Childhood Traumas hazitibiki, Uwe na pesa usiwe na pesa. Unaishi nazo mpaka kifo chako

Childhood Traumas hazitibiki, Uwe na pesa usiwe na pesa. Unaishi nazo mpaka kifo chako

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Wadau kwema?
Iko hivi hatua za ukuaji wa mtu huanzia stage ya utotoni hilo linaeleweka. Lakini stage hii ya ukuaji , ni sehemu iliyo sensitive sana kiasi kwamba ikiathiriwa kwa namna yoyote ile hupelekea kuamua hatma ya mtu baadaye sana maishani mwake.
  1. Wapo watu walionajisiwa na ndugu wa karibu wakiwa watoto.
  2. Wapo watu waliofanyiwa Bullying na watoto wenzao kipindi wakiwa wadogo.
  3. Wapo ambao walitamkiwa maneno mabaya na machafu wakiwa wadogo. mfano"wewe una sura mbaya" n.k
  4. Wapo wale walionyanyaswa na kunyanyapaliwa na ndugu wa karibu kutokana na ulemavu wao, au hata hali ya umaskini wa nyumbani kwao n.k
  5. Wapo wale walijikuta wananyimwa hata chakula na ndugu n.K
  6. Wapo waliotengwa na ndugu baada ya wazazi kutengana au kufariki...
Mifano ni nyingi sana hapa nikijaribu kuitoa. Lakini huu ndio uhalisia wa watu wengi waliyoyapitia wakiwa bado wadogo in which will haunt them later in life . Haya yote tunaweza kuziita traumas au maumivu ya kihisia ambayo wengi wetu wanatembea nayo mioyoni mwao. Mwisho wa siku haya yote ndio huamua mtu aweje kwenye jamii na ndio yatakayoamua jamii imchukulieje.
Leo hii kuna watu ;
  • Wanapenda kukaa peke yao. Yaani kwa kifupi hujitenga na wengine.
  • Hawataki kwenda kwa ndugu mfano shangazi,mjomba kuwasalimia ,kila wakikumbuka walichofanyiwa.
  • Wana hasira au unyonge uliopitiliza.
  • Hawajiamini wawapo kwenye eneo la watu wengi
  • Hawana furaha kwa kila jambo wanalolifanya au kulitazama n.k.
  • Wanajiua au kujidhuru kwa namna yoyote ilekutokana na hali hizi kuwatesa kihisia n.k
  • Wamechoka kihisia.
Zote hizi ni traumas ambazo watu hutembea nazo . Haijalishi ana status gani kwenye jamii. Awe kibega wa kubeba magunia sokoni au awe msaidizi wa karibu wa Rais wa nchi. Traumas Hazichagui wewe ni nani una pesa au hauna ,ni vitu nimejifunza haviwezi kuondoka till death.
20250305_221118.jpg

Sometimes music is a powerful pill to heal you ,some part of you .
 
Ukipata mtaalamu wa saikologia anakusaidia mpaka unakuwa sawa
 
Emotional scar

Wazazi wengi Bongo wanadhuru watoto wao kwa kutokuwajali kihisia "emotional neglect" yaani mtoto analia yeye anachukuliwa kawaida. Au kutosikiliza nini mtoto anataka bali kufanya kile yeye mzazi anataka.
 
Hii ni hatari sana mdau
 
Mimi ni victim wa hiyo namba mbili hayo mengine nayasikia tu kwa wengine, lakini kwangu hiyo trauma inategemea na hali yangu ya kiuchumi nikiwa sina pesa ndio huwa nakuwa na stress kiasi, ila nikiwa nazo yani nasahau shida zote nakuwa na furaha na binafsi nimejifunza kutafuta furaha kwenye mambo mengine yasiyohusisha ulazima wa kuwa karibu na watu
 
Hiyo tupo wengi sana.
 
TZ watu wengi hasa wazazi huwasababishia sana watoto matatizo ya kisaikolojia, unakuta mzazi anamwambia mtoto huna akili wewe, wewe mbona kama chizi nk, yakijirudia haya mara Kwa mara basi lazima mtoto ataathirika, hii hupelekea chuki, kutokujiamini na kujiingiza kwenye tabia mbaya. Inahitaji juhudi kujitoa kwenye matatizo ya aina hii.
 
Eeerf

Unasikia mzazi anamwambia mtoto "mwonee Kubwa jinga" dah!.. kwa wenzetu kama U.S u unasikia mtoto kaua mtoto mwenzake au kampiga visu mwalimu wake na kumuua. Ni hii mambo ya Bullying
 
Even psychologists suffer from their own psychological problems.
Wako watu wanatoa msaada na wanakaa Sawa. Mimi ni mmoja wapo, nime heal na nilipata msaada. So, ni kweli mambo haya yapo na si mazuri lakini usiseme kuwa huwezi kupona au kuwa sawa. Hapo utakuwa unapigilia msumari mtu asitafute msaada hata ukiwa mdogo
 
Back
Top Bottom