Hizo propaganda tu, Asilimia kubwa ya Vifaa ni vya china kama tu ndege nyingine Duniani....ambapo baadhi ya vifaa huagizwa nje hata Boeing hufanya hivyo hivyo.....
Marekani wanapiga sana vita China isionekane imeendelea kwa technologia kitu ambacho hawatakiweza....kwani China inakwenda kwa kasi sana.....ipo level nyingine....
Wamarekani walianza kusema Ndege hiyo haina ubora na kuipinga sana isiingie sokoni (kama vifaa vilikuwa vyao kwanini walipinga kwa nguvu zote kuwa haina ubora?)
Baada ya majaribio ya zaidi ya miaka 6 ikaonekana haina shida na hivyo kuruhusiwa iingie sokoni
Na hii ndio inaenda kuwamaliza Boeing kwa hizi ndege za kati kwa kiasi kikubwa kwani yenyewe Inauzwa bei ya kizalendo, inatumia mafuta kidogo, na inauimara wa kuaminika