Chiko Ushindi atua Dar es Salaam kujiunga ya Klabu ya Yanga

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
CHIKO USHINDI[emoji1078] ATUA DAR ES SALAAM

Mchezaji Mpya wa klabu ya Yanga [emoji617] Ambaye atatambulishwa muda wowote kuanzia sasa amewasili Nchini muda huu akitokea Congo Dr[emoji1078]
.
Yanga [emoji617] imekamilisha Usajili wa chico[emoji1078] ushindi Toka Klabu ya Tp Mazembe[emoji246]

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Anacheza nafasi gani uwanjani? Rekodi yake ikoje huko atokako?
 
Yanga SC wamekurupuka ma Kuhemka katika Kumsajili huyu kwani nimemfuatilia kutoka kwa Waandishi wa Habari za Michezo Congo DR na Rwanda na wanadai si mzuri kivile na alichonacho ni Miguvu tu isiyo na Tija sana.

Kwa Maoni yangu ( ambayo naomba yaheshimiwe ) ni kwamba 'technically' sidhani kwa jinsi Yanga SC ilivyosajili vizuri na inavyofanya vyema katika Ligi Kuu ya NBC ilikuwa na haja sana ya Wao kutaka Kusajili kwani Yanga SC imekamilika na hata bila ya huyu Chico Ushindi bado walikuwa na Jeuri ya Kupambana na hata Kutwaa Ubingwa.

Kinachowagharimu / Kilichowagharimu Yanga SC ni Siasa zetu za Simba na Yanga za Kujambishana ( Kutishana ) katika Usajili kwa Kipindi hiki ili tu Kuwaridhisha Mashabiki ili kuondoa Lawama ya kwanini Wapinzani wanasajili na Wao hawasajili?

Kwa Simba SC kujitosa katika Usajili ( hasa dirisha hili dogo ) Kwangu Mimi ilikuwa ni lazima kwani pamoja na kwamba Simba SC ina Wachezaji wazuri na mahiri ila ilipungukiwa Mtu Mmoja muhimu ambaye ni Mchezeshaji ( Playmaker ) kama ilivyo kwa Yanga SC kwa kuwa na Wao Khalid Aucho.

Hivyo Kumrejesha ( Kumsajili ) Kiungo Mchezeshaji ( Playmaker ) Mzambia Clatous Chota Chama kwa 99% Simba SC imeshatibu tatizo na kama Chama atacheza katika ile 'rythm' yake tuliyoizoea nina uhakika akina Sakho, Kagere, Kibu na Morrison Watafunga Magoli mpaka Watachoka kama pia si Kuyakinai kutokana na 'Pasi za Ubarikio' na 'Pasi za Upendo' za Clatous Chota Chama.
 
we toka lini ukwatajia mema yanga,
 
Mkuu kumbe hujagundua kuwa pale mbele Yanga inamtegemea Mayele tu. So akiwa injury au kadi mbadala wake ni Makambo ambaye ni kama kaishakata tamaa. Wale madogo wazawa bado sana.

So kunleta Ushindi ambaye mwenyewe umekiri ana nguvu ni chaguo sahihi kabisa. Na usisahau kuwa naye ni pendekezo la kocha baada ya dili la Phiri kukwama. So most likely ni mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…