhuru wa Mahakama. Tuna tatizo kubwa sana
 
Mkuu
Jaji mkuu amezungumzia Mahakama kusimamia utawala wa sheria ili mamlaka itoke kwa Wananchi.
Amezungumzia vifungu mbali mbali kana kwamba ndicho Wananchi wanacholalamikia.

Jaji Mkuu antambua malalamiko ya Wananchi si mamlaka ya kimahakama bali Mahakama kutelekeza mamlaka yake na kutumiwa na wanasiasa kufanya maamuzi. Huu ndio ukweli alioukwepa lakini anaujua.

Kuhusu kesi kuendeshwa mubashara, jana Tundu Lissu aliwakumbusha Majaji 3 . Jibu alilopewa ni kwamba wanalifanyia kazi. Leo Jaji mkuu kaenda Lushoto kuwapa maagizo kijanja, kwamba, uhuru wa kupata habari si uhuru wa kurusha mubashara.

Alichokisema Jaji mkuu ni ''hukumu'' ya shauri la Lissu. Wiki ijayo utasikia majaji 3 waki 'echo' kauli ya Jaji mkuu.

Mafunzo yanayoendelea kuhus uchaguzi ni kupoteza fedha za umma, tatizo ni Mahakama kupokwa Uhuru.

Kalamu
Sijui kwa nini nilikuwa na matumaini juu ya huyu Jaji Mkuu!

Kwamba angalau tungeanza kuona mabadiliko juu ya mwenendo wa mahakama zetu.
Sasa jambo dogo kabisa kama hili la mahakama kuamua kuonyesha mbashara kesi nalo linakuwa nongwa?
Anamwogopa nani; yeye siyo mkuu wa taasisi hiyo?
Kwa nini apewe maagizo kwenye swala ambalo ni la uamzi wake yeye na wenzake huko mahakamani?

Sasa kama hilo haliwezekani, njia iliyo baki ni hiyo moja tu, ya wananchi kuyalazimisha mabadiliko kamili katika mfumo wa utawala wa nchi yetu.

Kamwe hatuwezi kuendelea na mfumo huu uliopo sasa, halafu tuendelee kuamini kwamba tunayo nchi yenye heshima.
 
Huyu jaji mkuu anapiga porojo tu . Ndiyo kusema:-
...hauoni ubovu wa katiba yetu?
...haoni majaji wakitumiwa na rais kama toilet paper ktk mahakama?
.,.haoni tatizo katiba kumpa rais madaraka makubwa ya kimwmlaka na mkono mrefu wa uteuzi?

...hajaona katiba ya sasa haisapoti mfumo wa vyama vingi?
 
..George Masaju ndio alikuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati Magufuli akifungia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani.
Hivyo!
Asante kwa kukumbushia hili.

Pamoja na kuwa hivyo; sasa fikiria 'contradiction' iliyopo wakati akitetea ya wakati huo, na haya ya sasa inayobidi nayo ayatete vilevile!

Hizi ni dalili zilizo wazi kabisa, kwamba 'overhaul' ya kila kitu ni lazima itokee.
Haiwezekani kurekebisha yote haya kwa ku'tinker' hapa na pale.
 
Matukio katika picha wakati Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipokutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.

19 September 2025

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetangaza maandamano ya amani


Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Kanda ya Mbeya kimetangaza maandamano ya amani yatakayofanyika Jumatatu, Septemba 22, 2025, kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya hadi Mahakama Kuu Masijala ya Mbeya.

Kupitia barua rasmi iliyotumwa kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mbeya, Mwenyekiti wa TLS Kanda hiyo, Philip Mwakilima, amesema maandamano yataanza saa tatu asubuhi na kuhitimishwa saa nane mchana.

Kwa mujibu wa msomi Mwakilima, lengo la maandamano hayo ni kufikisha ujumbe kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Masijala ya Mbeya kufuatia tukio la kudhalilishwa na kushambuliwa kwa wakili msomi wa mahakama kuu Deogratias Mahinyila mnamo Septemba 15, 2025 katika eneo la Mahakama Kuu Dar es Salaam alipokuwa akitekeleza majukumu yake.

Aidha, amebainisha kuwa takribani mawakili 200 wanatarajiwa kushiriki, huku maandalizi yakiwa yamefanyika kuhakikisha usalama na nidhamu ili kuzuia usumbufu au uvunjifu wa sheria.Katika hatua nyingine, TLS Kanda ya Mbeya imeomba ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi ili maandamano hayo yafanyike kwa utulivu na amani.
Source : X
 
20 September 2025
MBEYA PROTEST | MBEYA LAWYERS | RUKWA AND SONGWE PROTEST TO THE HIGH COURT TO DELIVER THEIR MESSAGE


View: https://m.youtube.com/watch?v=VmNc9TDDad8

TLS Tanganyika Law Society Mbeya chapter protest against police brutality in Tanzania after one of their own members was beaten up in the vicinity of the High Court of Tanzania ...
 
..Jaji Mkuu anapaswa kujiongeza.

..kuendelea kutoa taarifa za muenendo wa mashauri kupitia magazeti ni kukumbatia ujima.

..Teknolojia ya habari imebadilika na mahakama nayo inapaswa kwenda na wakati.

..Jaji Mkuu hana sababu yoyote ile ya msingi ya kukataa matangazo mubashara ya mahakama zetu.

..Mahakama iruhusu Televisheni binafsi kurusha matangazo ya kesi mbalimbali.

Cc Nguruvi3
Unajuwa wanacho ogopa?
Hawana namna ya ku'filter' na kuondoa wasichokitaka kiwafikie wananchi. Magazeti yote wanafanya hivyo.
 
Dar es Salaam, Tanzania

Tanganyika Law Society (TLS) called for a nationwide protest on September 19, 2025

View: https://m.youtube.com/watch?v=8rjJbZfwcEg
Meanwhile The Tanganyika Law Society (TLS) called for a nationwide protest on September 19, 2025, to condemn the assault on lawyer Mahinyila at the Dar es Salaam High Court and other instances of police brutality against lawyers and citizens.

The nationwide protest aims to address the growing threat to the legal profession and the rule of law in Tanzania, following the condemnation of police violence by TLS President Boniface Mwabukusi.
 
20 September 2025

Wakili Peter Madeleka acharuka Mahakana na Mfumo wa Haki Jinai kunajisiwa

Haki na Ustawi wa watu Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ovsilh5r_xQ

Katiba sura 107 A inatamka kuwa Mahakama ni Mlinzi wa haki za watu, wakili Peter Madeleka anaendelea ni busara ninikuu kitabu cha Mithali 28: 16 kutoka Biblia - "Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana" mwisho wa kunukuu ...

Hati ya mashtaka chargesheet kubadilishwa / amended chargesheet ... sheria ya muenendo wa mashtaka CPA ...

DPP Mkurugenzi wa Mashitaka ...mahakama ya kiuchunguzi Kisutu ...

Kauli mbiu ya Kazi na Utu inayosisitizwa anasema wakili Peter Madeleka kuwa inachezewa, tulipofika Mahakama Kuu mbele ya jaji Philip kwa hati ya dharura ...

Wakili Peter Madeleka polisi walitaka kumkamata mteja wangu akiwa ndani ya mahakama, nikakataa na kufunga mlango wa ofisi ya mahakama kuzuia ukiukwaji wa taratibu za uhuru wa mahakama unaofanywa na mapolisi waliotumwa na wakubwa wao...
 
Unajuwa wanacho ogopa?
Hawana namna ya ku'filter' na kuondoa wasichokitaka kiwafikie wananchi. Magazeti yote wanafanya hivyo.

..Jaji Mkuu kama ana nia ya dhati ya kudhibiti Majaji wake na kulinda heshima ya mahakama basi aruhusu televisheni kuingia mahakamani.
 
..Jaji Mkuu kama ana nia ya dhati ya kudhibiti Majaji wake na kulinda heshima ya mahakama basi aruhusu televisheni kuingia mahakamani.
Ni kama anajihisi kuwa hana mamlaka ya kufanya hivyo!
 
..Jaji Mkuu kama ana nia ya dhati ya kudhibiti Majaji wake na kulinda heshima ya mahakama basi aruhusu televisheni kuingia mahakamani.
Anaogopa hatakuwa na uwezo wa kuficha maouvu ya Mahakama ! fikiria TAL anavyowapelekesha, sasa ikiwa 'live' si dhahma kwao! Ni yale yale ya kugeuza mahakama tawil la Chama likipokea maagizo kutoka juu

Masaju ni ''mwanafunzi'' wa Ibrahim Juma aliyeinajisi Mahakama kwa mengi ikiwemo kufanya kazi kama kibarua (Probation). Yaani CJ wa kwanza kuajiriwa kama kibarua ! tangu hapo mahakama haija recover! ni damage tu
 
Jaji Mkuu Masaju anazungumza siasa tu yaani anazungumza kila watu wanataka kusikia lakini bila uhalisia au dhamira ya kutenda. Mhimili wa Mahakama hapa Tanzania uko kwenye handbag ya Samia.
 
19 September 2025

VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA WALIPO MTEMBELEA JAJI MKUU OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA​



View: https://m.youtube.com/watch?v=yXqa4J5sp_Y

Jumamosi, 20 Septemba 2025​

USHIRIKIANO KATI YA MAHAKAMA YA TANZANIA NA JESHI LA MAGEREZA WAZAA MATUNDA​

· Kamishna Mkuu wa Magereza asema umepunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya malalamiko ya Wafungwa, Mahabusu

· Waipongeza Mahakama kwa kuondoa zaidi ya asilimia 80 ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili Wafungwa na Mahabusu

· Asema idadi ya Mahabusu yapungua na hakuna Mahabusu wa Mahakama za Mwanzo gerezani

· Wapongeza matumizi ya Mahakama Mtandao ambapo zaidi ya mashauri 10,000 yamesikilizwa kwa njia hiyo
Na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma


Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Jeremia Yorum Katungu ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoupatia Jeshi hilo ambao umewezesha kupatikana kwa mafanikio lukuki ikiwemo kupungua kwa idadi ya malalamiko ya Wafungwa na Mahabusu.

CGP Katungu alieleza hayo jana tarehe 19 Septemba, 2025 alipomtembelea Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma lengo likiwa ni kusalimiana na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali kwa ustawi wa utendaji kazi wa vyombo hivyo.

“Matokeo ya ushirikiano huu Mhe. Jaji Mkuu, kwanza magerezani kumekuwa na kupungua kwa malalamiko ya wafungwa na mahabusu kuhusiana na changamoto za mashauri, miaka ya nyuma ilikuwa ukiingia gerezani unaweza kusikiliza malalamiko kuanzia asubuhi mpaka jioni malalamiko yalikuwa mengi sana, lakini sasa hivi nikuhakikishie malalamiko sio kwamba tumeyamaliza yote lakini yamepungua kwa kiasi kikubwa sana na tafsiri yake ni kwamba ni ushirikiano uliopo katika utatuzi wa malalamiko hayo ambayo yamefanya wafungwa na mahabusu kuridhika na hivyo kusababisha utulivu gerezani,” alisema Kamishna Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza.

CGP Katungu alishukuru kwa dhati ushirikiano huo ambao umekuwepo kati ya Mahakama pamoja na Jeshi la Magereza na kukiri kuwa, kumekuwa na ziara za mara kwa mara za Majaji na Mahakimu akiwemo Jaji Mkuu ambaye alifanya ziara yake ya kwanza katika Gereza la Isanga tarehe 10 Julai, 2025.

Kamishna Mkuu huyo alikiri kwamba, ziara hizo zimekuwa na manufaa mengi ikiwemo ushughulikiaji wa mashauri ya wafungwa na mahabusu.

“Usikilizaji wa mashauri ya wafungwa na mahabusu kupitia Mahakama Mtandao ni eneo ambalo pia tumekuwa tukishirikiana vizuri, kama utakumbuka miezi kadhaa iliyopita mlitusaidia kutupa makasha 10 ambayo yanatumika kama vyumba vya Mahakama mtandao lakini pia mmeendelea kutusaidia vifaa vya TEHAMA ambavyo vinatumika kwenye Mahakama mtandao kwakweli tunashukuru katika eneo hilo na tumeendelea kuona ufanisi katika usikilizaji wa mashauri kupitia Mahakama mtandao,” alieleza CGP Katungu.

Kamishna Mkuu huyo wa Magereza alisema kwamba, kuanzia mwaka 2021 ndipo ulianza ushirikiano wa huduma ya wafungwa na mahabusu kusikiliza mashauri yao kwa njia ya Mahakama Mtandao ambapo kufikia Septemba, 2025 huduma ya Mahakama mtandao imeendelea kutolewa katika vituo 97 na mpango uliopo ni kuwa na huduma hiyo katika Magereza yote nchini.

“Katika kipindi cha mwaka 2021 mpaka sasa, zaidi ya mashauri 10,000 yamesikilizwa kwa njia ya huduma ya Mahakama Mtandao katika Vituo hivyo 97 na baadhi maamuzi yamefanyika kwa utaratibu wa Mahakama mtandao na hii kwakweli imekuwa na manufaa sana kuondokana na changamoto za ucheleweshaji wa mashauri,” alisema CGP Katungu.

Aliongeza huku akirejea maelekezo ya Jaji Mkuu alipofanya ziara katika Gereza la Isanga tarehe 10 Julai mwaka huu kuhusu kuondoa mahabusu wa Mahakama za Mwanzo gerezani kwamba maelekezo hayo yamefanikiwa kwa ufanisi mkubwa na sasa.

“Nikupongeze kwa dhati kabisa, maelekezo hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, tumekuwa na mawasiliano ya karibu sana na watendaji wako kuhusu suala hili na matokeo yanaonekana, sasa ulipokuja Gereza la Isanga kulikuwa na Mahabusu 6, 415 lakini kwa tarehe 18 Septemba, 2025 idadi ya mahabusu waliopo ni 4,658, utaona kuna idadi ya zaidi ya mahabusu 1,757 wamepungua na hayo ni matokeo ya ziara ambayo ulifanya na maelekezo uliyotupa ambayo utekelezaji wa maelekezo yako umeanza kuzaa matunda, na kitu cha kujivunia sana ni kwamba, tunavyozungumza sasa Mahabusu wa Mahakama za Mwanzo hatuna magerezani,” alieleza.

Aliongeza kuwa, Mahakama na Magereza inashirikiana pia ni katika eneo la kubadilishana taarifa ambapo alirejea maelekezo ya Jaji Mkuu alipofanya ziara katika Gereza la Isanga ambapo pamoja na mambo mengine aliomba kupatiwa taarifa za kila siku za idadi za Wafungwa na Mahabusu waliopo katika magereza mbalimbali nchini, amesema kazi hiyo wanaitekeleza kwa dhati kwa kuwa manufaa yake wameanza kuyaona ikiwemo kupungua kwa mashauri pengine hayakuwa na ulazima wa kukaa kwa muda mrefu.

“Lakini kuna kupungua kwa idadi ya waliopo gerezani hususani Mahabusu, Mhe. Jaji Mkuu nitoe tu takwimu kidogo ulifanya ziara tarehe 10 Julai, 2025, maelekezo uliotoa tunaendelea kuyatekeleza, lakini wakati unafanya ziara ile idadi ya wafungwa na mahabusu ilikuwa 25,784 lakini hadi kufikia tarehe 18 Julai mwaka huu idadi ilikuwa 24,761 kwahiyo idadi imepungua hususani ya mahabusu na kwamba Serikali imepunguza gharama kubwa ya kuwahudumia mahabusu na wafungwa,” alisema CGP Katungu.

Aidha, alizungumzia kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na vikao vya Mahakama Kuu kuchukua muda mrefu kufanyika, changamoto ya kupatikana kwa mtandao kwenye Mahakama mtandao, mahitaji ya vifaa vya TEHAMA,

“Magereza mengi hayana miundombinu inayowezesha urekebishaji wa wafungwa, kuna haja ya kuwa na viwanja vya michezo na burudani ndani ya viwanja vya Magereza, kuna haja pia ya kuwa na vyumba maalum vya kutumika kama madarasa. Kwahiyo sasa hivi magereza nyingi tunazojenga tunajitahidi kuweka miundombinu muhimu itakayowezesha urekebishaji,” alisema.

Kamishna Mkuu huyo alieleza kuwa, kuna changamoto ya baadhi ya Wilaya kukosa Magereza na kwamba lengo ni Wilaya zote ziwe na Magereza ili kurahisisha usafirishaji wa wafungwa na mahabusu. Ameongeza kwamba kwa sasa kuna ujenzi unaendelea wa jumla ya magereza 12.

Aliongeza kwamba vitendea kazi bado ni changamoto hasa magari, Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kununua magari na hivi karibuni wamepokea jumla ya magari 10 aina Land Cruiser pick up 10.

Naye, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza kutoka Jeshi Magereza nchini (CP) Nicodemus Tenga alisema kuwa, kwa sasa Jeshi hilo lina Wanasheria zaidi ya 264 na wamesambazwa kwenye vituo mbalimbali vya Magereza ikiwemo Magereza ya mikoani na wilayani.

Aidha, CP Tenga ameishukuru Mahakama kwa kuwafundisha wanasheria hao jinsi ya kutumia Mfumo wa Kieletroniki wa Usimamizi wa Mashauri (e-CMS) na kuwezesha magereza zote nchini kutumia mfumo huo na kuondokana na matumizi ya karatasi na imesaidia kupungua zaidi ya asilimia 80 ya changamoto kufuatia matumizi ya mfumo.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Magereza nchini, naye Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju alimpongeza Kamishna huyo kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya ambayo matokeo yanaonekana.

“Niwapongeze kwa haya mambo makubwa ambayo mmekuwa mkiyafanya naona unayatekeleza kwa kiwango kikubwa sana licha ya changamoto, nashukuru sana kwa hii taarifa ambayo umetupatia ni taarifa ambayo imejitosheleza ambayo itatusaidia sisi kuboresha huduma zetu ili kuhakikisha kwamba wajibu wetu katika utekelezaji wa haki jinai unatekelezwa kwa ufanisi ipasavyo,” alisema Mhe. Masaju.

Jaji Mkuu alisema kwamba, kuna umuhimu mkubwa wa kuwa ushirikiano na uhusiano mzuri baina ya Wadau wa Haki Jinai wakiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Jeshi la Polisi, TAKUKURU, Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya, Jeshi la Uhamiaji na wananchi ambalo lengo lake ni kupata na kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi kila sehemu ili lengo lililokusudiwa lifanikiwe.

Aidha, Mhe. Masaju amemtaka Kamishna huyo kuwa kama kuna changamoto zozote zinazohusu Mahakama ambazo zitaendelea kujitokeza asisite kuijulisha Mahakama na kwamba kwa sasa hatatembelea Magereza hadi atakapohakikisha kuwa changamoto zilizopokelewa wakati wa ziara yake katika Gereza la Isanga zifanyiwe kazi/ziishe.

“Nawashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao mmeendelea kutupatia hususani utoaji taarifa, na kwamba kuna taarifa au changamoto zaidi msisubiri tuwaombe nyie andikeni tuyafanyie kazi,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Aidha, amewashauri Viongozi hao wa Jeshi la Magereza kushughulikia mapema mapema maombi ya wafungwa wanaosubiri msamaha wa Rais kwa sababu kuna Kamati mahsusi ya kumshauri Rais kuhusu msamaha kwa wafungwa wanaosubiri adhabu ya kifo kwa kufuata utaratibu husika, kwa sababu itasaidia kupungua idadi ya wafungwa.

Aidha, Mhe. Masaju amemuomba Kiongozi huyo wa Jeshi la Magereza kuandaa taarifa kuhusu utekelezaji wa Kifungu cha 134 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, ili kujua kama kweli mashauri hayo yanamalizika ndani ya miezi sita.

“Tunatengeneza pia Kanuni ambazo zitawezesha katika mashauri yanayosikilizwa na Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Wilaya wao nao Mahakama na washtakiwa wawe nao sasa wanapata ushahidi wa upande wa kesi za mashtaka ili iwasaidie na wao kujitetea kwa ufanisi ipasavyo, haitoshi tu kwamba kumpa haki ya kusikilizwa lakini akiwa hana taarifa za tuhuma na ushahidi uliopo dhidi yake hapo hakutakuwa na haki ya kusikilizwa aliyopewa itakuwa imenyofolewa kwa kiasi fulani na itakuwa inakiuka Ibara ya 13 ya Katiba inayotaka usawa mbele ya sheria,” alisisitiza Jaji Mkuu.

Kadhalika, Mhe. Masaju alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi kubwa ya urekebishaji wanaofanya na kulishauri Jeshi hilo kuangalia uwezekano wa kuwarudisha hadi mipakani wafungwa kutoka nchi za Jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanamaliza kutumikia mifungo vyao badala ya kuendelea kujaza idadi ya wafungwa magerezanina kuwa na wahamiaji haramu nchini.
Source : tanzaniajudiciary.blogspot
 
Back
Top Bottom