Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
China imeazimia kutotegema tena gesi asilia toka kwa mataifa pinzani, ambayo ni Marekani na Australia. Na badala yake inawekeza ktk project ya kujenga bomba jingine jipya la gesi toka Russia ili kuongeza zaidi kiwango cha gesi inayonunua toka Russia.
Bomba la awali (lililopo sasa) hupeleka gesi toka Russia kuingia China kiwango cha mita za ujazo bilioni 38 kwa mwaka, ambazo ni sawa na lita trilioni 38.
Ktk mradi huu wa bomba jipya la gesi, China itaongeza kiwango cha mita za ujazo bilioni 10 kwa mwaka (sawa na lita trilioni 10 za gesi).
Pia Russia ipo ktk mchakato wa ujenzi wa bomba jingine la tatu la gesi (Power of Siberia 2 Pipeline), ambalo litapitia Mongolia kupeleka gesi China na litakuwa na uwezo wa kupeleka gesi mita za ujazo bilioni 50 (sawa na lita trilioni 50) nchini China.
Mabomba hayo kwa ujumla yataiwezesha China kununua gesi ya Russia mita za ujazo bilioni 100 (sawa na lita trilioni 100) kwa mwaka, ambayo ni takriban nusu ya gesi inayonunua China toka nchi za nje (China hununua gesi kiasi cha mita za ujazo bilioni 200 kwa mwaka toka nchi za nje). Kwa upande wake Russia, atanufaika kwa kupata soko jipya ambapo atakuwa akiuza karibu nusu ya ile gesi aliyokuwa akiipeleka Ulaya. Russia amekuwa akiuza takriban mita za ujazo bilioni 170 hadi 200 kwa mwaka ktk nchi za Ulaya.
asia.nikkei.com

China turns to Russian gas to curb dependence on Quad members
Beijing and Moscow eye pipeline capacity equal to half European demand