China na Afrika zikishirikiana vizuri kwenye kilimo zinaweza kuondoa baa la njaa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG31N687141180.jpg

Pili Mwinyi

Bara la Afrika, ambalo lina watu zaidi ya bilioni 1.3, hivi sasa linakabiliwa na mtihani mkubwa wa baa la njaa. Mbali na sababu nyingine nyingi zikiwemo ugaidi na vita vya wenyewe kwa wenyewe, baa la njaa pia linatokana na ukosefu wa mvua unaopelekea ukame na hatimaye kuwa na uhaba wa chakula, na kufanya mamilioni ya watu kuendelea kuishi kwenye umasikini uliokithiri.

Mwezi Januari, ripoti ya pamoja ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ilionya kwamba uhaba mkubwa wa chakula katika nchi 20 zinazotambuliwa kama maeneo yenye njaa, huenda ukaongezeka zaidi katika miezi ijayo.

Msukosuko huu wa njaa unaonekana kuongezeka zaidi katika nchi nne, tatu zikiwepo Afrika yaani Ethiopia, Nigeria na Sudan Kusini na moja Yemen ikiwepo Mashariki ya Kati. Msukosuko huu unahitaji hatua za haraka za misaada ya kibinadamu ili kuzuia njaa na vifo, kwani jumla ya watu milioni 20 wakiwemo watoto wasio na idadi wapo kwenye hatari ya baa la njaa.

Sababu za kuenea kwa njaa na kuwepo kwa uhaba wa chakula barani Afrika zinaonekana kuwa na utata na sio kama inavyodhaniwa mara nyingi kuwa zinatokana na ukosefu wa uzalishaji wa kilimo au hali mbaya ya hewa. Nchi za Afrika Kusini mwa Sahara zina mamilioni ya ekari za ardhi yenye rutuba, na kwa ujumla bara la Afrika linaweza kujilisha lenyewe. Lakini, cha kushangaza ni kwamba linaonekana ndio bara lililo nyuma zaidi kwenye masuala ya uzalishaji wa kilimo na kuzuia kujitosheleza kwa chakula na kushinda vita dhidi ya njaa.

Afrika imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za kilimo ambazo zinaweza kuzalisha chakula cha kutosha kulisha wakazi wengi wa kanda hiyo na hata kingine kusaza, lakini hali halisi ni tofauti kabisa. Ripoti ya FAO ya mwaka jana inaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2020, zaidi ya theluthi moja ya wakaazi wa Afrika, au takriban watu milioni 282, walikuwa na lishe duni, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 46 ikilinganishwa na mwaka 2019. Kwa maneno mengine, mtu mmoja kati ya watano barani Afrika anakabiliwa na njaa.

Kuna njia mbalimbali za kuweza kumaliza baa la njaa katika Afrika, hata hivyo inaonekana njia nyepesi na ya mkato kwa Afrika ni kutegemea zaidi kuagiza chakula kutoka nchi za nje na vilevile kutegemea msaada wa chakula ambao ni dhahiri haujawa dawa ya kuondoa njaa.

Wakati Afrika inategemea msaada wa chakula kwa kiasi kikubwa, cha kushangaza ni kwamba chakula kinachopotea baada ya mavuno kinazidi kile cha msaada kinachopelekwa kwenye bara hilo. Mwaka 2011, Benki ya Dunia na FAO kwa pamoja walitoa ripoti iliyokadiria kuwa thamani ya nafaka inayopotea baada ya mavuno pekee katika Afrika Kusini mwa Sahara ilifikia dola bilioni 4 kwa mwaka kati ya uzalishaji wa nafaka wa kila mwaka wa dola bilioni 27 kwa mwaka 2005 hadi 2007.

Ufumbuzi wa changamoto hizi, unahitaji miundo mbinu ya kilimo itakayovumilia mabadiliko ya tabia nchi, na ambayo inahitaji fedha nyingi na ujuzi wa kitaalamu, lakini kwa bahati mbaya Afrika haina kwa sasa. Hivyo ili kufanikisha au kufikia ufumbuzi huu, Afrika inahitaji kuwa na washirika wa kuaminika, ambao bila shaka wataonesha dhamira yao ya kweli ya kuleta maendeleo katika bara hilo.

Kwa Afrika, China ndio mshirika mzuri na anayefaa zaidi. Kulingana na takwimu za uwekezaji wa miundo mbinu katika Afrika, China ni mwekezaji namba moja barani humo. Miundombinu inayojenga China katika Afrika imejikita zaidi kwenye miradi ya nishati na usafiri, na kuondoa tatizo la ukosefu wa umeme na changamoto za usafiri na uchukuzi.

Kwa ujumla kuondoa kwanza changamoto hizi ni suala muhimu na la msingi, kwasababu wakati wa shughuli za kilimo umeme ni muhimu sana, na baada ya uzalishaji shambani bidhaa lazima zitahitaji kusafirishwa ili kufika sokoni.

Tangu kuanzishwa kwa FOCAC mwaka 2000, China imefanya kilimo kuwa ni moja ya sekta inazozipa kipaumbele zaidi katika kuiletea maendeleo Afrika. Ili kutambua umuhimu wa kilimo kwa uchumi wa nchi za Afrika na kuzingatia mchango mkubwa wa uzalishaji wa kilimo katika kukabiliana na uhaba wa chakula na umaskini katika nchi za Afrika, ndio maana nchi hizi zimekaribisha kwa mikono miwili msaada wa China katika sekta ya kilimo na zinaendelea kuonesha nia ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wa kilimo na China.

Mwaka 2017, Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) ulianzisha Mkakati wa Ushirikiano wa Kilimo kati ya China na Afrika, lengo lake likiwa ni kufanya kazi na washirika wa China na Afrika ili kuongeza rasilimali za umma na binafsi za China zikiwemo fedha, teknolojia na maarifa kwa ajili ya kuchochea, kuongeza na kuendeleza mageuzi ya kilimo jumuishi barani Afrika.

Wakati hii ikiwa ni hatua sahihi katika kupambana na njaa, ushirikiano kati ya China na Afrika, unapaswa kuinuliwa zaidi ili kufanya maghala ya kuhifadhi chakula kuwa nafuu na kufikiwa ili kupunguza upotevu wa chakula baada ya mavuno katika maeneo ya vijijini na mijini, kutoa miundombinu ya kutosha kusaidia kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi na kuleta ajira zinazohusiana zaidi na ICT katika sekta ya kilimo ili kuwashirikisha vijana, matokeo ambayo yatachangia pakubwa katika kumaliza baa la njaa katika Afrika.
 
China Wana technology nyingi Sana simple za kilimo tena kwa gharama nafuu
 
Soko la mazao ya kilimo China ni kubwa sana tungeweza litumia vizuri tungekuwa mbali sana
 
Mchina hawezi kutusaidia sisi kuondoa njaa. Tusimtukuze sana Mchona, yeye atuhakikishie tu soko, changamoto ya pembejeo atuachie wenyewe
 
Nyerere aliliona hili kitambo lakini wajinga wakajimilikisha mashamba ya umma
 
Back
Top Bottom