China: Fursa za biashara, usafiri na masoko

safi mkuu. vip kwenye swala la exportation unauzoefu....!?
Hapana , sina uzoefu wa kutosha japokuwa nimeeleza ABC za kuexport na mambo ya kuzingatia. Fuatilia uzi huu comments zilizopita. AHSANTE
 
Ninataka kutengeneza√ print nguo za clothline yangu pamoja na stationary line.Nimejaribu kufuatilia Nikaambiwa wasanii wengi wanafanyia China.Unaweza kusaidia kunipa mwanga kuhusu hili na gharama zake zikoje mkuu.
Unataka kununua materials na uje ufanye printing mwenyewe Tanzania au unataka kila kitu kifanyike China ,wewe ubebe tu mzigo baada ya kutengenezwa?
 

Ngoja nijibu Hii kama ulishawahi jibiwa sorry... Nikwamba hongkong iko ndani Ya china ila ina mambo Yake na sheria zake Tofauti na mainland so ukitaka kwenda Guanzoh kutokea hongkong Lazima uwe na viza tena ulichukua Tanzania ..zamani walikua wanatoa hapo hongkong lakini baada Ya watanzania wengi kupata matatizo ya unga wakazistopisha ..so wengi uwamua kutumia za Shenzhen ili kuingia Guanzoh ....anatoka hongkong anajifanya anaenda Shenzhen so akishuka Shenzhen hatoki nje anapata treni hapo hapo Ya kwenda Guanzoh ila wanatoa visa Ya siku tano tu...sasa omba usipate msala huko Guanzoh ukikutwa na Iyo visa ya Shenzhen ni majanga kwako
 
Unataka kununua materials na uje ufanye printing mwenyewe Tanzania au unataka kila kitu kifanyike China ,wewe ubebe tu mzigo baada ya kutengenezwa?
Yaani mimi ninataka mzigo uliokamilika tu.Kila kitu kifanyike China.
 


Walio sio wachoyo wa mafanikio hivi mbarikiwe....
 
Naitaji hiyo machine ya kubania glass za juice 0762825501 tuwasiliane nipo mwanza unaweza kunitumia picha zake whatsup
 
Yaani mimi ninataka mzigo uliokamilika tu.Kila kitu kifanyike China.
sawa. Hii kwa kifupi ni kwamba T-shirt zipo itategemea unataka ubora gani, watu wa printing wapo, inategemea tu wewe unataka design ikoje. Naweza kukusaidia katika hilo ukinipa quality, na sample ya design yako kisha nitawasiliana na wauzaji na watatupa makadirio ya gharama zao. Tuwasiliane mkuu.
 
Ebwana kipilipili nashukuru mchango wako maana wengi tumeelimika aise.
 
kwa wale wenye uhitaji wa viwanda vya uhakika vya
toothpaste
lotions
hair shampoo/oil/stiming
spray insecticides'

tuwasiliane
 
Much appreciation kwa Kipilipili, mtu kutoa details kama hizi hakuna dought kwamba sio mbinafsi. Tukipata wengi kama Kipilipili naamini tutapiga hatua
 

Heshima kwako mkuu Kipilipili!
Asante sana kwa Elimu endelevu ambayo unaitoa hapa jukwaani. Naomba unisaidie kujua kitu kimoja, Kule China kuna sehemu inaitwa YIWU ambapo nasikia kuna International market pia kubwa sana. Ni nini uzoefu wako na hii sehemu kwa kulinganisha na Guangzhou, yaani kwa aina ya vitu, ubora, gharama za kununua na kusafirisha mpaka bongo, pamoja na gharama za maisha kule?? Natanguliza shukran tena....ahsante
 
samahan wakuu kwa ku interrupt topic yenu lakin naomben mnisaidie kwa hili mm nkijan mdogo tu kwasasa npo dsm nmejchang nmepata million moja ivyo naombeni ushaur ni biashara gan itanpatia mapene kwa harak au tafadhal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…