China na Afrika kutotenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri

China na Afrika kutotenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
timg (2).jpg

Hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alitembelea nchi tatu za Afrika, Kenya, Nigeria na Senegal. Katika ziara hiyo, alijaribu tena kuichafua matope China ili kuimarisha ushawishi wa Marekani barani Afrika, lakini China na Afrika haziwezi kutenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri.

Katika ziara hiyo, Blinken alisema “Marekani imerudi”, akidai kwamba mikataba ya ujenzi wa miundombinu kati ya Afrika na “baadhi ya nchi” huzifanya nchi za Afrika kushindwa kudhibiti madeni, ila wachambuzi wengi wanaamini kuwa, kauli hiyo inalenga pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Lakini kama Blinken alivyohisi barani Afrika, mshikamano, urafiki na ushirikiano wa karibu kati ya China na Afrika ni vitu visivyoweza kupuuzwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama alimjibu Brinken moja kwa moja, akisema fursa kubwa katika ushirikiano na China zinaonekana, nchi ambayo ina uzoefu mkubwa katika miradi mikubwa ya uhandisi na miradi ya miundombinu. Gazeti la Citizen la Afrika Kusini limesema, Marekani ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, lakini hali hii haimaanisha nchi hiyo inaweza kuwafundisha viongozi wa nchi za Afrika namna ya kufanya, na nchi za Afrika zina haki ya kuchagua marafiki zake.

Kwa miaka mingi iliyopita, China imekuwa na ushirikiano mzuri na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali, na kupata mafanikio mengi makubwa. Kwa upande wa biashara, China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka na kufikia dola bilioni 200 za Kimarekani mwaka 2020 kutoka dola bilioni 10 ya mwaka 2000, na kuongezeka kwa mara 20. Kwa upande wa miundombinu, Afrika imekuwa soko la pili la China kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu katika nchi za nje. China imetekeleza miradi mingi ya miundombinu kwa kuendana na mahitaji ya nchi za Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa, tangu kuanzishwa kwa FOCAC, makampuni ya China yameongeza na kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za reli na karibu kilomita 100,000 za barabara barani Afrika, na kutoa nafasi zaidi ya milioni 4.5 za ajira kwa wenyeji katika nchi husika. Uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 43.4, za kimarekani, na kushika nafasi ya nne kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika.

Sasa tujiulize, nani ni rafiki wa kweli wa Afrika? Hapa kuna jibu. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na shirika maarufu la uchunguzi wa maoni la Afrika la Afrobarometer inaonesha kuwa, ushawishi wa China barani Afrika unashika nafasi ya kwanza duniani, mbele ya Marekani, mashirika ya kikanda, mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa dhati kati ya China na Afrika kwa miaka mingi.

Kitu kinachohitajika na Afrika ni uaminifu, sio mahesabu. Marekani inapaswa kusikiliza ushauri wa mtaalamu wa Afrika Kusini Eric Orland, ambaye amesema kushindana na China kila wakati ni mchezo unaoelekea kushindwa kwa serikali ya Marekani, ambayo inapaswa kuzingatia hatua zake zinazoweza kuisaidia Afrika kihalisi.
 
Sijasoma hii takataka ila nishaelewa na ww ni takataka.hata muda wa kujibu sijui nilitoa wapi.
 
China ni kama chatu, taratibu inaimeza Afrika kwa sasa. Urafiki wa china na Afrika ni kivuli cha unafiki ili kuficha ulaghai unaoendelea.
 
Entebbe Airport na wachina vipi tena?
Kwani Serikali ya Uganda imewahi kumkalamikia nani kuhusu suala hilo - tukisema acheni kusikiliza propaganda za magharibi kuhusu ujio wa Wachina barani Afrika hamtaki kutusikiliza - someni majibu ya waziri wa Nigeria alivyo mjibu Waziri wa Merikani akimunanga Mmerikani huyo asilete unafiki wa kujaribu ku-draw a wedge kati ya bara la Afrika na Uchina - kaelezwa urefu wa kilometa za barabara ambazo Wachina wamejenga barani Afrika, viwanda na idadi za ajira, reli, mabwawa ya kuzalisha umeme, mawasiliano kwa njia za simu (ujenzi wa mkonga wa mawasiliano, usambazaji wa optic fibre nchi nzima na jirani) nk.

Swali ni, je,mataifa ya magharibi specifically Merikani imewahi kulifanyia nini bara la Africa kitu gani cha maana kimaendeleo zaidi yakukazania kuanzisha bases za kijeshi na kulazimisha viongozi wa Kiafrika kushirikisha majeshi ya kimerikani kwenye mazoezi ya kijeshi yasiyo kuwa na kichwa wala miguu, masaa yote wanawaza vita tu na kutaka kushirikisha mataifa mengine kwenye endless proxy war s kila pembe ya Dunia.

Baadhi ya Waswahili wanajifanya kusahau kila kitu kuhusu maendeleo makubwa yaliyo letwa na Wachina barani Afrika, badala yake Waswahili nao wanaungana na kampeini chafu za Wazungu hasa hasa Wamerikani katika kuwasema sema vibaya ujio wa Wachina barani Afrika - Wazungu wanalichukulia bara la Afrika kama their own backyard.
 
All races its about market! Kwani kila kitu au ujuzi mwisho wake ni soko la ubunifu husika, China siyo mchoyo hata kwenda kwake ni rahisi, yupo openly kila bidhaa utapata Kwa bei ya pesa uliyonayo! Anaufahamu uchumi wa Afrika, na vipato vya waafrika
 
Kwani Serikali ya Uganda imewahi kumkalamikia nani kuhusu suala hilo - tukisema acheni kusikiliza propaganda za magharibi kuhusu ujio wa Wachina barani Afrika hamtaki kutusikiliza - someni majibu ya waziri wa Nigeria alivyo mjibu Waziri wa Merikani akimunanga Mmerikani huyo asilete unafiki wa kujaribu ku-draw a wedge kati ya bara la Afrika na Uchina - kaelezwa urefu wa kilometa za barabara ambazo Wachina wamejenga barani Afrika, viwanda na idadi za ajira, reli, mabwawa ya kuzalisha umeme, mawasiliano kwa njia za simu (ujenzi wa mkonga wa mawasiliano, usambazaji wa optic fibre nchi nzima na jirani) nk.

Swali ni,je,mataifa ya magharibi specifically Merikani imewahi kulifanyia nini bara la Africa kitu gani cha maana kimaendeleo zaidi yakukazania kuanzisha bases za kijeshi na kulazimisha viongozi wa Kiafrika kushirikisha majeshi ya kimerikani kwenye mazoezi ya kijeshi yasiyo kuwa na kichwa wala miguu, masaa yote wanawaza vita tu na kutaka kushirikisha mataifa mengine kwenye endless proxy war s kila pembe ya Dunia.

Baadhi ya Waswahili wanajifanya kusahau kila kitu kuhusu maendeleo makubwa yaliyo letwa na Wachina barani Afrika, badala yake Waswahili nao wanaungana na kampeini chafu za Wazungu hasa hasa Wamerikani katika kuwasema sema vibaya ujio wa Wachina barani Afrika - Wazungu wanalichukulia bara la Afrika kama their own backyard.
Umevuta bangi mbichi mixer vishabu?
 
Dawa ya Deni ni kulipa. Lakini Rafiki wa kweli wa Africa ni China, hao kina bugaluu washapitwa na wakati.
 
Dawa ya Deni ni kulipa.Lakini Rafiki wa kweli wa Africa ni China,Hao kina bugaluu washapitwa na wakati.
Rafiki anayeleta viwanda vya yeboyebo na ajira za 5000 kwa siku. Na viwanda vyenyewe vimefichwa uswahilini maana yake ni wakwepa kodi pia.
 
Kwani Serikali ya Uganda imewahi kumkalamikia nani kuhusu suala hilo - tukisema acheni kusikiliza propaganda za magharibi kuhusu ujio wa Wachina barani Afrika hamtaki kutusikiliza - someni majibu ya waziri wa Nigeria alivyo mjibu Waziri wa Merikani akimunanga Mmerikani huyo asilete unafiki wa kujaribu ku-draw a wedge kati ya bara la Afrika na Uchina - kaelezwa urefu wa kilometa za barabara ambazo Wachina wamejenga barani Afrika, viwanda na idadi za ajira, reli, mabwawa ya kuzalisha umeme, mawasiliano kwa njia za simu (ujenzi wa mkonga wa mawasiliano, usambazaji wa optic fibre nchi nzima na jirani) nk.

Swali ni,je,mataifa ya magharibi specifically Merikani imewahi kulifanyia nini bara la Africa kitu gani cha maana kimaendeleo zaidi yakukazania kuanzisha bases za kijeshi na kulazimisha viongozi wa Kiafrika kushirikisha majeshi ya kimerikani kwenye mazoezi ya kijeshi yasiyo kuwa na kichwa wala miguu, masaa yote wanawaza vita tu na kutaka kushirikisha mataifa mengine kwenye endless proxy war s kila pembe ya Dunia.

Baadhi ya Waswahili wanajifanya kusahau kila kitu kuhusu maendeleo makubwa yaliyo letwa na Wachina barani Afrika, badala yake Waswahili nao wanaungana na kampeini chafu za Wazungu hasa hasa Wamerikani katika kuwasema sema vibaya ujio wa Wachina barani Afrika - Wazungu wanalichukulia bara la Afrika kama their own backyard.
Hivyo vyote wamejenga bure?.
 
Hivyo vyote wamejenga bure?.
shida sio kujenga shida wazungu hawatak kufanya biashara nasi ya kutusogeza hata kdg , wao wamejikita kwny kudhamini vikundi vya kihuni kuchafua amani yetu ili waibe vingi kwa gharama ndogo , tofauti na uchina anatunyonya ila anatupuliza
 
Naungana na Uchina kupinga ubeberu wa Magharibi dhidi ya Maendeleo ya Kiuchumi yaliyoletwa na Uchina Barani Afrika.

Leo hii ukienda kuulizia Bei za Pikipiki za HARLEY DAVISON za Marekani au KAWASAKI za Japan Bei Yake Ni Zaidi ya Tsh 40M. Hiyo Bei unapata Probox karibu 3 za Kichina unapiga kazi huko Kijijini.

Ni Watanzania wachache(Mabwanyenye )ambao wanaweza kununua hiyo Pikipiki. Mchina Kaleta Pikipiki za Bei nafuu Kama KINGLION kwa Bei ya Tsh 2M. Leo hii Mpaka Kijijini ambako kulikuwa hakufikiki leo kunafikika.

Ukija kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara ndio siwezi hata kuongelea kabisa. Wakati Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani ANTONY LINKEN anaelekea Senegal Kuichafua Uchina alipita kwenye SUPER HIGHWAY ambayo inajengwa na Uchina nchini Senegal Mpaka yeye mwenyewe akashangaa.
 
Back
Top Bottom