Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Wahenga walisema la kuvunda halina ubani. Hata upambe vipi kwa matarumbeta na vifijo kama kibovu kibovu tu.
Mazembe huwa hawawezi kutoa mchezaji kizembekizembe. Kuiona mchezaji anatoka mazembe anakuja timu ambayo haipo hata kwenye shindano hata la kuku kimataifa, ujue mchezaji huyo ni mzigo.
Mchezaji anayejua boli akiingia hata sekunde 7 unamjua tu. Namna anavyokimbia na ku turn.
Kiwango cha makelele yaliyopigwa na uhalisia ni kama mbingu na ardhi. Yaani kwa kifupi huyo hawezi hata kumfikia Nchimbi yaani kwa Kaseke huyu Chiko akasome.
Maoni yangu ni kwamba kwa sifa tulizoambiwa na akina Manara na genge lake la propaganda za kishamba, tulitegemea tuone moto na nyasi kuungua na miguu ya Chiko. Kumbe mazee tumeuziwa mbuzi kwenye gunia.