China ilikuwa sawa na Tanzania, leo wao sawa na Marekani

Sera ya ubinafsishaji tuliielewa sana mpaka kufikia kubinafsisha ubinafsi wetu kwetu wenyewe yaani ule ubinafsi tukajibinafsisha.
Hii nchi ni mimi kwanza
Yaani mimi kwanza
Halafu mimi tena na baadae tena nitaanza mimi katika kila kitu na hii ndio sababu hatupendi mbele.
Chukulia mfano wa jamaa wale 360 wanaotuwakilisha kule yaani ni wao kwanza
V8
Posho
Kutibiwa nje
Biashara
Kwahiyo kiasi kikubwa sana cha pesa ya nchi kinaishia kwa watu wachache mno.
Middle class kwenye mapambano ya uchumi ndio ambao hujikuta kwenye jukumu la kunyanyua uchumi na hii kwa sehemu kubwa ni watumishi wa umma. Sasa mtumishi wa umma nchi hii analima nyanya Chungu na nyanya kukabiliana na ugumu wa maisha.
Tuendelee kutumia toothpick toka nchini China kwaajili ya kunyanyua uchumi wetu
 
Hakuna siku tanzania ilikuwa sawa na China, hata nusu yake tu hakuna siku hio,

Msije jidanganya sijui Tz ilikuwa sawa na China, India au South Korea
 
Haijawahi kuwa sawa na china na haiwezekani kuwa sawa na china
Unafananisha na taifa lililoanza kuifadhi kumbukumbu za maandishi miaka 2000 Bc lilokuwa na VYUO vikuu tangu miaka 2000
Taifa lililokuwa na BUNGE WAZIRI MKUU WAZIRI WA FEDHA WAZIRI WA MIUNDOMBINU(VIWANDA) nk yaani muundo kamili wa NCHI tangu miaka 2000 BC

Taifa ambalo lilianza kufanya gunduzi mbalimbali ambazo zina tija mpka sasa tangu miaka 2000 BC
Unajua kuwa CHINA ndio TAIFA la kwanza DUNIANI kugundua COMPUTER(google ABACUS)
China ni moja ya mataifa ya mwanzo kabisa ya kuunda tools zao ASTRONOMY INSTRUMENT
unajua kuwa meri za CHINA zilikuwa zinatia nanga pwani ya NZANZIBAR KILWA kuleta bidhaa zao kuuza na kwa changeble na GOLD na SILVA

CHINA haikuwahi kutawaliwa NJE ndani
CHINA siku zote ilikuwa inapambana vikari kwa JASHO na DAMU wakoloni wa west na japanese na wakati wote walikuwa wanashinda ingawa ilikuwa inawachukua muda na kucost blood za ndugu zao hwakuwahi kutawaliwa kibwege NCHI yote
MAFANIKIO unayoyaona hayo ya CHINA sasa hayajakuja ndani ya MIAKA 60 yamecost maelfu ya miaka malitre ya blood ya wazarendo wa kichina ni zaidi ya GENERATION 10 nyuma ndio mageuzi yakaja kuleta matokea katika gen hii ya sasa

Hicho unachojidanganya ni UJINGA kabisa
wakati huo BABU zako wanachukuliwa kwenda kupigana VITA KUU YA PILI YA DUNIA na mabeberu wa ULAYA
mababu wa KICHINA miaka hiyo wanaipigania CHINA yao
Utawala wa QING DYNASTY ndio mwishoni mwa miaka ya 1800 kuja 1900 ndio uliieteteresha CHINA baada ya familia ya kifarme kukubari kurubuniwa na kula Rushwa na WESTERN COUNTRY na JAPANESE EMPIRE

MAO ZEDONG akaja kuchange GAME PLAN kwa kuirudisha tena CHINA kwenye NAFASI yake amabyo iliyumba kwa karibu NUSU KARNE

kwa kifupi CHINA imerudi kwenye NAFASI ambapo kwa karibu miaka zaidi ya 60 imejiimarisha vizuri

Hvyo huwezi kufananisha TANZANIA na CHINA ni mbingu na ARDHI haijawai kuwa sawa na haiwezi kuwa sawa
Hiyo miaka unayosema wewe china tayari walikuwa wanaunda Gari zao wenyewe za za JIE FANG(FAW) kwa ALIES ya wao na RUSSIA
STEAM ENGINE za train na kuendeshea MITAMBO viwandani
Electronics Equipment
JOKOFU za BARAFU nk


things chache kati ya nyingi ambazo CHINA alizigundua kutoka miaka 3000 nyuma kuja sasa
WESTERN waliiba TECHNOLOGY zao na kuzihamisha NCHINI kwao

The horse collar
The wheelbarrow
The moldboard plow
Paper money
Cast iron
The helicopter rotor and the propeller
Computer
The decimal system
The seismograph
Matches
Circulation of the blood
Paper
Brandy and Whiskey
The Kite
The rocket and multi-staged rockets
Morden agriculture
Umbrellas
Printing tools
Gunpowder nk
 
Hamna kupiga hatua kwa mfumo wa kishenzi wa uongozi wa hapa Bongo
 
Wacheni uwongo hakuna kipindi tumewahi kuwa sawa au kuwakaribia wachina kiuchumi. Inchi iliyotuzidi miaka karibia 300 Toka ianze kijitambua ndio uipate kiuchumi?

Yaani mwaka 61 tuwenao sawa then mwaka 70 tu waje watujegee tazara?
 
Wakati hata USA haijawahi tambulika na wenye mali huko Red Indians wakikata Mbuga China ilikuwa inaswaga kwa swagger za hapa na pale na kufanya invention za huku na kule.... Watu waliojenga the Great wall of China ndio hao walikuwa na printing press karne na karne huko nyuma most inventions credited to west China walishafanya....
 
Muulize nyerere na viongoz waliofata mpaka saiv utapata majibu
 
Hakuna siku tanzania ilikuwa sawa na China, hata nusu yake tu hakuna siku hio,

Msije jidanganya sijui Tz ilikuwa sawa na China, India au South Korea
Unadhani kwanini bwana mbuzi dume
 
Wee jamaaa acha kutuibiaa

Unasemaje China ilikuwa sawa na tanganyika wakati

china ya kale walijenga ukuta mrefu zaidi duniani,

China ya kale ilikuwa na teknolojia ya silk,

China ya kale walikuwa maarufu dunia nzima kwa vyombo vya Udongo

China ilikuwa na central government tangia miaka ya kina yesu

China ndio wagunduzi wa karatasi
 
Katika uchumi sio suala la kukopi na kupaste eti ili nchi ifanikiwe.

Key factor ya kwanza ni uongozi bora. Kwa uelewa wangu hili ni eneo kuu lililotupiga chenga tangu uhuru hadi sasa ukiachana na maneno matamu ya unazi ( blabla) tena mengine toka kwa wasomi na wanasiasa wanaoheshimika ya jukwaani au katika TV.

Jambo la pili ni kitu inaitwa comparative advantage au hata absollute advantage. Maana yake je wewe una nin mfano sisi labda tuna maliasili mbalimbali.

Tatu huwa nawauliza watu kwa lugha nyepesi je kuna mtu mweusi anaweza kugeuza mchanga/udongo kuwa mashine? Watu weupe wote wanaweza kugeuza mchanga/udongo kuwa mashine mbalimbali mfano injini , mota, nk. Kwa lugha nyingine teknolojia. Hii ndio factor muhimu kwa nchi kuendelea kwa kasi. Sasa hao wenzetu wana vyote viwili teknolojia na utawala bora. Kama nchi ingekuwa na utawala bora tungeweza kutumia maliasili zetu kujenga miundombinu mbali mbali iliyo bora ambayo ingevuta maeneo mengine ya kimaendeleo kama zilivyo nchi za uarabuni walivyofanya kwa kutumia rasilimali moja tu ambayo ni mafuta.
Hao unaowaona wanaitwa wawekezaji kwa kiasi kikubwa ni wapiga madiii ya wizi kwa kushirikiana na viongozi kwa ajili ya kuvuna maliadili na katika sekta zingine huku nchi ikiwa haifaidiki ipasavyo bali kiduchu na wakati huo huo rasilimali hizo zikiisha, hivyo baadae itakuwa ngumu zaidi hapo rasilimali zitakapopungua/kuisha huku watu wakiongezeka kama taifa kupiga hatua za kimaendeleo kama wenzetu wa uarabuni.
Ila hata kama tungekuwa na utawala bora bado tusingeweza kuwa sawa na nchi kama China, Korea, japan sababu kuu ikiwa hatuna teknolojia. Na elewa teknolojia sio suala la kupewa ( imported) tu bali ni kitu kinachotokana na brains za watu wenu ( home grown)

Teknolojia hatuna na utawala bora hatuna pengine toka uhuru hivyo achilia mbali viwango vya china na wengine wao sahau hata kuwa na viwango vya nchi za uarabuni.

Kuendekeza tumbo kumebomoa sana bongo za wasomi weusi na wanasiasa ndio maana dunia yote ya watu weusi kuanzia Afrika mpaka huko Amerika kusini kule carrebian nchi za weusi zina matatizo makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Tuanzie wapi sasa? Mimi kwa uelewa wangu pa kuanzia ni kupigania mgombea binafsi katika ngazi zote za uongozi kwa sababu hao hawatafungwa na mifumo ya vyama ambayo ni corrupt inayowazuia watu waadilifu na wenye maono kupata jukwaa la kisiasa. Pili tabia za hasa watanganyika wakalahoi ( afadhali wazabzibari wanajitambua zaidi) za kuunga mkono hoja kishabiki na kichawa inabidi waachane nazo na kuanza kuchambua na kupima kinachosemwa bila kumuangalia anayekisema.
 
China imepanda na kushuka.

Tanzania kuna wanasiasa wanaamini ubepari utainua nchi
 
point ya maana sana.

Nchi zote tajiri duniani ziliianza kuwa na serikali/central governments miaka zaidi ya 2000.

Sisi waafrika tumeanza kuwa na central government beyond clans just 100 years ago
 
Ni kweli sana China haijawahi kuwa sawa na Tanzania.

China is the oldest civilization duniani, watu wameanza kutumia Farasi kulimia hadi vita miaka buku, but hadi leo wabongo hatujui kuendesha punda
 
TZ kua sawa na china kwa kufikiria haraka ni kitu ambacho hakiwezekani na hakijawahi wezekana.
Inamaana tulivyokua tunapata uhuru idadi ya viwanda vyetu ilikua
Sawa na china? Idadi ya barabara zenye lami, usafiri anga na Technology tulikua sawa kweli??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…