Yanga SC wamekurupuka ma Kuhemka katika Kumsajili huyu kwani nimemfuatilia kutoka kwa Waandishi wa Habari za Michezo Congo DR na Rwanda na wanadai si mzuri kivile na alichonacho ni Miguvu tu isiyo na Tija sana.
Kwa Maoni yangu ( ambayo naomba yaheshimiwe ) ni kwamba 'technically' sidhani kwa jinsi Yanga SC ilivyosajili vizuri na inavyofanya vyema katika Ligi Kuu ya NBC ilikuwa na haja sana ya Wao kutaka Kusajili kwani Yanga SC imekamilika na hata bila ya huyu Chico Ushindi bado walikuwa na Jeuri ya Kupambana na hata Kutwaa Ubingwa.
Kinachowagharimu / Kilichowagharimu Yanga SC ni Siasa zetu za Simba na Yanga za Kujambishana ( Kutishana ) katika Usajili kwa Kipindi hiki ili tu Kuwaridhisha Mashabiki ili kuondoa Lawama ya kwanini Wapinzani wanasajili na Wao hawasajili?
Kwa Simba SC kujitosa katika Usajili ( hasa dirisha hili dogo ) Kwangu Mimi ilikuwa ni lazima kwani pamoja na kwamba Simba SC ina Wachezaji wazuri na mahiri ila ilipungukiwa Mtu Mmoja muhimu ambaye ni Mchezeshaji ( Playmaker ) kama ilivyo kwa Yanga SC kwa kuwa na Wao Khalid Aucho.
Hivyo Kumrejesha ( Kumsajili ) Kiungo Mchezeshaji ( Playmaker ) Mzambia Clatous Chota Chama kwa 99% Simba SC imeshatibu tatizo na kama Chama atacheza katika ile 'rythm' yake tuliyoizoea nina uhakika akina Sakho, Kagere, Kibu na Morrison Watafunga Magoli mpaka Watachoka kama pia si Kuyakinai kutokana na 'Pasi za Ubarikio' na 'Pasi za Upendo' za Clatous Chota Chama.