Tatizo letu nambari one ni
Kijakazi...Kijakazi hawakilishi mtu moja, anawakilisha wengi na wote mtazamo wao ni kama wa huyu Kijakazi wetu wa JF hapo juu. Kijakazi ni zaidi ya jina, ni utamaduni, ni tabia na ni udhaifu unaosababishwa na uelewa finyu. Tukiitoa CCM hatuwezi kurudi hapa tena kujadili yale yale...tunajadili yale yale kwa sababu tuko pale pale na watu wale wale na mfumo ule ule, hapana, mabadiliko hayaji hivyo. Tukiitoa CCM tumepiga hatua na tumepiga baragumu, tunamtangazia yeyote yule anayekuja kwamba uvumilivu sasa basi, usipotimiza na wewe unaondoka. Huo mfano kwa sasa hatuna kwani pamoja na CCM kupoteza dira, akina Kijakazi bado wamejazana mle mle, hawajui watokako wala wanakoelekea, wapo wapo tu!
Nikirudi kwenye mada ya
Mwanakijiji, nakiri watawala wetu ni werevu, ni kama walivyokuwa Wajerumani na sisi wananchi, kama Chifu Mangungo, ndio wajinga. Tunayoyashuhudia ni mavuno ya yale tuliyoyapanda wenyewe na kwa hiari yetu...inakuwaje mtu na akili zako timamu unampa uongozi mtu asiye na sifa wala historia ya kupigania haki? CCM inapata kiburi kwa sababu sisi wenyewe tumeiruhusu, viongozi wetu hawatetei maslahi yetu kwa sababu tumeshindwa kuyadai na serikali yetu inaingia mikataba ya hovyo kwa sababu tumeshindwa kuwawajibisha.
Kijakazi, unatoa mfano wa Ufaransa, je yupo kiongozi wa Ufaransa anayeweza kuwaambia wananchi wake na wabunge kuwa mkataba serikali yao iliyoingia na mwekezaji ni siri, thubutu!