China, Marekani na Ulaya walitozana sana kufikia hapo. Maendeleo ni gharama, serikali isigeuke nyuma!

Mimi napingana na wewe kwa sababu ,
huwezi kumlimbikizia masikini utitili wa kodi wakati kipato chake ni kidogo,
Mzunguko wa bado in mdogo mno,na watu wengi hawana pesa mfukoni, na hii ni sawa na kumkamua ng'ombe aliyekonda maziwa wakati humlishi vizuri
 
Mbaya zaidi ubadhirufu utaofanya na fweza za ubadhirifu huo ndio zitatumika kutukandamiza wanyonywaji vizuri siku sii nyingi.
Tuna mbuga za wanyama madini kibao.. gesi makaa ya mawe bandari.. hela zake zinaenda wapi!!!!
 
Tunahitaji maendeleo sasa,
 
Tatizo hizo fedha zinatumiwa kwa mambo ya hovyo kama:
utekaji, ubambikaji kesi, wizi, nk
 
Naomba kuelewa..., Hivi kabla ya hizi tozo za miamala (ambazo serikali inachukua mapato zaidi hata ya mwekezaji mwenyewe) kulikuwa hakuna kodi au watu walikuwa hawalipi kodi ?

Kumbuka kinachofanyika sasa ni kuhatarisha uhai wa hata hizo Biashara..., hata ng'ombe unamlisha kwanza ashibe kabla ya kumkamua maziwa...

 
Hatukatai tozo bali kiwango na unyumbulifu wake (isiwe kila pahala ni tozo tu).
 
Akijibu niambie
 
Kwa hiyo leo mnajifananisha na mashoga?
 
Suala la maendeleo hakichagui na lina manufaa kwa wote, halina mjadala,kujenga shule mtoto was kitanzania asome unataka siasa? Mama mjamzito yuko hoi kitandani unampa siasa atakuelewa?
Kwa hiyo ni shule na sio daraja la jangwani tena?
 
Kwa nyongeza tu, mwenye kutaka kuthibitisha hayo aangalie Documantary ya George Washington na Kodi za mvinyo (wine). Kuliaka moto lakini leo ndio imewapa kujulikana na kutoa misaada kwa wengine.

Usikose, tafadhali itafute na iangalie.
 
Kwa nyongeza tu, mwenye kutaka kuthibitisha hayo aangalie Documantary ya George Washington na Kodi za mvinyo (wine). Kuliaka moto lakini leo ndio imewapa kujulikana na kutoa misaada kwa wengine.

Usikose, tafadhali itafute na iangalie.
Asante ndugu
 
Hakuna ubaya wowote kuchangia maendeleo lakini sio maendeleo ya Majengo makubwa makubwa mfano kwann hauimarishi vituo vya Utafiti ili vituibulie mambo mapya tuyatumie kujenga uchumi...

Tunazuiaje Wizi wa hiyo michango kwa mfano....

Tunachofanya kinaendana na Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2025???

Kwa Hiyo kuna mambo meengi ya Kufanya kwa kukusanya mawazo na kuyafanyia kazi..Tatizo letu anaewaza na kuamua ni mtu mmoja au kikundi flani ukionekana unaenda Tofauti basi utahojiwa weee..Lakini wanasahau zama huja na kubadilika anaehoji leo kesho atahojiwa mfano ni Pole pole.
 
Hao uliowataja walikamuana na hela ilifanya kazi iliyokusudiwa.

Kwetu hapa subiri taarifa ya CAG mwakani ubadhirifu wa kufa mtu na hakuna anawajibika.

Kwenye miamala ya simu, mafuta na umeme kuna VAT sasa tozo za nini wakati tunalipa kodi.
Kwa kweli kama ubadhirifu hautakuwepo Tozo itakuwa ni sahihi lakini kama Ubadhirifu utakuwepo basi hizi Tozo zitakuwa ni uonevu tu,
 
Huwezi kupata maendeleo ya nchi kwa kuwakamua wananchi wako kupitia tozo - sahau.

Marekani na hata hao wachina hawajafika hapo walipo kwa kutumia tozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…