CHIKAWE: Katiba haitungwi Jangwani au Kibandamaiti

CHIKAWE: Katiba haitungwi Jangwani au Kibandamaiti

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
914
Chikawe amesema haya kwenye mkutano wa wanasheria Dodoma.Anasema yeye haoni tatizo lolote katika mswada uliopitishwa wa kuunda bunge maalumu la katiba na kwamba siyo lazima kukubaliana na kila kitu cha wapinzani na kama wana hoja basi waseme bungeni siyo kwenye mikutano ya hadhara.
My take:Namshangaa Huyu Chikawe hajui kwamba katiba si ya bunge ni ya wananchi.Na kama katiba ni mali ya wananchi basi mahali pekee pa kueleza kasoro hizo ni kwa wenye mali yaani wananchi na hawa wanapatikana kwenye mikutano ya hadhara.
Macho ya Chikawe,Lukuvi na Wasira yana matatizo,kwa sababu watu wengi pamoja na wasomi waliobobea na wanasheria wanaona mapungufu mengi katika mswada uliopitishwa lakini hawa watatu hawaoni mapungufu yoyote.Nawahurumia sana.
 
Mimi siwashangai hawa mawaziri wa JK kwa kauli zao tata na kauli nyepesi dhidi ya hoja nzito...Tumezoea sana. Tarehe 10/10/2013 ndio atafahamu kuwa KATIBA NA SHERIA ZINAWEZA KUTUNGIWA BARABARANI.
 
Wana maneno ya hovyo hovyo!
halafu yanadai tuliyapa ridhaa yatuongeze.
Miccm na liccm lao wanakeraaaje?
 
Kanuni moja ukiwa mwanaccm lazima ujitoe fahamu ktk mambo ya msingi
 
Kumbe ndiyo maana hata ccm wenzake wa kwao walimkataa !
 
Hawa jamaa kimsingi ni vipofu kwa sasa, hawaoni wala kutambua kuzinduka kwa tabaka la watawaliwa...
 
chikawe ni mlevi wa madaraka sawa na wote waliolewa madaraka na wote wana kariri mambo ya ma ccm.watanzania wote tuungani ili kupata katiba na sii kupitia ccm.



Chikawe amesema haya
kwenye mkutano wa wanasheria Dodoma.Anasema yeye haoni tatizo lolote
katika mswada uliopitishwa wa kuunda bunge maalumu la katiba na kwamba
siyo lazima kukubaliana na kila kitu cha wapinzani na kama wana hoja
basi waseme bungeni siyo kwenye mikutano ya hadhara.
My take:Namshangaa Huyu Chikawe hajui kwamba katiba si ya bunge
ni ya wananchi.Na kama katiba ni mali ya wananchi basi mahali pekee pa
kueleza kasoro hizo ni kwa wenye mali yaani wananchi na hawa
wanapatikana kwenye mikutano ya hadhara.
Macho ya Chikawe,Lukuvi na Wasira yana matatizo,kwa sababu watu wengi
pamoja na wasomi waliobobea na wanasheria wanaona mapungufu mengi katika
mswada uliopitishwa lakini hawa watatu hawaoni mapungufu
yoyote.Nawahurumia sana.
 
Ni kule bungeni wanakofanyiwa ubabe na kufukuzwa nje kila leo, au anaongelea bunge lipi?
 
Huyu huwa hapimi kauli zake maana nakumbuka ni huyu huyu aliyekuja na kauli za mwanzo kabisa kwamba katiba ya sasa haina tatizo hivyo hakuna haja ya katiba mpya; lakini siku chache baadae bosi wake JK alimpuuza na kutangaza haja ya kuwa na katiba mpya. kwa hiyo mkuu asikupe shida maana uwezo wake wa kusoma alama za nyakati na upepo wa kisiasa uko very limited.
 
Wote hawa akili yao ni moja!
We waache waendelee kujitoa akili kwa kuropoka hovyo hovyo, mashavu yatawashuka siku bwana wao atakpoufyata na kutambua busara iliyojaa kwa wapinzani.
 
Hii nchi sio ya Chikawe peke yake,JK peke yake au wabunge wa C.C.M peke yao,lazima waelewe hii nchi ni ya Watanzania wote,wasitake kututisha,Jaji Warioba jana kawaumbua mchana kweupe,wao waliamini kua kuwaweka watu kama kina Warioba,Butiku na wana C.C.M wengine ingekua rahisi kutimiza matakwa yao,matokeo yake mambo yamewageuka!sasa kwa kauli kama hii huyu Chikawe nae atajiita ni MSOMI WA SHERIA?mawazo ya kutunga katiba yanachukuliwa hata sokoni
 
Ukitaka uwaziri Tz. lazima akili zako ukabidhi kule ikulu. Yule jamaa wa ikulu ndo anaye-icontrol kwa remote. Wao mawaziri hawana independent thinking.
 
Chikawe amelewa madaraka ila soon hataamini kitakachojiri.
 
Hilo bunge analodai wapinzani wakasemee ni hilo lililohodhiwa na ccm! Katiba si ya wabunge wala wanasiasa ni ya wananchi. Mpaka kieleweke tunataka katiba ya nchi si katiba ya zidumu fikra potofu za wababe wezi na wauza unga.
 
Alisahau Kuongeza na Hili
Katiba haitungwi Lumumba
 
Alisahau Kuongeza na Hili
Katiba haitungwi Lumumba

Isitoshe kama anajua Katiba haitungwi Jangwani wala Kibandamaiti sasa ANAWASHWA nini? Si asubiri MTI uzame kunako halafu ndio atuambie hizi Ngonjera!!

Hakika viongozi tulionao ni Janga.Walipo tumia wingi wao kule Bungeni kuwadhalilisha wapinzani hakujua kuwa wanawafundisha njia nyingine ya kudai haki zao?

Wananchi ndio Mahakama ya Mwisho na yenye maamuzi ya mwisho. Hakuona kule Misri wananchi kwa kuungana na Wapinzani na kutumia viwanja na mabarabara na wakapata walichokitaka!!?

Nini kinacho wadanganya hawa viongozi wetu na kusahau kuwa hata Tanzania wanaoishi ni binadamu na sio Malaika na lolote laweza kutokea!? Watu wamechoka na badala ya viongozi kujua hivyo wao bado wanaiimba kale kawimbo kao ka Kinafiki ka AMANI!!

Hivi Mungu ni wa Tanzania tu? Au Tanzania ina malaika wanaoweza kuvumilia manyanyaso miaka yote? Natamani siku moja nionee huu utulivu ukitoweka halafu tutiane ADABU kidogo hawa wanaodhani kuwa wao ndio wenye miliki ya Nchi hii tuone wataenda wapi!!

Tumechoka sisi na kuburuzwa kila mara. Muwanyime wengine wasitoe mawazo yao na kusikilizwa bungeni halafu wakiamua kuwaachia Bunge lenu na kuja kwa wananchi kuwaelimisha,tena mnaanza kuleta Usengelenyuma nyie Ma-Ccm!!
 
Back
Top Bottom