mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Nchi za magharibi hazijaamini hadi sasa kuwa Urusi imeweza kuhimili vikwazo lukuki vya kiuchumi, kinyume chake nchi za magharibi hususan ulaya magharibi ndizo zilizoumia zaidi. Ilitegemewa kuwa urusi itashindwa kuhimili na hivyo kushindwa kuendesha vita vyake dhidi ya ukraine.
Kwa upande mwingine China japo ina uwezo wa kuivamia na kuishinda Taiwan kwa nguvu za kijeshi, lakini haina ubavu wa kuweza kuhimili vikwazo vya kiuchumi toka nchi za magharibi kama urusi ilivyoweza. Ndiyo maana China haina ubavu hata kidogo wa kuweza kuivamia Taiwan. Itabaki kupiga kelele tu na vitisho vya mazoezi ya kijeshi kuizunguka Taiwan. Mabeberu wa nchi za magharibi wanajua china hana ubavu huo wala hawezi kufanya yale ambayo urusi inafanya leo!!
Sababu kuu kwa nini China haiwezi kuhimili vikwazo vya kiuchumi vya mabeberu:
1. Uchumi wa China unategemea uuzaji wa bidhaa za viwandani na soko lao kubwa ni nchi za ulaya na marekani. Kwa bahati mbaya hizi bidhaa si bidhaa za lazima kiasi kwamba nchi zikigoma kununua zitaathirika, lakini pia kuna bidhaa mbadala toka mataifa mengine.
Hii ni tofauti kabisa na Urusi ambayo yenyewe huuza bidhaa ambazo ni za lazima katika maisha na bidhaa ambazo haziwezi kukosa soko duniani yaani mafuta na gesi!! Ukikataa kununua kwanza lazima uumie na utalazimika kuzitafuta kwa gharama zaidi! Mfano, Poland ilikataa kununua gesi ya urusi kwa sharti la kulipa kwa ruble. Lakini Poland ililazimika kununua gesi hiyo hiyo ya urusi kupitia kwa Ujerumani na kwa bei ya juu zaidi!! Hivi sasa nchi za ulaya wanalazimika kununua gesi kimiminika toka marekani ambayo kwanza haitoshelezi lakini pia ni gharama mara nne zaidi, wakati urusi inauza gesi kwa masoko mengine ya china na India.
2. China inategemea pia viwanda vyake ambavyo vingi vipo huko huko marekani na ulaya! Viwanda hivyo vikipigwa marufuku China haina ubavu wa kuzalisha bidhaa nyingi kuweza kutosheleza masoko yake hata nje ya ulaya na marekani.
3. China haijitoshelezi kwa vyakula na bado hadi leo inategemea kuagiza vyakula toka mataifa mengine hasa marekani na ulaya. Wakinyimwa chakula na kwa vile ni wengi hawawezi kustahimili. Tofauti na Urusi inayojitosheleza kwa vyakula na sehemu kubwa kuuza nchi za nje.
Kwa kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo uwezo wa China kuishinda Taiwan kijeshi unavyozidi kupungua maana Taiwan itauziwa silaha za maangamizi na za kujilinda!!
Kama ilivyo kwa Urusi kama ingechelewa zaidi kuivamia ukraine, ingekuta ukraine imejiimarisha zaidi kijeshi.
China inatia huruma lakini haina jinsi zaidi ya kulalamika!! Lakini ni afadhali kutokuthubutu kuliko kuthubutu halafu ukafilisika!!
Kwa Urusi tunavyozungumza, keshaweka kibindoni tayari majimbo matano ikiwemo Crimea na Ukraine hana jinsi zaidi ya kulia lia kwa mabeberu kuomba misaada ya fedha na silaha!! China ubavu huo hana vinginevyo itaaibika!!