Chief kalumana inasemekana amakamatwa na polisi akiwa eneo la kuapishwa mawakala na mawakala wa chadema hawajaapishwa hadi sasa.
=====
Jeshi la polisi mkoani Kagera limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na mgombea ubunge jimbo la Bukoba Mjini, Chief Karumuna baada ya kugomewa kuapishwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Bukoba mjini Mourice Limbe.
Mgombea huyo aligoma kutoka katika eneo la uwanja wa Kaitaba mara baada ya zoezi la kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa kukamilika akitaka wagombea nao waapishwe kauli iliyopingwa na msimamizi wa uchaguzi akisema wao wataapishwa kwa pamoja siku ya kesho.
Tundu Lissu atoa tamko: Figisu za uchaguzi zimeanza, Mawakala wa CHADEMA wakataliwa kuapishwa
Tundu Lissu afafanua lazima wasimamizi wa uchaguzi wazingatie Kifungu cha 7.4 Kanuni kuhusu mawakala wa wagombea wa vyama baada ya kujaza fomu namba 6 zinasema ngazi ya Kata inaweza kufanya zoezi la kuapisha na siyo lazima ifanyike ktk ngazi ya mkurugenzi