SI KWELI China imepitisha Sheria ya kuwanyonga wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja

SI KWELI China imepitisha Sheria ya kuwanyonga wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Inasemekana huko mitandaoni kuwa Serikali ya China imepitisha Sheria ya kupinga Mapenzi ya Jinsia Moja(ushoga), na Adhabu kali kwa yeyote atakaye jihusisha na na Mapenzi ya Jinsia Moja ndani ya nchi hiyo.


1692501059702.png
 
Tunachokijua
Uchina ni nchi iliyoko katika Asia Mashariki. Ni moja ya nchi kubwa zaidi duniani kwa idadi ya watu, ikiwa na zaidi ya bilioni 1.4. China inaongozwa Kikomunisti ikiwa chini ya Utawala wa Rais Xi Jinping. Nchi hii ya Kikomunisti imekuwa na kanuni na sheria zake katika mambo mbalimbali.

Mnamo Agosti 17, 2023 mtumiaji wa mtandao wa X (Zamani Twitter) aitwaye @Dalalikiongoz aliweka andiko katika ukurasa wake linalodai kwamba China imepitisha sheria ya kuwanyonga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Je, ni kweli Serikali ya China imepitisha Sheria hiyo?
JamiiForums imepita vyanzo mbalimbali vya habari Vya China na Mataifa mengine lakini tumebaini kuwa hakuna sehemu yoyote iliyoripoti Serikali ya China kupitisha Sheria ya kuwanyonga watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Aidha, JamiiForums imebaini taarifa pekee kuhusu Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja China iliripotiwa na vituo vikubwa vya Habari ikiwamo Voice of America Mei 22, 2023 na NBC News Juni 13, 2023. Taarifa hiyo ilihusu Serikali ya China kukifunga kituo kikongwe kinatetea haki za Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja mnamo Mei, 2023. Mathalani, sehemu ya habari iliyotolewa na Voice of America iliandikwa:
Kituo cha LGBT cha Beijing kilichokuwa na umri wa miaka 15, moja ya watangulizi wa "harakati ya mwelekeo tofauti wa kimapenzi" nchini China, kilitangaza wiki hii kwamba kimemaliza shughuli zake bila maelezo. Wachambuzi walisema kufungwa kwa kituo maarufu cha haki kuliona kama jambo lisiloweza kuepukika na kielelezo cha mazingira ya kisiasa yenye ukandamizaji unaongezeka nchini China chini ya Xi Jinping.

Taarifa hiyo, inatupa mwanga kuwa watetezi wa haki za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja wanapitia wakati mgumu chini ya utawala wa Rais xI Jinping lakini hakuna taarifa yoyote kwamba Serikali ya Taifa hilo imepitisha sheria ya kuwanyonga.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo Vilivyopitiwa na JamiiForums taarifa hii iliyoibuliwa na @Dalalikiongoz haina ushahidi mpaka sasa.
Hata sisi Tanzania yatufaa tuwaige.shoga pamoja na wauza bandari kwa maslahi ya mwekezaji wanyongwe.
 
Back
Top Bottom