#COVID19 China kuigeuza Afrika kutoka “jangwa la chanjo” kuwa “chemichemi ya chanjo jangwani”

#COVID19 China kuigeuza Afrika kutoka “jangwa la chanjo” kuwa “chemichemi ya chanjo jangwani”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1629267677175.png


Hivi karibuni televisheni ya Marekani ya CNN ilitoa makala yenye kichwa cha “mjomba wangu anayeishi Kenya alikufa kwa COVID-19 kwa sababu ya kutopata chanjo, lakini naweza kuchanjwa katika duka la dawa nchini Marekani”, ikisimulia upatikanaji wa chanjo usio na usawa duniani, hali ambayo inaitwa na nchi za Afrika kuwa “ubaguzi wa rangi wa chanjo”. Mwandishi wa makala hiyo alisema, wakati nchi tajiri duniani zinapohodhi chanjo kuliko zinazohitaji, Afrika inapambana na virusi bila silaha, basi “tuko pamoja” inakuwa kauli mbiu tupu mdomoni mwao.

Kutokana na athari ya wimbi la tatu la maambukizi na virusi vinavyobadilika vya Delta, mwezi Julai kiwango cha vifo vya COVID-19 barani Afrika kiliongezeka kwa asilimia 80 kuliko mwezi uliotangulia, na kufikia kilele chake tangu ugonjwa huo ulipuke. Wakati huohuo, kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa chanjo na watu kukosa hamu ya kuchanjwa, ni asilimia 1.5 tu ya watu barani Afrika wamechanjwa kikamilifu. Lakini katika sehemu iliyo karibu na mapomoroko ya Viktoria, moja ya maporomoko matatu makubwa zaidi duniani, kuna mji wa maporomoko nchini Zimbabwe, ambapo tangu mwezi Machi watu wa mji huo walipoanza kupwa chanjo ya Sinopharm ya China, hadi sasa watu elfu 21 wamechanjwa, sawa na asilimia 70 ya watu wa mji huo, na kuwa mji wa kwanza kutimiza lengo la kinga ya jumuiya (Herd immunity) nchini Zimbabwe. Katika wimbi jipya la maambukizi lililotokea hivi karibuni, mjini humo watu zaidi ya 150 waliambukizwa, kati yao hakuna aliyekufa; lakini katika mji jirani, kati ya watu 400 walioambukizwa, watu 12 wamefariki dunia. Mbali na hayo, serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa licha ya mji wa maporomoko, hatua kali za “zuio” zitaendelea kutekelezwa kote nchini. Na katika mji huo wa maporomoko, watalii wa nje waliochanjwa wanaweza kuingia na kusafiri, watu wanaweza kula migahawani na vituo vya utalii vinaweza kutembelewa na watalii.

“Kinga mwili” iliyojengwa na chanjo ya China sio tu imeokoa maisha ya watu wa mji wa maporomoko ya Viktoria, bali pia imesaidia kurudisha shughuli za uzalishaji na maisha katika hali ya kawaida, na huu ni mfano wa matokeo ya ushirikiano wa chanjo kati ya China na Zimbabwe, na kati ya China na Afrika. Hadi sasa China imetoa dozi milioni 800 za chanjo kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100, kiasi ambacho ni mara 84 zaidi kuliko Marekani na asilimia 227 zaidi kuliko Ulaya. Na kati ya nchi zilizopokea msaada wa chanjo ya China, theluthi moja ni nchi za Afrika. Katika mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu ushirikiano wa chanjo dhidi ya COVID-19 uliofanyika hivi karibuni, serikali ya China ilitangaza kuwa itajitahidi kutoa dozi bilioni 2 za chanzo hiyo kwa nje mwaka huu, na pia kufadhili dola za kimarekani milioni 100 kwa mpango wa COVAX ili kuziwezesha nchi zinazoendelea kupata chanjo.

Hivi sasa, uwezo wa uzalishaji wa chanjo hiyo wa China ni dozi bilioni 5 kwa mwaka, kwa hivyo dozi bilioni 2 zilizoahidiwa na China zina maana kuwa kila mchina anapochanjwa dozi mbili za chanjo, China inatoa dozi moja kwa nchi za nje. Hata hivyo, dozi hizi bilioni 2 zinaweza kukidhi mahitaji ya asilimia 10 tu ya watu wa nchi nyingine, na dunia inahitaji juhudi za pamoja za Marekani na Umoja wa Ulaya wenye uwezo wa kuzalisha chanjo. Lakini kama mwandishi wa makala hiyo iliyochapishwa kwenye CNN alivyosema, kwa mujibu wa makadirio ya gazeti la The Washington Post, chanjo zilizohodhiwa na Marekani zinaweza kuwatosheleza watu milioni 750, lakini Marekani ina jumla ya watu milioni 260 tu. Wakati huohuo mvutano kati ya makampuni ya kuzalisha chanjo ya Marekani na Umoja wa Ulaya pia umekwamisha mchakato wa usambazaji wa chanjo kwa nchi zinazoendelea haswa nchi za Afrika.

Hivi sasa, mbali na kujenga na kupanua mnyororo wa uzalishaji wa chanjo katika nchi za Afrika, makampuni ya kuzalisha chanjo ya China ambayo imeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani kwa matumizi ya dharura, pia yanafanya utafiti juu ya virusi vinavyobadilika vya Delta, na kampuni ya Sinovac inapanga kutoa ombi la matumizi ya dharura kwa chanjo yake mpya dhidi ya virusi vya Delta hivi karibuni. Ikiwa nchi muhimu zaidi ya kutoa chanjo duniani, China itasaidia kuharakisha upatikanaji wa chanjo barani Afrika na kuigeuza Afrika kutoka “jangwa la chanjo” kuwa chemichemi ya chanjo jangwani.
 
Back
Top Bottom