China Kufadhili Ujenzi SGR Mwanza -Isaka

Hao hao china si ndio hutoa nguo za ccm?
Kuna gazeti limeandika china kugawa mitungi ya gesi ya majumbani kuunga juhudi za SSH.
 
China walikubali kujengela reli yote ya kati, mpaka kigoma, mwanza, mwanza, rwanda na burundi, hii ilikuwa awamu ya nne, awamu ya tano akaja JPM akaanza kuvuruga, anaenda kukopa kwenye vikoba ajenge reli kwa riba ya kibiashara, na mkopo kuanza kulipwa baada ya mwaka. Hovyo kabisa
 
Tanzania na mchi nyingi afrika kiujumla, ni kama demu mzuri mwenye msambwanda lakini kichwani hana akili, sehmu za siri zinateseka, kuja kutahamaki meno kaifikia watoto 6, kila mtoto na baba yake, na pande zote zishatumika.

Ni kama tumelaanika vile, kutwa kuomba misaada, lakini viongozi hawana jitihada zozote zile, matumizi yao hayaendani na shida za tanzania.
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ambao unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyia kazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.

Pia, soma: Kwanini ujenzi wa SGR hapa Mwanza umesimama?

Dkt. Nchemba amesema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Balozi Chen kwamba China kupitia Taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, amesema kuwa Nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo Afrika.

Amesisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.

Amesema mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

View attachment 3119766
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akiwa na ujumbe kutoka ubalozi wa china nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa. Kushoto ni Bw. Chu Kun na kulia ni Katibu wa Balozi, Bi. Ma Shukun.
Sina Imani na serikali yangu
 
Mbona waTz mnataka kucheza na akili zetu sana nyie?

Sijui mwaka jana ama mwaka juzi ule, Nchemba alitutangazia kutiliana sahihi kuingia mikataba ya ubia na Italy kuendeleza ujenzi huo.

Leo tena kawa mChina!

Ina maana fedha za Mtaliano zilipigwa au zilifanya kazi gani?

Mwakani tena tutasikia habari za SGR hiyo hiyo Mwanza-Isaka kukopewa fedha eneo jingine.

Sasa awamu ya kujenga vipande vingine vilivyoainishwa katika kuunganisha EAC, ya Burundi na DRC itakuja kufanyika kweli!

Huu mwemdo wa konokono katika ujenzi wa miradi baada ya kifo chaJPM unabarikiwa na nani?

Na kama imeshindikana kwanini msilitangazie taifa tukaondoa mind set zetu katika jambo hilo?
 
Back
Top Bottom