CHINA: Marekani iwajibike kwa kueneza UKIMWI Duniani na seasonal flue mwaka 2009 maana chimbuko la H1N1 na UKIMWI ni Marekani

CHINA: Marekani iwajibike kwa kueneza UKIMWI Duniani na seasonal flue mwaka 2009 maana chimbuko la H1N1 na UKIMWI ni Marekani

It is up to Everyone. Stop buying anything that comes out of CHINA. Only people can boycott them by NOT buying their crap and putting pressure on companies that do by putting them out of business.
 
Je, Marekani imelipa hasara kutokana na majanga ya H1N1, UKIMWI na msukosuko wa fedha duniani?

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, Marekani inapaswa kufahamu kuwa adui wao ni virusi, sio China, kwani kama nchi nyingine, China pia ni mwathirika wa maambukizi ya virusi vya Corona.

Geng amesema hayo baada ya Rais Donald Trump wa Marekani jana kusema China inapaswa kuwajibika kwa ueneaji wa virusi hivyo.

Geng amesema virusi ni adui wa binadamu wote, na vinaweza kutokea wakati wowote na mahali popote, na China ni mwaathirika wa virusi hivyo. Ameongeza kuwa, hakuna aliyeiwajibisha Marekani kwa majanga yaliyoanzia nchini humo kama mafua ya H1N1 yaliyotokea nchini Marekani mwaka 2009 na kuenea katika nchi 214 duniani, na kusababisha vifo vya watu laki mbili, na pia mgogoro wa kifedha uliotokea mwaka 2008 nchini Marekani na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi duniani, aidha ugonjwa wa UKIMWI pia ulitokea kwanza nchini Marekani.

Geng amesisitiza tena kuwa, kwa mshikamano na ushirikiano tu, ndio jumuiya ya kimataifa itashinda virusi vya Corona, ameitaka Marekani kuacha kuipaka matope China, na kujishughulisha vizuri zaidi na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.
Hawa mabeberu wanakata tawi walilolikalia kwa tamaa za u-superpower, ona sasa dunia inasambaratika tunakosa wote
 
Truth be told; China walifanya uzembe kwenye ku-handle hili tatizo. Wangekuwa wawazi tangu mwanzo huenda hali isingeharibika kiasi hiki.
 
Hizo programme Za UKIMWI zimeanza lini? Dawa Za kufubaza virusi vya UKIMWI zimepatikana lini? Waliopata UKIMWI mwanzoni waliteseka sana miaka hiyo, hakuna fidia itakayoyosheleza madhila ambayo familia nyingi zimepitia kwa gonjwa la UKIMWI.
naamini dawa ya COVID-19 itapatikana mapema kuliko ya UKIMWI.
Halafu tunaambiwa tunapewa msaada wa dawa Za UKIMWI kwamba badala ya kusema wanalipa wanasema ni Masaada.
Watoto yatima hawa tunasomesha sie kwa kujinyima wewe unasema dawa Za kufubaza makali ya UKIMWI zinazotolewa kujikosha kwamba ndio malipo yetu ya kuletewa UKIMWI.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na ndo maana mwanzoni nilianza kwa Kusema "Atleast" Marekani inafanya Kitu Kufidia kosa Lao. Atleast. Unaona kabisa they are doing something kama kutoa pole for what they did.

Na ni msaada ndio, kwani mkuu US ingeamua kuignore kutotoa Hizo Arv Bure na elimu juu ya ukimwi waafrika wangefanya Nini? Tungejipanga tungeenda Kuwapiga? Tungeishia kulalamika tu. Kumbuka hizo ela ni kodi za wa wamarekani. Ni wameamua tu.
 
Mchina hamfahamu Mmarekani vizuri. Marekani ataacha historia mbaya sana kwa China ,muda utasema
 
It is up to Everyone. Stop buying anything that comes out of CHINA. Only people can boycott them by NOT buying their crap and putting pressure on companies that do by putting them out of business.
Hizi ni dalili kuwa umevalia chupi "made in china".
 
Na ndo maana mwanzoni nilianza kwa Kusema "Atleast" Marekani inafanya Kitu Kufidia kosa Lao. Atleast. Unaona kabisa they are doing something kama kutoa pole for what they did.

Na ni msaada ndio, kwani mkuu US ingeamua kuignore kutotoa Hizo Arv Bure na elimu juu ya ukimwi waafrika wangefanya Nini? Tungejipanga tungeenda Kuwapiga? Tungeishia kulalamika tu. Kumbuka hizo ela ni kodi za wa wamarekani. Ni wameamua tu.
USA anapora kila mahali na kuchochea vita ili aibe rasilimali hasa madini, gesi asilia na mafuta. Na Afrika ndiye muathirika mkuu wa huu wizi na mauaji.

Tatizo la binadamu mweusi ni msahaulifu na mjinga.
 
Mzee hizo Points ni za darasa la tano huko kipindi hicho akili haijakua ndo points tulizokuwa tunatumia kuonekana Bright mbele ya umma.

Hata Tanzania mkiwa Superpower Mtafanya The Same Anayofanya Marekani and Maybe Even Worse. Ni nature ya Dunia ilivyo. "Survival Of the Fittest". Kwani waafrika wenyewe kwa wenyewe hamuibiani? Rwanda anafanya Fitna Gani pale Uganda? Sasa ukiwa wa hovyo hovyo utatengeneza Chuki ya Bure uumwe vidonda vya tumbo kumbe ndo mfumo wa Dunia.

Back
Top Bottom