Chimbuko la neno Kwampalange

Chimbuko la neno Kwampalange

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Kwa Mpalange
Ni neno maarufu sana nyakati hizi ukizingatia utandawazi umekuwa kwa kasi sana

Neno Kwampalange limekuwa likitafsiriwa kwa maana chanya na hasi

Kwa upande chanya Kwampalange ni sehemu ya
Buza ikiwa kama kata ya Wilaya ya Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 15125

Kata ya Buza
NchiTanzania
MkoaDar es Salaam
WilayaTemeke
Idadi ya wakazi∆55,082
-
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao zaidi ya 55,082 waishio humo.

Huku upande hasi likihusishwa na kitendo cha kufanya mapenzi haramu

Ukweli ni kuwa chimbuko la neno Kwampalange limetokana na mzungu aliyekuwa akiitwa Mpalange na alikuwa akiishi Buza miaka ya 1968 kurudi nyuma,
Mzungu huyo alikuwa akijishughulisha na kilimo kata ya Buza na mnamo mwaka 1968 alirudi kwao na kumuzia mzee mmoja eneo hilo 1968,
Mzee aliyenunua eneo hilo alikuwa akiishi Magomeni Mwembechai.


Article hii haijakamilika hivyo basi kama una taarifa zaidi kuhusu Kwampalange unaweza kutushirikisha"

images (5).jpeg
 
Inawezekana mbona yule wa Wikeliks anaitwa Julian Asange na Manchester utd Kuna beki anaitwa Harry Maguire kwa mswahili asingetamka/ Asanji/wala /Maghwaya/
 
Kilichoipa umaarufu kwa mpalange ni uwepo wa malaya wa bei rahisi ni sawa na pale tandika mk*nd* buku.
Kilichoipa umaarufu, kuna dada alifumsniwa na mume wa mtu, akadhalilishwa kisawasawa.

Kuna siku akahojiwa na hizi tv za mtandaoni, ndipo akaeleza yule bwana hawezi kumwacha, maana anampatia vyote, akasisitiza akihoji yeye anampeleka mpaka buza kwa mparange, je yule mkewe anamfikisha huko.
 
Kilichoipa umaarufu, kuna dada alifumsniwa na mume wa mtu, akadhalilishwa kisawasawa.

Kuna siku akahojiwa na hizi tv za mtandaoni, ndipo akaeleza yule bwana hawezi kumwacha, maana anampatia vyote, akasisitiza akihoji yeye anampeleka mpaka buza kwa mparange, je yule mkewe anamfikisha huko.
Huyo mpaka kusema hivyo,tayari neno 'kwa mpalange' walishalihusianisha na tendo kinyume Na maumbile.
Kuna dada video yake ilisambaa akisaidiwa na majirani kupelekwa hospitali baada ya jamaa (mpemba)kumfumua rinda kweli kweli.kuna sauti kwenye video hiyo ikasikika ikisema 'huku ndiyo buza Kwa mpalange Sasa'.baada ya hapo Sasa,utani ukaanza wa kuambiana nitakupeleka Kwa mpalange wakimaanisha tendo kinyume.na limeshaenea nchi nzima baada ya kusikika kwenye wimbo,ingawa wengine hawaelewi maana yake.
 
Kwa mpalange ipo buza na si mbagala Kama mdau mmoja hapo juu alivyosema

Ukitaka kufika kwa mpalange kwa wakaz wa maeneo mengine panda gari Hadi tandika nenda Msikiti wa CHIHOTA kwa nyuma Kuna gari zinaenda huko

Au panda gari za buza shuka kwa mama kibonge Kuna bajaji na toyo nyingi za kwenda huko

Kwa Sasa kwa mpalange barabara inatengenezwa kwa ajili ya kupiga lami ambayo itaunganisha mbagala kilungule chamaz na maeneo mengine ya mabagala Kwan Kuna daraja kubwa linajengwa hapo

Ila kwa Sasa watu wanapita daraja la mbao ambalo linaunganisha na mbagala kilungule



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom