Chimbuko la neno Kwampalange

Chimbuko la neno Kwampalange

Siku ya Kwanza kufika eneo hilo nilikuwa sipajui kama ndio kwa Mpalange nikajisemea moyoni hili eneo mtu ukibanwa na wahuni hata upige kelele vipi ni ngumu kujinasua wala kupata msaada , sababu vichaka vilikuwa vingi na ukiingia huwezi kuescape mpk upandishe kilima kikali mno ambacho kama siyo mtu wa mazoezi huwezi toboa bila wahuni kukudaka .Na watu wengi walilizwa mno nasikia mpk wengine kufanyiwa vitendo vibaya

Wahuni Buza walilipenda sana kwa sababu lilikuwa kama eneo la kimkakati kutokana na Mazingira kusini kilima kaskazini kilima katikati kwenye tambarare vichaka vingi na nyumba ziko mbali

Kwa sasa mambo yako shwari vichaka kama vya zamani hakuna tena barabara zinapanuliwa na kuboreshwa watu wameongezeka ,pamechangamka hakuna uhuni na kasi ya ukuaji inaongezeka .
 
Itakua mzungu aliitwa Mpalange,ndomaana wanaimba ukipata bwana wa kizungu mpeleke ...
 
Redio ya clouds fm kipindi Cha leo Tena waliweka kambi buza siku kadhaa na walifika hapo siku nzima kuhoji historia ya eneo Hilo...Hilo eneo Kuna mtu alikuwa anaitwa mpalange..sio mzungu Kama mtoa mada anavosema..huyu mpalange aliwaachia watoto wake ndio wakagawa Hawa viwanja na kuuza ..kwa mujibu wa maelezo watoto wake hawaishi hapo Ila wametawanyika sehemu nyingine waishi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sifa kuu ya kwa mparange ilikuwa ni barabara za tope .
Watu wamehusisha tope ndo wakaja na usemi huo
 
Na Yule aliyesema kabakwa na lava lava?
Akahojiwa akaulizwa amekubaka wapi.akasema huku nyuma kwani wewe haujui.
Yule aliyemuhoji akajibu sijui.
Akaniambia huku kwa mpalange
Huyo mpaka kusema hivyo,tayari neno 'kwa mpalange' walishalihusianisha na tendo kinyume Na maumbile.
Kuna dada video yake ilisambaa akisaidiwa na majirani kupelekwa hospitali baada ya jamaa (mpemba)kumfumua rinda kweli kweli.kuna sauti kwenye video hiyo ikasikika ikisema 'huku ndiyo buza Kwa mpalange Sasa'.baada ya hapo Sasa,utani ukaanza wa kuambiana nitakupeleka Kwa mpalange wakimaanisha tendo kinyume.na limeshaenea nchi nzima baada ya kusikika kwenye wimbo,ingawa wengine hawaelewi maana yake.
 
Labda kwa sababu kuna bonde
Kwa mpalange ni jina la eneo lililotokana na mzee mmoja MWINYI enzi hizo alimiiki eneo kubwa Sana na alikuwa na watumishi wengi Sana, eneo hili limeoakana na miinuko miwili mmoja unaelekea mwanagati na mwingine buza na pia Kuna mto mkubwa, MTO MZINGA.
Chanzo Cha kuharibiwa jina la eneo hili na wahuni ni baada ya tukio la jamaa kuuwawa na kuja kutupwa kando kando ya mto MZINGA eneo la kwa mpalange, Hy maiti iligundulika iliingiliwa kinyume na maumbile na kuharibiwa vibaya
Baada ya tukio hilo ikawa sehemu ya utani au watu wakikwazana kuambiana kuwa nitakupeleka kwa mpalange, wakimaanisha kuwa atamfanyia Kama alivyofanyiwa huyo jamaa aliyeuwawa na kutupwa hapo kwa mpalange. KWA MPALANGE ni jina tuu Kama vile sinza kwa remmy, kwa warioba, kwa Aziz Ally n.k Ila kumeharibiwa baada ya tukio Hilo la kutupwa maiti hapo.
 
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom