Sky,
Napenda kuchangia kidogoniyajuayo kuhusu
Chief David Kidaha Makwaia.
Kwanza mimi nilipata bahati ya kukutana na
Chief Kidaha hapa Dar es Salaam
mwaka wa 1968.
Mwanae
Edward Makwaia nilikuwa nasomanae darasa moja St. Josephs Convent
School basi siku moja akaniambia kuwa baba yake amekuja kutoka Nairobi kwa
hiyo nimsindikize kwenda kumwamkia.
Hivi ndivyo nilivyobahatika kumuona
Chief Kidaha.
Lakini wakati ule mimi mtoto sikuwa najua kwa nini
Chief Kidaha alikuwa anaishi
Kenya.
Chief Kidaha baada ya uhuru aliwekwa kizuizini Tunduru kupitia Preventive Dentition Act ya 1962 na baada ya kutoka aliamua kuhama nchi na kwenda Kenya.
Chief Kidaha Kidaha ni mtoto wa
Chief Makwaia Mohamed Mwandu wa Busiya.
View attachment 1191693
Chief Makwaia Mohamed Mwandu Nimeona tangazo la Busiya Chiefdom katika mitandao ya kijamii na nikaangalia, ‘’clip,’’ yake. Hili ni ta...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha
Abdul Sykes katika miaka ya 1980s nilikutana na
Chief Kidaha Makwaia kwenye
Nyaraka za Sykes kupitia barua aliyoandika
Dr. Wilbard
Mwanjisi.
Dr. Mwanjisi alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika African Government Servant
Association (TAGSA) mwaka wa 1951 aliandika makala kali sana katika jarida la chama, makala ambayo aliwashambulia Waingereza kiasi
Rashid Kawawa akiwa mwanakamati wa Halmashauri Kuu ya TAGSA aliandika barua kuonya kuwa makala hiyo isichapwe bila ya kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya TAGSA.
Katika makala hii
Dr. Mwanjisi aliitaja hotuba ya
Chief Kidaha Makwaia ndania ya LEGCO
kuwa ni hotuba muhimu sana na akamsifia
Chief Kidaha Makwaia kuwa ni mwanasiasa
makini wa kupigiwa mfano (‘
Doctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December, 1951
(
Sykes' Papers),
Katika hotuba hiyo
Chief Kidaha alikuwa anaishauri serikali ya Kiingereza kuondoa ile sheria ambayo ilikuwa inawapiga marufuku Waafrika wafanyakazi wa serikali kujishughulisha na siasa.
Kitu ''interesting,'' katika kipindi hiki ni kuwa
Chief Kidaha alikuwa na mazungumzo na Katibu wa TAA,
Abdul Sykes, mazungumzo haya yakifanyika nyumbani kwa
Abdul Sykes,
Abdul akijaribu kumshawishi
Chief Kidaha aingie TAA ili wamchague kama Rais kisha waunde TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Mazungumzo haya hayakufanikiwa.
Baada ya uhuru
Dr. Mwanjisi na yeye aliwekwa kizuizini na kama alivyofanya
Chief Kidaha baada ya kutoka kizuizini alikwenda kuishi Kenya.
Na bahati mbaya sana waandishi wa historia ya TANU hawakutaka kufanya mahojiano yoyote
na marehemu
Ally Sykes katika historia ya TANU na kwa hili historia iliyokuja kuandikwa ikakosa mengi muhimu katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Hii ndiyo sababu
Chief Kidaha Makwaia haonekani kokote katika historia ya kudai kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Ningependa kuhitimisha kwa kueleza kuwa baada ya kutawazwa kwa
Malkia Elizabeth, uongozi wa TAA ulituma salamu za pongezi kwa Malkia kwa kutawazwa kwake barua ya pongezi ilitiwa sahihi na Rais wa TAA
Julius Nyerere, Makamu wa Rais
Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu
Dome Okochi Budohi, Naibu Katibu
Dossa Aziz, Mweka Hazina
John Rupia, Naibu Mweka Hazina
Ally Sykes.
View attachment 1191697
Chief David Kidaha Makwaia