Kilanga huaga unanichanganya kidogo, ni kwamba wewe huamini kabisa uwepo wa Mungu au huamini katika mungu wa Quaran na Biblia? Hebu nifafanulie kidogo na mimi nielewe.
Jina ni Kiranga, si Kilanga.
Kwa kuanzia, mimi sitakibkuamini, nataka kujua. Kwa muktadha mzuri.
Pia, kwa hivyo, na kwa kufuata mantiki, siamini katika Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na ujuzi wote.
Zaidi, si Mungu tu, sikubaliani na hqbqri zote za supernatural. Kama uchawi, majini, malaika, astrology, na mengine kama hayo.
Kwa hivyo, ukifuata habari hizi, utaona kuwa si Mungu wa Biblia na Quran tu ambaye simkubali.
Pia simkubali Mungu wa Bhagavad Gita, wa Torah, Talmud, Upanishads, Egyptian Book of The Dead, Tibetan Book of The Dead, Vedas, Agamas, Tripitaka, Dhammapada, Kojiki, Guru Granth Sahib, Dao De Jing, The Book of Shadows, The Four Valleys, The Seven Valleys, Avesta.
Lakini sioni sababu ya kuzungumzia vingi hivi jwa sababu hapa JF watu wengi wanajua Quran na Biblia zaidi.