Chukua tuition hii:
(Qur'an 6:19-23)
19. Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha. 19
[
https://www]
20. Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao. Wale walio zikhasiri nafsi zao hawaamini.20
[
https://www]
21. Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi. 21
[
https://www]
22. Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio shirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai? 22
[
https://www]
23. Kisha hautakuwa udhuru wao ila ni kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina. 23
Ukisikia neno "sema" maana yake kuna muamurishaji na mpokea amri.
Sasa katika Aya ya 19 hapo ni Malaika akimuamuru mtume.
Na Malaika ndiyo nafsi ya kwanza hapo na mtume ni nafsi ya 2.
Aya ya 20 neno "wale" ndiyo linawakilisha nafsi ya tatu.
Aya ya 22 neno "tutapo") na neno ("wakusanya") ni maneno yenye
Tofauti kabisa kimantiki.
Neno "tutapo" ni neno la umiliki na neno "wakusanya" ni nafsi
ya 3.
Sasa kwa ujumla ni kwamba, maagizo ya Mwenyezi Mungu kwenda kwa mtume yalipitia kwa malaika ambaye ni nafsi ya kwanza kwenda kwa mtume ambaye ni nafsi ya pili na kwenda kwa watu ambao ni nafsi ya tatu.
Hapo Mwenyezi Mungu anabaki katika kuwakilishwa na malaika.