Chimbuko na Upotofu wa kanisa la Waadventista Wasabato


Kwa ujumla dini za sabato yehova ni dini za upotoshaji na utapeli mwingi sana, ndiyo maana hata hazina wafuasi wengi hapa duniani! Akina Elllen white na wenzie wamewaingiza wasabato mkenge hadi leo, ndiyo maana wengi wamechanganyikiwa. Wengine waliwahi kukaa pale Airport Dar kwa siku kadhaa (wasabato masalia) wakidai wanakwenda Iraq kwa kutumia biblia ( ndiyo passport yao), lakini serikali ikawaacha na imani yao potofu, wakaja wakakurupushwa na njaa na kusambaratika huku wakiacha vinyesi kila mahala pale walipokuwa wanalala.
 
Hiki ulicho andika wewe siyo NENO LA MUNGU(ambako ni kweli na uzima - KRISTO), bali ulicho andika ni UONGO NA NI MAUTI.

Kweli na uzima ni haya maneno:

"
Mathayo 5:33
Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;

Mathayo 5:34
lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;

Mathayo 5:35
wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

Mathayo 5:36
Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.

Mathayo 5:37
Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu."

NB: Kuwa makini na Biblia kwani si maandishi yote ni Neno la Mungu Bali mengine ni Maneno ya MAUTI.
 

Kwanini wasabato wanaapa kwenye UBATIZO?
 

Ukiachana na hoja ya siku ya kuabudu bado una uhakika ellen white hakinzani na maandiko? Na swali mbona unaapa tena ukimtaja kwa kumuamin kwamba ni nabii wa mungu?
 
Tuitunze kwa akili Lakini pia tusiache kabisa kuitunza kma makanisa ya j2 yanavofanya.
Kwasababu hiyo hata mbinguni itakuwepo

Mimi napata ukakasi kidogo kwa wasabato! Ni msabato gani anaitunza sabato kama ilivyoandikwa kwenye biblia? Au ndio kufunganishwa na sheria bila kuwa na haki ya Yesu Kristo?
 
Nimehoji hayo maswali lakin sipati jibu kwa wasabato kwanini?
 
Hongera kwa kueleza kwa ukweli lini sda walianza. Uko sawa. Lakini hukusema pia lini RC ilianza kumbuka Rc kama lilivyo jina lenyewe Roman Catholic maana ya Rumi inayoenea( sambaa) ilianza 476 BK na kufikia 538 ilikuwa imeshila dola kumbuka ilikuwa Rumi ya kishenzi( yaani isiyo na dini) ikijihuisha kwa kuingiza dini na karne ya 5 na 6 Rumi yenye dini iliyochanganya na upagani( ushenzi) ilikuwa in full swing kwa kuua na kutesa wafia dini qaliokuwa wakipinga upotoshaji.
Petro unayemtaja kama Papa wa kwanza jambo ambalo ni uongo aliuawa na dola hii ya Rumi kwa kusulubiwa.
Tatizo husomi ilitabiriwa kuwa Rumi ya kidini ingekuwa na nguvu tu kwa miaka 1260 kuanzia liposhika dola 538 na ingekoma.

Niseme tu ni kweli wa Sda hawa unaowaona kanisa lao lilisajiliwa miaka uliotaja 1863 lkn Rc pia ilianza 538 haya makanisa yote yana mwanzo.

Swali ni hili je Neno la Mungu lina mwanzo? Na mwamzo wake ni wapi?
Je ibada ina mwanzo? Na mwanzo wake ni lini?
Je manabii waliokuwa wanawaambia watu wamrudie Mungu walikuwa wakianzisha dini mpya?
Huenda unachanganya mambo kati ya dini mpya au kurudi ulikokuacha.

Baada ya Rc kudanganya na kuzua usomaji wa Biblia kwa watu. Isomwe tu na makasisi wa kanisa na wengine waelezewe tu giza la uelewa lilifunika jamii hadi hapo watu waliamua kuanza matengenezo.
Kwa taarifa Martin Luther huyo mjerumani alikiwa kasisi wa Rc akayakataa mafundisho potofu kama kuokolewa kwa Matendo, kulipia msamaha n.k, John Huss na wengine. Ni kuambie tu kuwa haya yalikuwa ndani ya biblia yakitabiri namna watu wataurudia ukweli wa Mungu.

Mwisho usishindane kutetea dhehebu tetea kile Mungu amesema. Au la jiunge kundi la kuikataa biblia , kukataa ibada kwa Mungu na kusema dini ni utumwa, lkn ikichukua biblia yenyewe haijui sda wala Rc inajua kusema ukweli mmoja tu ulikuwepo tangu zamani ikiwemo ibada ya Sabato
 
Mimi napata ukakasi kidogo kwa wasabato! Ni msabato gani anaitunza sabato kama ilivyoandikwa kwenye biblia? Au ndio kufunganishwa na sheria bila kuwa na haki ya Yesu Kristo?
Ukweli kabisa kama si Yesu na Haki yake hakuna atunzaye si sabato tu matakwa yote ya Mungu. Je umewahi kujuliza maswali kuwa ni nani aliye mtakatifu atayeokolewa? Yaani hana dhambi?
Je umewahi kujiuliza ikiwa hayupo asiye na tatizo kwanini Mungu anataka wakamilifu? Rafiki elewa hili neno, " katika Kristo Yesu" "ndani yake" " kwa Yeye" ndio ngao yetu nje na Yesu tuna laana, hukumu na kifo cha milele. Mwamini Yesu yaamini maneno yake mengine mwachie atatenda.
 
Ukiachana na hoja ya siku ya kuabudu bado una uhakika ellen white hakinzani na maandiko? Na swali mbona unaapa tena ukimtaja kwa kumuamin kwamba ni nabii wa mungu?
Sitaki mie mtu aamini kuwa Ellen ni nabii au sio. Ila yapime maneno yake kwa nuru ya Neno la Mungu i.e Biblia ikiwa yanakinzana yatupe. Lkn mara nyingi hukizani huja pale tunaposima na kuweka uelewa wetu au kusoma ili kutumia kama rungu. Ndio maana hata biblia wengi hudhani inapingana. Huoni ulaji unatetewa na kupingwa kwa bibilia? Huoni ndoa za mke mmoja au zaidi zinatetewa na kupingwa kwa kutumia biblia? Swali biblia inakinzana? Ni big No!
 
Yesu mwenyewe alisema yeye ndiye Bwana wa sabato(Luka 6:5),sasa kama amri ya nne iling'aa
kuliko ya kwanza wakati amri ya kwanza inatufundisha kumwabudu Mungu peke yake,basi sabato ni kuu kuliko Mungu mwenyewe.
Na hapo kuna upotoshaji mkubwa.
 

Biblia haitoshi kujipambanua yenyewe bila maandiko ya ellen white? Yaaani msinge pekeee na Nuru haitoshi kuwa biblia kwa kuliongoza kanisa?
 
Swali kutoka mathayo 3:33-37 kwann ukitaka kuwa msabato unaapishwa? Sina majjbu bado
 
Biblia haitoshi kujipambanua yenyewe bila maandiko ya ellen white? Yaaani msinge pekeee na Nuru haitoshi kuwa biblia kwa kuliongoza kanisa?
Unauliza swali gani hili? Ni sawa na kuuliza kwanini Mungu ameleta manabii wengi? Kwanini asikomee mmoja tu wakatosha
 
Swali kutoka mathayo 3:33-37 kwann ukitaka kuwa msabato unaapishwa? Sina majjbu bado
Kuapa unakujua? Kamusi ina sema maana ya kuapa nini?
Halafu hili fungu Math 3:33-37 HALIPO.

Bora ungetumia hili

"Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni."
Mathayo 10:32
 


Ukiuliza swali hili, Dini au Dhehebu Fulani lilianzishwa lini? Utapata majibu ya kufurahisha, maana kila dhehebu na kila Dini inadai ilikuwepo tangu mwanzo wa ulimwengu unaumbwa. Lakini ukweli ni kwamba Dini hizi zilizopo ukiondoa Dini ya kiyahudi isiyoamini ukristo wala uislamu, madhehebu yote ya kikristo na Dini ya kiislamu vilikuja baada ya kristo, kiimani tunaamini Dini ya kwanza ni imani ile ya Adamu na Hawa au Eva ambayo haikuwa na jina hadi nyakati za kina Nuhu na Abraham ambao ukristo na uislamu vyote vinafuata hadi Kwenye kizazi cha Mose, imani ya Mose ndio kristo aliikuta ilijulikana kama Dini ya Mose. Miaka yapata 60 baada ya Kristo inasadikika ndipo lilipoanza kanisa la katoliki chini ya uongozi wa Papa wa kwanza na mwaka 610 baada ya Kristo Mtume Muhammad SAW alianzisha Dini ya Uislamu, kabla ya ukatoliki kupata upinzani na makanisa ya Kiprotestant kujitenga na ukatoliki, makanisa ya mwanzo yakiwa ni Lutheran lilianzishwa na Padri aliyeasi ukatoliki Luther Martine Ujerumani mwaka 1520, kisha Mfalme Henry wa Tatu alianzisha Anglicana Uingereza mwaka 1543. Anglicana Ikijitenga na ukatoliki na baadaye madhehebu mengine yakifuatia, Baptists, Salvation Army, Lutheranism, Evangelical, Moravian Marekani na mengineyo yakiendelea kuibuka Hadi Sasa.
 
Ukiachana na hoja ya siku ya kuabudu bado una uhakika ellen white hakinzani na maandiko? Na swali mbona unaapa tena ukimtaja kwa kumuamin kwamba ni nabii wa mungu?
Kwa aliyoyafunua kwa dunia hii ambayo ilikuwa imeshapotea. Yule ni Nabii wa Mungu.

Hakuna sehemu amepingana na Biblia. Lamda nitajie hapa.
 
Kwa aliyoyafunua kwa dunia hii ambayo ilikuwa imeshapotea. Yule ni Nabii wa Mungu.

Hakuna sehemu amepingana na Biblia. Lamda nitajie hapa.

Mimi ukinijibu kuhusu viapo vya ubatizo nitakuona wamaana sana na kukusikiliza vzr
 
Kwanini wasabato wanaapa kwenye UBATIZO?
Nafikri, wanaapa ili iwasaidie kulinda uaminifu wao kwa Mungu katika kushika Sheria zake hasa ya sabato.

Huku wamesahau kwamba Neno la Mungu linasema usiape kwa chochote.
Huku wamesahau pia kuwa kama unategemea torati, umelaaniwa kwa sababu huwezi kuitimiza:

Wagalatia 3:8
Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.

Wagalatia 3:9
Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.

Wagalatia 3:10
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

Wagalatia 3:11
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…