China, Marekani na Ulaya walitozana sana kufikia hapo. Maendeleo ni gharama, serikali isigeuke nyuma!


Mfumo wetu unategemea sana Kiongozi mmoja. Akiwa dhaifu, asiye na maono na uthubutu nchi yote inakuwa dhaifu.

Kuna umuhimu mkubwa wa katiba mpya. Kinga kuondelewa, viongozi kuwajibishwa na sheria wasipowajibika. Mahakama, Bunge na jeshi la polisi kuwa huru.

Uteuzi ufuate taaluma ya mtu, weledi na maadili. Pia kuwepo na confirmation hearing.

CV, historia ya mteuliwa itajadiliwa na kuchunguzwa na kuthibitishwa na baadaye kukubaliwa au kukataliwa. Hapo tutapata watu makini kwenye uongozi.
 
Maendeleo ya taifa hupatikana kwa kuweka mazingira na sera za kuwawezesha wananchi kuwa matajiri na wala siyo kuwakamua.
Ili uwe tajiri ni lazima ukusanye kutoka kwa wengine na siyo kubadilisha mfuko mmoja kupeleka mwingine (utajiri wa nchi ni mapato ya serikali pamoja na ya wananchi).
Kinachofanyika ni kutoa kwa wananchi (mfuko mmoja) kupeleka kwa serikali (mfuko mwingine).
Tanzania inatakiwa kupata utajiri kutoka Msumbiji, Malawi, Zambia, DRC, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na Comoros kwa kuanzia.
Viongozi wanatakiwa kuwaza hivi, na baadaye kuongeza wigo hadi mataifa ya mbali.
Fikra za maendeleo kupitia tozo kwa wananchi ni za kale hata kabla ya ukoloni zilishapitwa na wakati.
Utumwa na ukoloni ni matokeo ya watu wenye akili za kimaendeleo kuondokana na tozo nyingi kwa raia wao.
Hata hivyo, haya ni mawazo ya kujadiliwa na taasisi za usalama na intelijensia zaidi kwa faida na mustakabali mwema wa taifa.
 
Bogus kabisa
 
TUJITEGEMEE, hongera sana...kazi iendelee. Naona kulingana na mawazo ya mlio wengi wapinzani ndio wanaisoma namba! Kosa walilolifanya naambiwa ni kufikiri wanaweza wakavuna nyanya kwenye shamba la sukuma wiki. Ubahatishaji wao wa awali wa jema na safi kupatikana kwenye dampo limeangukia pua na sasa kejeli zinaelekezwa kwao kwa upofu wao na ugonjwa wao katika uhuishaji!

Dhahabu haikutukwamua, almasi haikutukwamua, Tanzanite haikutukwamua, mafuta ya gesi hayakutukwamua, maliasili na utalii hazikutukwamua, viwanda na mikopo hazikutukwamua ila sasa tunaye mama. Mama aliyetulia na hakurupuki hata akizungukwa na mafield marshal kama madelu katulia tuli! Tozo, miamala na luku lazima zituvushe hata kama wapinzani wanasoma namba!

Nimekaa nikajiuliza...hivi hawa wapinzani wana mihuri? Wamepigwa mihuri na nani? Heri hata wakati wa mkoloni kwani waliopigwa mihuri ni mifugo tu. Hawa wapinzani watakamuliwa hadi wahame nchi, nasikia milango ya Burundi iko wazi. Tatizo moja...wengi wa wapangaji ni waajiriwa na wengi wa waajiriwa wanatoka kambi ya kijani kwani sifa kuu ya kupata ajira ni utii kwa chama.

Wanaoteseka hawalii, wanaolia ni wenye neema! Je wewe ndugu yangu TUJITEGEMEE, uko upande gani? Kama nawe kwa bahati mbaya unaisoma namba karibu, kama ni mwenye nyumba au mpangaji karibu, kama ni mkulima, mfanyakazi au mfanya biashara karibu na kama unaishi kijijini, mjini au jijini karibu...kama kokoro, serikali ya mama haina macho, haina sikio wala hisia, inazoa tu!
 
Ni andiko zuri hili, lakini hujaeleza juu ya ubadhirifu/ matumizi mabaya ya pesa zinaochangwa. Hii inafany andiko kuwa la kipumbavu zaidi tangu kuwepo kwa dunia.Period!
 
Hawakuwa na viongozi "wapumbavu,wabinafsi na walafi" kama wetu.
Unakosema China ukileta umwigulu unakula shaba mapema tu.U-mahera ndiyo usiseme kabisaaa!
 
Moja kati ya bandiko la kipuuzi katika historia ya jf. Unajua uchina, usa na europe wanavyotoza hizo kodi? Hakuna utozaji wa kodi mara mbil mpaka tatu kwenye kitu kimoja..ww ni hewa kabisaa kichwani.
Uzuri wa hili tunapigwaa wotee yaaan..
 
Naam Mkuu, ni kweli... Kazi iendelee!

Mkuu, Mama ameishaTushukuru sisi raia kwa kukubali baadhi ya mambo ambayo wasaidizi wake waliyapanga kwa ajili ya kuhakikisha tuna kuwa wazalendo kweli kweli. Tumezoea mwana kumshukura Mama, lakini Mama akimshukuru mwana kwa 'kukubali' mambo ya uzalendo 'raha' iliyoje kwa mwana!!!

Mkuu, Yaani uzalendo huu! Unanikumbusha msemo wa watu wa madhehebu, wa kuwa sadaka ama zaka yenye baraka ni ile unatoa roho inauma!!

Mkuu Najaribu kukwepa swali lako ujue, lile la kuhusu niko upande wa wanaoteseka hawaliI ama wanaolia wenye neema!
 
Watanzania hatukatai tozo ila je inatumika ipasavyo au ndo hizi wanazojengea daraja bovu la mbao kwa mil 31 na kule hazina wanagawana mil 400 kwa siku na yule waziri katutia hasara mwenye ile tour yake aliyoenda na wasanii
 
Umesema yote mkuu. Kwa kuongezea, wanasema. "Nchi inayotaka kuendelea kwa kutoza watu wake kodi ni sawa na mtu aliye ndani ya ndoo kisha anajaribu kujinyanyua."
 
Wewe ni fala ama? Tozo za kumuumiza masikini halafu kenge mmoja anakuja kuzila hizo pesa adhabu yake alipe faini milioni 8? Utakuwa mla TOZO mwehu wewe
 
Andiko limenishawishi na kubadili mtazamo wangu juu ya tozo ...
Hakika mjenga nchi ni mwanachi mwenyewe.... Watanzania wenzangu tulipe Kodi sanjani na kusupport tozo mbalimbali ili nchi yetu isonge mbele kimaendeleo...tujitoe kwa Hali na mali vizazi vijavyo vije kujivunia Tanzania yetu..
 
tunajuana chief, walipa tozo na wakusanya tozo... walipa tozo tupo huku uraiani na wakusanya tozo wanatembelea maV8, watoto wawakusanya tozo wanasomo feza... wakusanya tozo wanamichepuko kila kona ya nchi, wakusanya tozo wanamiradi kedekede, wakusanya tozo hawativiwi mwananyamala, mwisho wasiku kupitia masikio yetu tunaambiwa na sieijii tumepigwa nk.... HAPO NDIO SHIDA ILIPO..
 
Kwao ukila kodi za wananchi hawana msamaha hata kama ni raisi utashughulikiwa.Kule wananchi wao maendeleo wanayaona
Huku fisadi ufungwa miaka michache plus fine mbuzi

 
Watanzania waelewe, serikali haina vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kodi ya Watanzania.
Hii ni kauli kabisa inatoka kwa mtu mwenye akili timamu? Kweli CCM ni Chama Cha Mapunguani.
Tuna chuma kimelala tu ardhini kule Liganga na Mchuchuma, tuna import hadi sindano za kushonea kwa mkono wakati madini ya chuma tunayo. Huu ni upunguani wa CCM.

Mnahubiri viwanda, hamuyaishi mahubiri yenu, uzeni ndege hizo zinazo generate hasara ya billions of money, endelezeni project za kuzalisha chuma, mnaweza mkauza kwa kuanzia kama raw materials, na baadae mkiendelea mkaanza kuuza finished goods.

Ujinga wenu na uvivu wenu wa kufikiri unawatesa wananchi kwa makodi yasiyo nankichwa wala miguu.

Mmeushupalia tu uchawi na ushirikina, mnakimbiza Mwenge mnatumia mabilioni, nyie ni mataahira kabisa.

Kama Mwenge unaweza kuleta amani pasipo na amani, kwanini mwaka 1978 wakati majeshi ya Idd Amini yamevamia Kagera hamkuupeleka ukalete amani?

Shame on you mama D, USSR chinembe, Mwigulu Nchemba na mazezeta wote wa CCM
 
Wakati wao wanatozana Sisi tuliacha lini kutozana? Wenzetu wanatozwa hela zinafanya kazi. Subiria miaka 10 ijayo utafute kile kilichofanywa kutokana na hizo tozo. Ukikiona untag
 
...kama kokoro, serikali ya mama haina macho, haina sikio wala hisia, inazoa tu!
Swali lako Mkuu, limenitafuna karibu usiku kucha. Kiasi niliangukia kwenye video ( nimeiambatanisha hapa chini) ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ikimuonyesha akizungumza na wananchi wa Uganda wakiongozwa na rais wao Museveni huko huko Uganda alipoalikwa.

Kuanzia dakika ya 6 mpaka ya kumi Mwalimu alizungumza maneno mazito sana. Maneno ambayo yana maana sana nyakati hizi kwa wale wenye nia ya Kujitegemea kikweli kweli kama Taifa.

Karibu kuifuatilia video hii .Utalazimika kuiangalia kupitia ukurasa wa YouTube, kwa hiyo click link ya " Whatch on Youtube" kwenye weusi wa picha iliyowekwa hapa chini.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…