Naona ulinikimbia upo huku, umesema ni Allah pekee anapotumia wingi
Nimecheka sana,huna huna hoja ya kunifanya nikimbie kama ningekuwa nakimbia hoja.
Sijawahi kukimbia katika hoja. Nikumbushe nilikukimbia wapi na ilikuwa lini ?
Katika korana tunaona Allah kasema akitaka mke atamchukua from us , je yeye ni Hermaphrodite
Korana ndiyo nini ? Pili amesema wapi haya na Mtume hiyo aya ameifasiri na maswahaba waliielewa vipi hiyo aya ?
Kama yeye sio Hermaphrodite (Intersex) hiyo
US ni kina nani?
- Koran ( 21:17) " Had We intended to take a pastime (i.e. a wife or a son, etc.), We could surely have taken it from Us.....
Kwa huu ujinga ambao tunawaambia kila siku ndiyo una dai umekimbiwa,yawezekana hujui maana ya kukimbia.
Huo wingi ni maarufu sana na karibu kila lugha wingi huu unatumika,ni wingi wa kufadhilisha jambo kuonyesha upekee au ubora na utukufu,kama napoweza kusema "Kiatu hiki huvaa watu kama sisi" huku nafsi inayorejewa ni nafsi ya kwanza umoja.
Allah anasema :
16. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo.
17. Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyao mchezo.
18. Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua. (al-Anbiyaa : 16 - 18)
Katika hiyo aya ya 17,hayo maneno yako uliyo yaweka katika mabano
"...(i.e a wife or a son, etc)" . Haya umeyapata wapi na umejuaje kama huo mchezo unao kusudiwa hapo ni hayo uliyo yataja ?
Uwe na heshima kijana,wewe ni dhaifu kuliko nyumba ya bui bui,huwezi kukimbiwa.