Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Afrika hakuwez kuwa na dini au asili ya imani sababu hamkuwa na utaratibu wa kurekodi matukio kwenye maandishi,wala hakuna formula kila mtu na lake. Ndio maana tunasema mila za kiafrika ni za uongo tu.Ukipata kitabu kinachoelezea chimbuko na evolution za imani na dini za kiafrika kichambue pia
Inaboa kuchambua na kujadili imani za kigeni kila siku
Mkuu Muhammad(s.a.w) sahihi alienda madina mwaka 623.So, ni sahihi kuwa walienda Madina mwaka 623. Au sijaelewa hoja yako. [emoji848]
Ww jamaa ni muhimu sana hapa Tanzania. Nimejifunza mengi sana, asanteKwa sasa naishia hapa. Ila bado nasoma vitabu vya huyu mama. Hiki cha History of God kimezungumza dini za Uislam, Ukristo na Uyahudi, so naendelea nacho ambapo kinagusa maeneo mengine nje ya Uislam. Baadae nitasoma vitabu vyake viwili ambacho kimoja kimemzungumzia Muhamad na Kingine kimeuelezea Uislam exclusively. So napo nitadonoa mawili matatu nitakayoona yanafaa nitayaweka hapa.
Hoja ni kwamba wameanza kusali swala tano tangu 621 kabla hawajaenda Medina 623 tofauti na maelezo uliyowasilisha yaliyosema walisali mara tatu kwa kuiga/kukubalika kutoka kwa wayahudi wa madinaSo, ni sahihi kuwa walienda Madina mwaka 623. Au sijaelewa hoja yako.
Tupe basi kisa kwanini Aqsa?Mkuu Muhammad(s.a.w) sahihi alienda madina mwaka 623.
Ila kabla ya kuhama Muhammad alishaacha kusali mara 2 na kupewa sala 5 .Hii ni baada ya kisa cha ISRAA na MIRAJI ambacho kilitokea October 621 hapo ndipo alipopewa swala 5. (Muhammad hakusali sala 3).
Nahicho kisa cha Israa na Miraji kilianzia ktk Masjid Haraam (Makkah) to Baytul Maqdis(Masjidi Aqswaa) Parestina ktk Mwaka 621
Hoja hii naipinga sababu kuna kitu umeacha na kuna kitu umekiweka ambacho kinavunja msingi wa hoja yako.Tuanze polepole.
Hoja yangu ya msingi ni kwamba, mtu anaweza kujua jibu fulani si sahihi, kwa sababu lina contradict basic principle, bila hata ya kujua jibu sahihi ni lipi.
Unakubaliana na hoja hii au unaipinga?
Sababu hiyo ni maana ya Uislamu. Yaani kumnyenyekea na kumtii Allah kwa kumuabudu.Ni vipi kwenye kunyenyekea na kutii pekee kumfanye mtu aitwe muislam?
Uislamu umegawanyika sehemu mbili. Uislamu wa ujumla ndiyo huo walio kuwa nao mitume na manabii na Adamu na Uislamu maalumu alio kuja nao mtume.Uislam una misingi (nguzo) je unao ushahidi wa kimatendo aliyoyafanya Adam kutimiza nguzo zote tano za uislam?
Ajue kwanza nini?Hoja hii naipinga sababu kuna kitu umeacha na kuna kitu umekiweka ambacho kinavunja msingi wa hoja yako.
Unapoweka tamko "...,kwa sababu lna cntradict basic principle". Hii kauli inazua maswali ya kabla na baada kwa huyo muhusika. Swali la kwanza linalo zuka ni je mtu huyo anakuwa anazijua hizo "basic principle" ?
Kwa maana rahisi ni kuwa mfano wako ulio utoa unamtaka mtu sharti ajue kwanza na si kinyume chake.
Juu ya square root. Sababu hiyo ni istilahi ya kifani. Tofauti na kitu kama maji aufano wake.Ajue kwanza nini?
Wingi huo ni wingi wa kufadhilisha,katika lugha hili lipo sana na si wingi wa kiidadi. Hapo ni Allah pekee.
Kiarabu kinaweza kuwa ngumu kwako kueleweka, labda nikueleweshe kupitia kifaransa, neno "Vous" linapotumika huwa na maana ya wewe (umoja) au ninyi, lkn kwenye umoja si kwamba linatumika kwa kila mtu, la hasha. Ikiwa mtu unamheshimu, utatumia " Vous " yaani wewe ninayekuheshimu yaani mtu mwenye cheo, lkn akiwa mtu wa kawaida unasema 'tu '
Kwenye English language, "You " pia humaanisha wewe au nyinyi, je ni wakati gani na mazingira wasomi wa English wapo wengi wataeleza.
Kwa hiyo kwenye kiarabu litumikapo neno نحن "sisi " kwenye nafsi ya umoja humaanisha utukufu au cheo,
Wasio jua huwa wanaingia mzima mzima eti wakiona ni hoja yenye kusupport imani ya Mungu zaid ya mmoja.La hasha sivyo.
Magwiji huwa wanawacheka wakiwaona kama ni wenye upungufu wa elimu.
Kama hujui square root ya 2 unaweza kusema kwamba square root ya 2 si 10?
Logical non sequitur.
Wewe una inferiority complex.Ila wee jamaa na kiinglishi chako bwana, mtu akishajua kuongea kiingereza anataka aonekane kwa kila mtu anajua, na hii kitu zaidi nimeiona kwa waswahili, anaongea kiswahili anatia na neno la kiingereza [emoji1787] ila wachache tu hawajionyeshi
Kwa taarifa yako tu, elimu yako ya kidunia/Secular haitakusaidia chochote baada ya kufa kwako, kaa ukijua hilo!
Kwa kuzingatia jibu lako ni wazi uislam wa Adam na uislam wa Muhammad ni aina mbili tofauti wa uislam.Uislamu umegawanyika sehemu mbili. Uislamu wa ujumla ndiyo huo walio kuwa nao mitume na manabii na Adamu na Uislamu maalumu alio kuja nao mtume.
Hapa kuna mambo mawiliSababu hiyo ni maana ya Uislamu. Yaani kumnyenyekea na kumtii Allah kwa kumuabudu.
Naona ulinikimbia upo huku, umesema ni Allah pekee anapotumia wingi
Korana ndiyo nini ? Pili amesema wapi haya na Mtume hiyo aya ameifasiri na maswahaba waliielewa vipi hiyo aya ?Katika korana tunaona Allah kasema akitaka mke atamchukua from us , je yeye ni Hermaphrodite
Kwa huu ujinga ambao tunawaambia kila siku ndiyo una dai umekimbiwa,yawezekana hujui maana ya kukimbia.Kama yeye sio Hermaphrodite (Intersex) hiyo US ni kina nani?
- Koran ( 21:17) " Had We intended to take a pastime (i.e. a wife or a son, etc.), We could surely have taken it from Us.....
Siyo tu Adamu na Mtume,bali kwa manabii wote. Utoafuti ni katika sheria ila imani yao moja na ndiyo maana hakuna Mtume wala nabii wa kweli ambaye hakuwa Muislamu.Kwa kuzingatia jibu lako ni wazi uislam wa Adam na uislam wa Muhammad ni aina mbili tofauti wa uislam.
Nani amekwambia Uislamu wa Muhammad hauna msingi na sheria ?Kwanini uislam wa ujumla uwe na msingi, sheria na taratibu tofauti na uislam maalumu aliokuja nao Muhammad ili hali sifa ya Mungu ni kuwa na uwezo mkubwa wa kupanga na kujua ya mbele. Alisahau nini kupanga kila kitu katika umma wa kipindi cha hapo kabla?
Unaweza kuthibitisha Allah yupo kweli na habari za kuwepo kwake si kamba za watu tu?Nimecheka sana,huna huna hoja ya kunifanya nikimbie kama ningekuwa nakimbia hoja.
Sijawahi kukimbia katika hoja. Nikumbushe nilikukimbia wapi na ilikuwa lini ?
Korana ndiyo nini ? Pili amesema wapi haya na Mtume hiyo aya ameifasiri na maswahaba waliielewa vipi hiyo aya ?
Kwa huu ujinga ambao tunawaambia kila siku ndiyo una dai umekimbiwa,yawezekana hujui maana ya kukimbia.
Huo wingi ni maarufu sana na karibu kila lugha wingi huu unatumika,ni wingi wa kufadhilisha jambo kuonyesha upekee au ubora na utukufu,kama napoweza kusema "Kiatu hiki huvaa watu kama sisi" huku nafsi inayorejewa ni nafsi ya kwanza umoja.
Allah anasema :
16. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo.
17. Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungeli kuwa ni wafanyao mchezo.
18. Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa mnayo yazua. (al-Anbiyaa : 16 - 18)
Katika hiyo aya ya 17,hayo maneno yako uliyo yaweka katika mabano "...(i.e a wife or a son, etc)" . Haya umeyapata wapi na umejuaje kama huo mchezo unao kusudiwa hapo ni hayo uliyo yataja ?
Uwe na heshima kijana,wewe ni dhaifu kuliko nyumba ya bui bui,huwezi kukimbiwa.