View attachment 1191675
David Kidaha Makwaia Pichani, yupo na mwingereza Lord Iveagh siku ya kutawazwa kwa malkia Elizabeth mwaka 1956.
Chifu David kidaha, alikuwa ni chifu wa wasukuma, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 ,alikuwa ndio ngazi kati ya ukoloni na machifu ,na baada ya ukoloni barani Afrika na pia alikuwa na urafiki mkubwa na Gavana wa Tanganyika toka mwaka 1949 hadi 1958, Lord Twining.
Mwakwaia alicheza katikati ya viongozi wa Kiingereza na machifu wa majimbo kadhaa ya Tanganyika, alishuhudia Kipindi cha mpito cha Afrika mashariki kutoka kipindi cha ubeberu hadi baada ya Uhuru.
Makwaia alizaliwa na kuwa muislamu akiwa ni mtoto wa Chifu wa kisukuma ,Makwaia Ng'wandu wa Bwiha Mkoa wa Shinyanga Tanganyika, alijifunza kilimo katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwanzoni mwa miaka ya 1940 Kabla ya kuingia Chuo cha Lincoln, Oxford ,ambapo alisoma kanuni na utendaji wa Serikali za mitaa ,Falsafa na Siasa.
Maisha ya Makwaia kisiasa yalitoa fursa nyingi katika dunia ya viongozi wa kikoloni Tanzania ,na viongozi wa kikabila ,alimpokea Baba yake uchifu wa Busiha mwaka 1945 na baadae akaja kuwa chifu mkubwa wa wasukuma ,Taasisi yenye zaidi ya machifu 50 ,yenye ofisi yake na bendera kupitia hili akatambulika kwa waingereza kama sauti ya mzawa mwenye mamlaka ,mwaka huohuo akachaguliwa kuwa kati ya wabunge wawili waafrika kwenye baraza la kutunga sheria (Legco).
View attachment 1191674