Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Hivi karibuni, “China Haul” imepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii duniani. Kutoka droni, hadi vipaza sauti visivyotumia waya, kutoka vifaa vya nyumbani, hadi mavazi ya kisasa, watu wenye ushawishi wanafungua na kuonesha bidhaa zilizonunuliwa nchini China, na kuvutia mashabiki wengi.
Kulikuwa na wakati ambapo watu wengi wa China walisafiri nje ya nchi kufanya manunuzi. Lakini hivi leo, watumiaji wa kigeni wanavuka bahari kufanya manunuzi nchini China. Mabadiliko haya yanatokana na maendeleo ya kasi ya sekta za utengenezaji za China. Kwa mfano droni na kamera za panoramic, bidhaa hizo za teknolojia ya juu zilizotengenezwa nchini China zina ubora wa juu na kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja, pia bei ni rahisi zaidi kuliko zile zilizotengenezwa na nchi nyingine, hivyo zinapendwa sana na watu wa nchi mbalimbali duniani.
Wakati huo huo, mazingira ya sera za kibiashara yanayoendelea kuboreshwa pia yamewavutia sana wateja wa nchi nyingine kuja kununua nchini China. Kwa mfano mji wa Shanghai, tangu sera ya “marejesho ya haraka ya kodi baada ya ununuzi” kuanza kutekelezwa mwaka jana, idadi ya maombi ya marejesho imeongezeka mara 14.7, huku kiasi cha mauzo kikiongezeka mara 9.7.
Kinachostahili kuzingatiwa zaidi ni kwamba licha ya bishara, “China Haul” ina maana nyingine kubwa. Washawishi wa kigeni wanapoeleza kwa dhati shauku yao kuhusu bidhaa hizi mbele ya kamera, kwa hakika wanajenga daraja la kuaminiana kati ya tamaduni tofauti. Inaonesha kuwa bidhaa zilizotengenezwa China si kama tu kwamba zina ubora na sifa nzuri, bali pia zinatoa thamani ya kihisia, na kuchagua bidhaa za China kunakuwa chanzo cha fahari. Kuanzia “China Travel” hadi “China Shopping”, na kutoka “China Cool” hadi “China Haul”, mfululizo huu wa maneno maarufu yanayohusu China unaonesha mwelekeo dhahiri: mtazamo wa dunia kuhusu bidhaa za China unabadilika kutoka kuiona nchi hiyo kama “kiwanda cha dunia” hadi kuiona kama chanzo cha uvumbuzi na nchi muhimu ya kufanya manunulizi.
Umaarufu wa “China Haul” ni matokeo ya maendeleo ya viwanda vya China na sera yake ya kufungua mlango. Kupitia kila bidhaa, na kila video ya kufungua vifurushi, China halisi, yenye sura nyingi na inayobadilika kwa kasi, inaonekana, inaeleweka na kukumbatiwa na watu wengi zaidi duniani.