Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Gazeti la The Economist la Uingereza hivi karibuni lilitoa ripoti kuhusu filamu ya China ‘Karibu kwenye Mkahawa wa Dragoni’, ikisema China inatekeleza sera ya kidiplomasia ya Mkahawa wa Dragoni, maana yake ni kwamba China inazingatia zaidi mambo ya kiuchumi na maisha ya watu.
Ukweli ni kwamba, China inathamini sana maendeleo ya kiuchumi yanayotokana na historia yake ndefu ya umaskini, na baadaye kujiendeleza kwa kasi na kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani. Uzoefu huu umeleta uelewa wa kipekee wa China kuhusu mahusiano ya kimataifa: maendeleo si kiashiria cha kiuchumi tu, bali ni msingi wa utulivu wa kijamii, heshima ya watu, na uhuru wa kitaifa. Vile vile, kwa watu wa nchi nyingi zinazoendelea, masuala muhimu zaidi si nadharia za kisiasa, bali ni kama nyumba za watu zina umeme, watoto wanakwenda shule, bidhaa za kilimo zinaweza kuuzwa, hospitali zinaweza kufanya kazi, na watu wanaweza kupata chakula na maji safi ya kunywa.
China pia ina kanuni thabiti katika sera yake ya kidiplomasia. Inasisitiza kuheshimiana, kushirikiana na kunufaishana, na kushikilia kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha masuala ya kisiasa.
China pia imetoa mapendekezo mbalimbali kuhusu mambo ya amani, usalama na maendeleo. Katika miaka mingi iliyopita, kwa kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na majukwaa mengine ya ushirikiano, China imeendelea kuboresha miundombinu ya nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na usafiri, umeme, usambazaji wa maji, shule na hospitali, na kubadilisha maisha ya mamia ya mamilioni ya watu. China pia ni mchangiaji mkubwa zaidi wa kazi za kulinda amani kati ya wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Filamu ya ‘Karibu kwenye Mkahawa wa Dragoni’ inamweka mpishi mmoja wa China katika kanda ya Mashariki ya Kati iliyokumbwa na vita. Kamera haiwaangazii marais au majenerali, bali inawalenga watu wa kawaida wanaojaribu kuendesha mkahawa na kujitahidi kuishi. Chaguo hili linaloonekana kuwa rahisi katika sanaa ya filamu, lakini lina maana kubwa kisiasa. “Kula vizuri” kunatukumbusha kwamba lengo kuu la kisiasa si kutoa kauli tupu za kuvutia, bali ni kuunda utaratibu wa kijamii unaoruhusu watu wa kawaida kuishi maisha ya kawaida.
Gazeti la The Economist linasema kwamba filamu ya Kichina lazima ifuate vigezo vya Magharibi. Hata hivyo, kutambuliwa kwa filamu hakutegemei tuzo za Hollywood, na hadithi yake haina haja ya kulingana na maoni ya nchi za Magharibi. Filamu ya ‘Karibu katika Mkahawa wa Dragon’ imetoa dirisha la kitamaduni, ambalo linaruhusu dunia kuona maono mapana ya Wachina kwa mahusiano ya kimataifa, yaani kuweka amani, maendeleo, kuishi kwa utulivu, na ustawi wa watu wa kawaida kwenye ajenda ya kimataifa.
Hii ndiyo maana ya kina ya dhana ya jamii yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu. Dunia haihitaji vigezo sawa vya mambo ya kidiplomasia, inahitaji majibu halisi kuhusu changamoto mbalimbali zinazokabili binadamu, ikiwemo vita, umaskini, mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na maradhi.