Chief Kidaha Makwaia alituwakilisha siku ya kuapishwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza

Chief Kidaha Makwaia alituwakilisha siku ya kuapishwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza

Nyerere alikuwa na quality zifuatazo

1. Charm/Bashasha
Nyerere alikuwa na uwezo wa kukufanya ujifeel so good around him, kwa jokes, tabasamu.

2. Sharp mind
Nyerere alikuwa ana akili inayofanya kazi fasta sana, alikuwa na uwezo wa kutambua gaps kwenye hoja za wenzie na kuzitumia against wao. Na kama hoja ina mashiko alikuwa ana uwezo wa kumfanya mwenye hoja asijiamini

3. Alikuwa ni mtaalam wa kusuka alliances
Pindi akiona kuwa anahitaji uungwaji mkono katika jambo lake alikuwa na uwezo wa kutafuta kuungwa mkono mapema kabisa kabla hajaleta hoja barazani. Ukifuatilia harakati za uhuru utaona jinsi alivyokuwa akiwapanga wajumbe wanaojua kuzungumza kiswahili vizuri mapema ili hoja ikiletwa mezani then mmoja baada ya mwingine wanaanza kusimama na kuitetea.
Hata alivyomsaidia Mkapa kumshinda JK ndani ya CCM ni. kutokana na uwezo wa Nyerere kuwashawishi wajumbe wa Zanzibar wamuunge mkono.

4. Alikuwa ni mobilizer mzuri
Viongozi wenye kufuata mirengo ya kijamaa huwa ni wazuri kwenye kumobilize masses, Hata Nyerere alikuwa na kipaji cha kurally Taifa zima kusapoti agenda zake kama vile kuvunjilia mbali mfumo wa kichifu, Kuondoa mifumo ya nyarubanja, kumpiga Iddi Amini, Kuunga mkono azimio etc

Udhaifu wa Nyerere
1. Alipenda sana power
Ndo maana reform za msingi za kumpunguzia rais madaraka aliziintroduce alipokuwa anakaribia kung'atuka au akiwa ameng'atuka

2. Wakati mwingine Ukatoliki wake ulimshinda nguvu kwenye fairness

Hii inadhihirishwa na kuamua kuitia nchi katika kuunga mkono waasi wa Biafra, baadhi ya wachambuzi wanaeleza kuwa hii ni kutokana na Biafra kuwa inaungwa mkono na Vatican kutokana majority huko kuwa ni wakatoliki.

3. Alikuwa stubborn
Pindi alipokuwa akiamini kitu alikuwa hakubali mawazo mbadala kirahisi, mfano mzuri ni sera zake za uchumi baada ya azimio la arusha, zilikuwa za populism zaidi

4. Alikuwa mwema kwa loyalists hata kama wanaharibu
Kipindi cha Nyerere so long as una imani na CCM na yeye na wala humchsllenge kutishia power yake au ya chama, pindi ukiharibu kazini basi ungeweza kuhamishiwa shirika jingine
Nyerere alifeli kwenye elimu na kuandaa mfumo wa uchumi.
 
Chief Makwaia Baba yake David Makwaia,alikuwa mjomba wa Bob Makani. Mama Yake Bob Makani ni mtoto wa Chief.
For real? Familia kubwa, nilikaa na mtoto mmoja wa Chief David Makwaia alikuwa anamchana Bob Makani kama pretender, alisema kwamba the Makanis ni majirani tu wa kwao kwenye Uchifu lakini wana pass off kama watu wa line ya Uchifu.

Naweza kumtafuta mtu anieleze vizuri hapa.

Halafu hapa JF tunaweza kuwa tunajibizana ndugu.
 
For real? Familia kubwa, nilikaa na mtoto mmoja wa Chief David Makwaia alikuwa anamchana Bob Makani kama pretender, alisema kwamba the Makanis ni majirani tu wa kwao kwenye Uchifu lakini wana pass off kama watu wa line ya Uchifu.

Naweza kumtafuta mtu anieleze vizuri hapa.

Halafu hapa JF tunaweza kuwa tunajibizana ndugu.
Ni kweli kabisa. Chief Makwaia na mama yake Bob ni mtu na dada yake. Uliza. Hata mama yake Bob alipofariki alizikwa huko Negezi kwenye makazi ya Chief Nhw'aya Makwaia. Pia huyo bibi alikuwa anaitwa Ng'wana Nh'waya. Baba yao alipokufa mzee Kidaha David Makwaia,ambae mwanae yupo pale BOT IT department akawa chief. Baadae na yeye alipokufa Edward makwaia akawa chief,na ndo anaendelea mpaka leo.
Ila si unajua familia za kisukuma watoto wa Ujombani ni kama wa kuja tu.
 
For real? Familia kubwa, nilikaa na mtoto mmoja wa Chief David Makwaia alikuwa anamchana Bob Makani kama pretender, alisema kwamba the Makanis ni majirani tu wa kwao kwenye Uchifu lakini wana pass off kama watu wa line ya Uchifu.

Naweza kumtafuta mtu anieleze vizuri hapa.

Halafu hapa JF tunaweza kuwa tunajibizana ndugu.
Ha ha ha ha aaaaf unakuta mmoja anaandikia sebuleni na mwingine yupo chumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sky,
Napenda kuchangia kidogo niyajuayo kuhusu Chief David Kidaha Makwaia.

Kwanza mimi nilipata bahati ya kukutana na Chief Kidaha hapa Dar es Salaam
mwaka wa 1968.

Mwanae Edward Makwaia nilikuwa nasomanae darasa moja St. Josephs Convent
School basi siku moja akaniambia kuwa baba yake amekuja kutoka Nairobi kwa
hiyo nimsindikize kwenda kumwamkia.

Hivi ndivyo nilivyobahatika kumuona Chief Kidaha.

Lakini wakati ule mimi mtoto sikuwa najua kwa nini Chief Kidaha alikuwa anaishi
Kenya.

Chief Kidaha baada ya uhuru aliwekwa kizuizini Tunduru kupitia Preventive Dentition
Act ya 1962 na baada ya kutoka aliamua kuhama nchi na kwenda Kenya.

Chief Kidaha Kidaha ni mtoto wa Chief Makwaia Mohamed Mwandu wa Busiya.

View attachment 1191693


Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes katika miaka ya 1980s nilikutana na
Chief Kidaha Makwaia kwenye Nyaraka za Sykes kupitia barua aliyoandika Dr. Wilbard
Mwanjisi.

Dr. Mwanjisi
alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika African Government Servant
Association (TAGSA) mwaka wa 1951 aliandika makala kali sana katika jarida la chama, makala ambayo aliwashambulia Waingereza kiasi Rashid Kawawa akiwa mwanakamati wa Halmashauri Kuu ya TAGSA aliandika barua kuonya kuwa makala hiyo isichapwe bila ya kujadiliwa na Halmashauri Kuu ya TAGSA.

Katika makala hii Dr. Mwanjisi aliitaja hotuba ya Chief Kidaha Makwaia ndania ya LEGCO
kuwa ni hotuba muhimu sana na akamsifia Chief Kidaha Makwaia kuwa ni mwanasiasa
makini wa kupigiwa mfano (‘Doctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December, 1951
(Sykes' Papers),

Katika hotuba hiyo Chief Kidaha alikuwa anaishauri serikali ya Kiingereza kuondoa ile sheria ambayo ilikuwa inawapiga marufuku Waafrika wafanyakazi wa serikali kujishughulisha na siasa.

Kitu ''interesting,'' katika kipindi hiki ni kuwa Chief Kidaha alikuwa na mazungumzo na Katibu wa TAA, Abdul Sykes, mazungumzo haya yakifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes, Abdul akijaribu kumshawishi Chief Kidaha aingie TAA ili wamchague kama Rais kisha waunde TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Mazungumzo haya hayakufanikiwa.

Baada ya uhuru Dr. Mwanjisi na yeye aliwekwa kizuizini na kama alivyofanya Chief Kidaha baada ya kutoka kizuizini alikwenda kuishi Kenya.

Na bahati mbaya sana waandishi wa historia ya TANU hawakutaka kufanya mahojiano yoyote
na marehemu Ally Sykes katika historia ya TANU na kwa hili historia iliyokuja kuandikwa ikakosa mengi muhimu katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu Chief Kidaha Makwaia haonekani kokote katika historia ya kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Ningependa kuhitimisha kwa kueleza kuwa baada ya kutawazwa kwa Malkia Elizabeth, uongozi wa TAA ulituma salamu za pongezi kwa Malkia kwa kutawazwa kwake barua ya pongezi ilitiwa sahihi na Rais wa TAA Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi Budohi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes.

View attachment 1191697
Chief David Kidaha Makwaia
Mzee kumbe unaweza kuandika historia ya nchi vizuri bila kuinasibisha na mambo ya imani!
This is awesome
 
Chief Makwaia Baba yake David Makwaia,alikuwa mjomba wa Bob Makani. Mama Yake Bob Makani ni mtoto wa Chief.

..Major.Makwaia aliyepata kuwa mpambe wa Mwalimu Nyerere ana uhusiano wowote na Chief Makwaia?
 
Nadhani hii ni moja kati ya historia muhimu zilizofichwa makusudi katika siasa za kudai uhuru wa nchi yetu, kwani historia za aina hii zipo nyingi.

Tunataraji sikumoja atatokea mwanahistoria uliyehuru na kuandika upya historia ya kudai uhuru upya bila upendeleo, historia itakayokuwa tunu kwa vizazi vyetu na kutoa heshima kwa wale wote waliochangia vilivyo katika harakati za kudai uhuru lakini kwa makusudi mifumo ilijengwa ili wasahaulike.

It is a high time for dedicated historians to unveil the deliberately hidden history.
Hata baba wa babu yangu Chifu Mfaranyaki wa Songea wamemsahau kwenye vitabu vyao, alipigana sana vita ya majimaji kipindi hicho
 
View attachment 1191675

David Kidaha Makwaia Pichani, yupo na mwingereza Lord Iveagh siku ya kutawazwa kwa malkia Elizabeth mwaka 1956.

Chifu David kidaha, alikuwa ni chifu wa wasukuma, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 ,alikuwa ndio ngazi kati ya ukoloni na machifu ,na baada ya ukoloni barani Afrika na pia alikuwa na urafiki mkubwa na Gavana wa Tanganyika toka mwaka 1949 hadi 1958, Lord Twining.
Mwakwaia alicheza katikati ya viongozi wa Kiingereza na machifu wa majimbo kadhaa ya Tanganyika, alishuhudia Kipindi cha mpito cha Afrika mashariki kutoka kipindi cha ubeberu hadi baada ya Uhuru.

Makwaia alizaliwa na kuwa muislamu akiwa ni mtoto wa Chifu wa kisukuma ,Makwaia Ng'wandu wa Bwiha Mkoa wa Shinyanga Tanganyika, alijifunza kilimo katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda mwanzoni mwa miaka ya 1940 Kabla ya kuingia Chuo cha Lincoln, Oxford ,ambapo alisoma kanuni na utendaji wa Serikali za mitaa ,Falsafa na Siasa.

Maisha ya Makwaia kisiasa yalitoa fursa nyingi katika dunia ya viongozi wa kikoloni Tanzania ,na viongozi wa kikabila ,alimpokea Baba yake uchifu wa Busiha mwaka 1945 na baadae akaja kuwa chifu mkubwa wa wasukuma ,Taasisi yenye zaidi ya machifu 50 ,yenye ofisi yake na bendera kupitia hili akatambulika kwa waingereza kama sauti ya mzawa mwenye mamlaka ,mwaka huohuo akachaguliwa kuwa kati ya wabunge wawili waafrika kwenye baraza la kutunga sheria (Legco).
View attachment 1191674
Halafu jitu linatokea mafichoni linasema wasukuma hawajasoma.
 
Back
Top Bottom