Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Tovuti ya Travel And Tour World ya Marekani hivi karibuni ilitoa makala, ikisema China imekuwa moja ya nchi zinazowavutia zaidi watalii wa kimataifa duniani.
Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2025, idadi ya watalii walioingia nchini China ilizidi milioni 150, ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 17 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imesamehe visa ya muda mfupi kwa nchi nyingi, hatua ambayo imewarahisishia watalii wa kigeni kuingia China kwa kiasi kikubwa. Takwimu zilizotolewa na Idara ya Uhamiaji wa China zinaonesha kuwa mwaka 2025, zaidi ya wageni milioni 30 waliingia China bila visa, ambalo ni ongezeko la karibu asilimia 50 kuliko mwaka 2024.
Tukisema sera ya kusamehe visa imefungua mlango wa kuwakaribisha watalii wa kigeni, basi uvumbuzi wa kidijitali, haswa njia rahisi za malipo ya kuvuka mipaka umeanzisha njia laini inayowawezesha wageni kusafiri bila shida yoyote kote nchini China. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana, watalii walioingia nchini China walitumia zaidi ya RMB yuan bilioni 80 kupitia majukwaa ya malipo ya kidijitali. “Mapinduzi haya ya kidijitali” yamebadilisha sana uzoefu wa wageni, na kuwawezesha kufurahia safari zao, bila ya wasiwasi wa kubadilisha fedha.
Kutoka majengo marefu yanayoingia mawinguni jijini Shanghai hadi mandhari nzuri ya kiasili huko Guilin, watalii wa kigeni wanatembelea miji na vijiji nchini China ili kushuhudia mandhari nzuri ya China na jinsi Wachina wanavyoishi maisha yao. Licha ya mapenzi kwa utamaduni mkubwa wa China, watalii wa kimataifa pia wanapongeza maendeleo ya kasi ya uchumi na jamii vya China.
Ushindani mkubwa wa China katika soko la kimataifa la utalii pia unatokana na mpango wake wa kimkakati. Makala ya Tovuti ya Travel And Tour World ya Marekani inasema, ujumuishaji wa kina wa utamaduni na utalii ndio msingi wa mkakati wa maendeleo ya utalii wa China. Hivi sasa, China inatoa huduma za kiutamaduni ikiwemo maonyesho ya kisanii, maonyesho ya mada mbalimbali, na hata michezo, mambo yanayochanganya utalii na matukio ya kitamaduni yanayovutia. Kutokana na juhudi hizo, China imeshuhudia ukuaji mkubwa wa soko la utalii..
China kuwa moja ya nchi zinazowavutia zaidi watalii wa kimataifa kunatoa ishara wazi kwa dunia: hii ni nchi yenye hadithi ya historia na uhai wa kisasa, yenye sera chanya na uwezo wa uvumbuzi, na pia yenye udhati katika kushirikisha matunda ya maendeleo yake na jamii ya kimataif