China na Afrika zajenga kielelezo cha ushirikiano wa Kusini na Kusini

China na Afrika zajenga kielelezo cha ushirikiano wa Kusini na Kusini

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
3.png



Likiwa kama bara lenye idadi kubwa ya nchi zinazoendelea, Afrika inaweza kusemwa kuwa "chanzo cha msingi" wa diplomasia ya China. Ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na moja ya nchi za Kusini, China imefanya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kirafiki kati ya Kusini na Kusini na nchi za Afrika, kitu ambacho ni sehemu muhimu ya diplomasia ya ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.



"Watu wenye mitazamo sawa hawaoni milima na bahari kama kikwazo cha umbali wao." Ingawa China na Afrika zimetengana kwa umbali wa maelfu ya maili kijiografia, mawasiliano ya kirafiki kati yao yana historia ndefu. Historia zinazofanana na majukumu ya kihistoria ya pamoja yameziunganisha kwa karibu China na Afrika, na kuanza kukumbatia njia ya ushirikiano wa kunufaishana.



Kutoka kuamuliwa kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kina wa kimkakati kati ya China na Afrika katika Mkutano wa Kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2015, kuamuliwa kujengwa kwa pamoja jumuiya ya karibu zaidi kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2018, hadi kwenye Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2021, pande mbili ziliamua kushikana mikono na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya; Na kutoka "Mipango Kumi ya Ushirikiano" na "Hatua Nane" hadi "Miradi Tisa" ya mwaka jana, katika miaka kumi iliyopita, chini ya utaratibu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, uhusiano kati ya pande mbili umeingia katika kipindi bora zaidi cha historia. Katika kipindi hicho, mambo mbalimbali ya ushirikiano yaliendelea kutekelezwa. Wakati huo huo, China imeunganisha Pendekezo la“Ukanda Mmoja, Njia Moja”na Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 pamoja na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030, ili kuhimiza maendeleo endelevu ya muda mrefu ya Afrika. Kwa sababu juhudi za dunia za kufikia malengo hayo zinaweza kufanikiwa tu kama Afrika itafanikiwa



Katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona, China na Afrika zimeonyesha kielelezo cha mshikamano na ushirikiano wa Kusini-Kusini na kuondokana na matatizo kwa pamoja. Mwezi Juni mwaka 2020, China ilifanya mkutano maalum wa kilele juu ya mshikamano na kupambana na janga hilo kati ya China na Afrika, na kuwa nchi ya kwanza duniani kufanya mkutano na bara la Afrika wa kukabiliana na janga hilo. China imetekeleza kikamilifu ahadi yake thabiti ya kufanya chanjo dhidi ya COVID-19 kuwa bidhaa ya umma kote duniani. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, China ilikuwa imetoa karibu dozi bilioni 2 za chanjo hiyo kwa jumuiya ya kimataifa.



Miaka 50 iliyopita, nchi za Afrika zilibeba jukumu muhimu sana katika kuhakikisha China inarejeshewa kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa. Tangu wakati huo, China na Afrika zimekuwa washirika muhimu katika kukuza mageuzi ya mfumo wa utawala duniani na utaratibu wa kimataifa. Katika hali ya sasa yenye utata duniani, China na Afrika kwa pamoja zimepinga vitendo vya kujilinda na msimamo wa upande mmoja, na kutoa mfano kwa nchi zinazoendelea kushirikiana katika masuala ya kimataifa. China imeahidi mara kwa mara kuunga mkono Umoja wa Afrika katika kujiunga na kundi la nchi 20 (G20), ikitumai kuisaidia Afrika kuwa na sauti zaidi na kushiriki zaidi katika masuala ya kimataifa.



Katika miaka kumi iliyopita, China imepata mafanikio ya kihistoria kwa kuondoa umaskini uliokithiri, kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na kuanza safari mpya ya kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote, huku Afrika ikiwa na ushawishi mkubwa zaidi kimataifa, Eneo la Biashara Huria lilianzishwa rasmi, na kuwa na mustakabali mzuri katika kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063. Kuna msemo wa kale wa Kichina unaosema: Watu wawili wakiwa na moyo mmoja, nguvu zao zinaweza kuvunja dhahabu. Wakati kuna mabadiliko makubwa duniani ambayo hayajaonekana katika karne hii, watu bilioni 2.5 wa China na Afrika wanapaswa kuendelea kuungana na kushirikiana, kutazamana na kusaidiana, kutunza kwa pamoja mbegu za maendeleo zilizo mikononi mwao, na kujenga kielelezo cha Ushirikiano wa Kusini- Kusini.
 
Back
Top Bottom