Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..


Kwa nini si lazima kuweka mikataba hii hadaharani?

Kiongozi wa upinzani bungeni anamuwakilisha nani?

Na kwa nini kiongozi wa upinzani bungeni apate nakala zote za mikataba lakini zisiwekwe hadharani?

Je vipi kama serikali ikimnunua kiongozi wa upinzani bungeni na kutaka kupitisha mikataba isiyo na maslahi kwa nchi?
Huoni kwamba kwa kutaka mikataba aonyeshwe kiongozi wa upinzani tu bungeni na isipowekwa wazi (hata a redacted version where say, some sensitive figures pertinent to negotiation are redacted in the public version) unatengeneza a single point of failure?

Je vipi kama kiongozi wa upinzani bungeni hana utaalamu wa kisheria wa kuona mapungufu yaliyo katika mikataba?

Serikali ni nini?
 
Swali linaweza kuulizwa: ni nani aliye mjinga baina yetu? Wao wanaotuambia kuwa mikataba iliyosainiwa ni siri yao tuwaamini au sisi tunaokubali kuwa ni siri tukiamini walichotuambia?

Huwezi kuweka hadharani Mkataba wa kibiashara lazima uwe na njia ya ku safeguarding sensitive information such as financial details, commercial or technological secrets. Tupo kwenye ulimwengu wa Ushindani.Huwezi kuongele mkataba wa project ya gas bila kuweka technological details.

Cha mhimu ni kwanza tuwe na timu ya wazalendo wanaopitia hii mikataba. Na hii itawezekana kwa kuhakikisha kwamba kuna threshold katika negotiation za contracts.

Mfano mimi nina propose tuwe na threshould ya USD 100,000, Any contracts inayofika kwenye hicho kiwango lazima kuwe na wawakilishi kutoka kambi ya Upinzani in the contracting process. Hii itasaidia kuwa na ukweli na watu wenye macho mawili wanaosimamia intests za nchi.

Tatizo tulilonalo sio siri za mikataba bali ni uwezo wa negotioators kusimamia maslahi ya Taifa. Maana hata kama ukiweka mkata wazi wakati umeshapitishwa utaingia kwenye matatizo zaidi.

Upande wa Public, nadhani inabidi itafutwe namna yaku fanya talking points zinazo reflects mikaba bila kuathiri siri za mikataba.
 
maswali yanaweza kuja kivingine na mbinu zikaangaliwa kivingine, narudia tena tatizo ni katiba tu. hamuwezi kufukuzana na sungura kutwa mnazunguka mmbuyu inafika wakati lazima mseme muweke mtego ambao sungura aponyoki tena.

Angaikeni na checks na namna zitavyozibiti mambo bungeni, serikalini na kwenye mihimili ya sheria (polisi, mahakama, wakaguzi etc) kila mmoja awe na ubavu wa kumtishia mwenzake equally (hizo ndio sababu kwengine maraisi wanapelekwa mahakamani kwa kuvunja katiba) lakini habari za majimbo sijui muungano it is just looking for other problems to solve a very simple problem.
 

Nitapoongelea Kiongozi wa upinzani Bungeni nina Imani ni Institution. Kwahiyo ni jukumu la kiongozi wa Upinzani bungeni kupata expertise ambayo itamshauri kuhusu msimamo wa Kambi ya Upinzani kuhusu state ya Mkataba.

Katika ulimwengu wa geo-politics, huwezi kuhakikisha ushindani kwa kuweka mikataba hadharani, pili hii mikataba yote inalindwa na sheria za kimataifa katika nyanja mbalimbali(Project Finance Law is not as straight as you might want it to be). Kama ungekuwa ni mkataba ambao hauko gauided in a sense of Project finance unaweza ukatafuta loopholes kidogo za kuuweka hadharani but in total what you suggesting is not an International Practices.

Mikataba mibovu ni Failure ya Usalama wa Taifa ku-Impliment their dute to Protect Tanzania Economic Intrests, kwahiyo hata ukiweka mikataba hadharani haitasaidia kitu chochote.
 
Nitapoongelea Kiongozi wa upinzani Bungeni nina Imani ni Institution. Kwahiyo ni jukumu la kiongozi wa Upinzani bungeni kupata expertise ambayo itamshauri kuhusu msimamo wa Kambi ya Upinzani kuhusu state ya Mkataba.

Kama unaongelea institution, kuna institution iliyo na authority zaidi ya wananchi?

Katika ulimwengu wa geo-politics, huwezi kuhakikisha ushindani kwa kuweka mikataba hadharani,

Naelewa hili. Ndiyo maana nikatoa mwanya kwa redaction. Sijui kama umeelewa maudhui ya mwanya huu. Kuna vitu havina haja ya kufichwa, kwa mfano, tunajenga bomba la gesi Mtwara mpaka Dar, kampuni gani inajenga na mambo mengine basic kama hayo. Kwa nini ufiche kila kitu kwa sababu ya geopolitics za minutiate details ambazo unaweza kuzi redact katika the public version?

pili hii mikataba yote inalindwa na sheria za kimataifa katika nyanja mbalimbali(Project Finance Law is not as straight as you might want it to be).

Kwa hiyo hakuna nchi ambayo imeweka mikataba hii wazi?

Kama ungekuwa ni mkataba ambao hauko gauided in a sense of Project finance unaweza ukatafuta loopholes kidogo za kuuweka hadharani but in total what you suggesting is not an International Practices.

What is "an International Practices" (sic)? Practice gani exactly hii, iko dictated na body gani na Tanzania inafungwaje na hii stipulation?

Naomba niwekee link hapa nijifunze na mimi.

Mikataba mibovu ni Failure ya Usalama wa Taifa ku-Impliment their dute to Protect Tanzania Economic Intrests, kwahiyo hata ukiweka mikataba hadharani haitasaidia kitu chochote.

Failure si ya Usalama wa Taifa tu. Ni failure ya process nzima inayo pre-suppose kwamba ukiwapa wabenzi fulani dhamana ya ku vet mikataba hii, watakuwa na national interests at heart.

Wakati wanaweza kuchukua ten percents zao na kusepa, huku wakiachia mikataba mibovu itu cost as a nation.

Solution? Weka mikataba wazi online, wananchi waione na kui discuss na kama kuna haja ya kumsue mtu kwa uzembe watu wa sue.

Hata ikibidi kwa ku redact the most sensitive information ambayo inaweza kuhitaji "need to know" access mimi sioni ubaya kuliko hivi sasa hatujui chochote kuhusu mikataba hii.

Bado hujajibu serikali ni nini. Maana inaonekana kama unatumia the narrow definition of "serikali" kwamba ni wale custodians tu, bila kujua kwamba katika demokrasia serikali ni umma.

Si kama nataka kuwa some anti-business Eva Morales. I even considered the counter points, that would advocate secrecy. In a very balanced piece if I may say so myself.

Here

http://www.vijana.fm/2011/01/18/a-campaign-for-greater-transparency-tanzania-government-contracts/

The final conclusion is we will benefit more from transparency than from secrecy.
 

Mikataba kuwekwa wazi si lazima waione watu wote lakini kuna umuhimu wa wale wenye sababu za kuiona waione kiurahisi kama wanashuku sababu za mkataba wenyewe. Tutajuaje kama haikufanyika kiupendeleo hiyo mikataba na watu kujali percentage zao wao kwanza kabla ya maslahi ya wengi.

Kuna umuhimu si wa mikataba tuu kuwa wazi bali bidding zote za tender na details za kila tender kupatikana kiurahisi kwa vyombo vyote vya kijamii vyenye interest na huo mkataba. mfano mkataba wa madini lazima uwashikilishe viongozi wa kijamii wa hilo eneo na wao wauone au waangalie kama una manufaa kwao kabla ya serikali kuamua kwenda kuwaachia mashimo huko.

Ni suala muhimu sana mikataba kupatikana na kujulikana kwa viongozi na stakeholders hili hata waandishi nao waweze kutoa opinion zao kutokana na options ambazo zilizopo na kama kweli jamii imepewa the best option. Majuzi kwa waingereza kuna kampuni ya treni ilinyan'ganywa tender na kwa madai ya waziri wa usafiri mdhabuni mpya alikuja na cheapest formular ya kuweza kutoa hiyo service. Baada ya mwekezaji alienyimwa kuanza kelele kwakuwa na yeye aliziona tender zingine ya kuwa jamaa wanaporojo kwa hela wanazotaka kutoa hawawezi mudu hiyo services.

Hapo ndio waandishi na wabunge wengine walipopata interest ya kuchunguza tender zote na kweli ikajaonekana jamaa walikuwa na hadithi wasingeweza iendesha hiyo line ya train kwa ahadi walizotoa kupata tender their numbers dint add up, jamaa akarudishiwa tender na waziri kibarua kikaota majani. Point hapo ni kwamba hivi vitu vikiwa wazi tunaweza ona kama kweli tunapata good value for money au hata kama tunahitaji hizo tender kwa nchi maskini kama sisi.
 
kijakaz umeongea sawa. kweli kuna madudu yamekaa vibaya and we cant do anything about them though with time some things are being corrected. la usiri wa mikataba sie ndo tuko sehemu mbaya kwahiyo bora tu tuionage hiyo mikataba. ebo! naam, kweli leo tunalia na ccm. kesho wataingia cuf na cdm napo tutaanza kulia kivyake. ni kulia tu sie waafrika. tutabadilisha tu milio mi nadhani
 

Tatizo ni zaidi ya katiba.

Tuna tatizo la utamaduni wa "top down" approach.

Kufikiri "waheshimiwa" wana the best interests of the nation muda wote na "wataalam" wanajua wanachofanya.

Shirikisha wananchi wote katika mambo yanayowahusu, wape elimu, weka uwazi, utaona vitu vinajitengeneza vyenyewe organically.

Ushaweka misingi ati.

On the other hand hata ukija na katiba nzuri kama ya mbinguni, lakini kama watu mazezeta na hawashirikishwi wakuu wanaweza kuwa wanavunja katiba kama wewe unavyovunja mkate na hakuna hata wa kuwaandikia a newspaper article.
 
Kuna taratibu tayari ambazo mantiki yake ni kuweka mtitiriko wa uongozi kutoka ngazi za juu mpaka chini kinachoharibu ni middle management ambapo ni wakuu wa mikoa na wilaya kitendo cha hawa watu kuteuliwa na kutokuwa na maamuzi ya local government ndio tatizo kubwa. Kutoka hapo wakaruka chini kuwapa nguvu fulani madiwani za kuweza kuamua vitu vichache. Ni kuboresha tu mfumo wa sasa chini kwa namna ya uchaguzi waserikali za mitaa na watu kugombania nafasi kupitia vyama vya siasa na sera za maendeleo.

Na huko juu ndio tatizo aswa people are not accountable pengine ni uzezeta kama unavyodai, lakini katiba lazima itoe clear powers for sectors to make checks without external interference's. In short no one should be above the constitution and tanzanians rights moja wapo ni madaraka ya raisi lazima yaondoke.

Narudi likizo yangu mjadala mwema.
 

Mkuu mawazo yako ni mazuri and I wish ingekuwa hivyo katika ulimwengu wa Ukweli.

1. Mimi na wewe tunakubaliana kuhusu reduction, refer post zangu zote( Isipokuwa wewe umeiita reduction, na mimi nimeiita Talking points)

2. Hata Nchi ambazo freedom of Information iko juu na inaheshimika kama uingereza, inapokuja kwenye Mikata ya kibiashara huwa wana refuse kutoa Information. Sasa sijui wewe ndugu yangu una mfano wa nchi gani.

3. Article yako nimeisoma lakini, It doesnt make sence in legal and commecial world.Google UNCTAD uangalie wanasema nini kuhusu confidentiality.Wana Documents nyingi tu na nimekuwekea moja hapa jamvini.
 

Attachments


Ninakubariana na wewe. Nadhani kama utaanza kutafuta sahihisho kuanzia kwenye tendering process then utaweza kupata jawabu. Ndio maana nikasema lazima tuwe na utaratibu wa kuainisha list ya watu kwenye uongozi wa kitaifa amabao lazima waweze kuiona mikataba.Na hii itasaidia, kama tatizo ni kwamba watu watanunuliwa then hili ni tatizo lininge la kwamba tunawapataje hawa watu.
 

Perfect Sir!
 
Mbona kununuwa watu au kutoa zawadi ni vitu vya kawaida sana kwenye lobbying process, na hapa nazungumzia nchi zenye checks za kweli na sheria zenye meno.

Lakini ikija julikana kwamba kulikuwa na upendeleo au hongo ilitumika ku influence the decision si kwamba mkataba tu unavunjwa bali na fine ya kutosha kuipotezea muda na kipato serikali itakufuata (hilo linawafanya watu wafikirie mara mbili kutoa hongo kishamba). Vilevile kitendo cha kuangalia mikataba (ambayo sio sensitive kama ya jeshi) kina involve many stakeholders from different aspects kila mmoja anaungalia kwa maslahi yake kwa maana hiyo hata kama kuonga inabidi pia uje na good plan ya kuonga all the stakeholders involved.

Hata kama serikali ikikupa wewe mkataba jamaa wataendelea kuikashifu serikali kwa upande wao kama utekelezaji wenyewe unawahathiri wao na hauna faida kwao (kama kwenye huo mfano wa railway line nilioutoa), hapo tena ni jukumu la wananchi kama wataamua kuirudisha tena serikali chaguzi za baadae.
 

Nimekuwekea hapa, sheria ya Uingereza inavyosema kuhusu hili swala.
 

Attachments


You are missing my point entirely.

Sisemi kwamba katiba haihitaji marekebisho.

Ninachosema ni kwamba, hata ukiwa na katiba inayombana kila mtu vilivyo, kama hamna elimu na ushiriki kwa upande wa wananchi ambao wanatakiwa kuwa hold viongozi accountable hujafanya kitu bado.

While on the other hand, hata ukiwa na katiba ya kidhalimu, kama una population iliyoamka na kuelimika inaweza kuwang'oa viongozi na kuweka katiba mpya.

Kwa hiyo, overall, elimu na mwamko wa wananchi unakuja kwanza kabla ya mabadiliko ya katiba.

Sasa hivi wananchi wamepewa fursa ya kujadili katiba, waseme wanataka nini, wengine wanasema uchinjaji wa kuku uelezwe kwenye katiba.

Sasa ndo mabadiliko ya katiba tunayotaka hayo?
 
Swali linaweza kuulizwa: ni nani aliye mjinga baina yetu? Wao wanaotuambia kuwa mikataba iliyosainiwa ni siri yao tuwaamini au sisi tunaokubali kuwa ni siri tukiamini walichotuambia?
Anayeambiwa si mjinga hasa kwani kashikiliwa ... thubutu atie neno. huko mjengoni ndo hivo tena mchezo wa kuvuta kamba upande majitu 80% upande mwingine watu 20%. wewe umepaza sauti na mimi na yule. hivo ndivo watu wa bara huwafukuza tembo kwa kelele za madebe, miluzi moshi n.k.
 
Hivi kweli hicho (maandishi mekundu) ni kitu cha kutafutia jibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…