Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Kweli muda unakimbia sana 🕦, kutoka Kuwa movie mpaka maisha Halisi watu watakua na uwezo wa kufunga ndoa na maroboti wa Ai, na Roboti zitakua na uwezo wa kubeba Mimba.
China iko kwenye mpango wa kutengeneza roboti mwenye uwezo mkubwa wa kuweza kuzaa binadamu. Tumbo la uzazi la bandia (artificial womb) litaweza kupokea virutubisho kupitia bomba. Ambapo Roboti ataweza kubeba Mimba ndani ya miezi Kumi kabla ya kujifungua.
Maroboti hayo yamebuniwa na Dk Zhang Qifeng ambaye ni mwanzilishi wa kaiwa Technology ambayo inapatikana Guangzhou nchini China. Ikiwa yote yataenda kulingana na mpango, mfano huo utafanya kwanza mwaka ujao.
Kwa wale binadamu wenye changamoto ya kudhaa wataweza kukodisha Roboti la kubeba mimba. Ambapo ataweza kugharimu yuan 100,000, $13,928.
Bei ya chini kwa sasa Utaweza kuipata marekani kutoka dola 100,000 na kuwa hadi dola $200,000.
#china🇨🇳 #biotech #robotics #womb #kujifungua #chinatech #bongotech255