China na Tanzania zaendelea kujiimarisha kwenye masuala ya uvumbuzi wa kilimo

China na Tanzania zaendelea kujiimarisha kwenye masuala ya uvumbuzi wa kilimo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
W020231208513733415548.jpg
Tanzania na China ni nchi ambazo zimekuwa zikiimarisha uhusiano wao ulioanza tangu enzi na dahari. Uhusiano huu umejengwa katika misingi imara na isiyotikisika, ambapo mbali tu na kujikita kwenye mambo ya diplomasia, pia umeingia hadi katika miradi mbalimbali ya kilimo ambayo inawanufaisha zaidi wananchi wa pande zote mbili.

Kupitia utekelezaji wa mradi wa pamoja wa kilimo wenye lengo la kukuza uzalishaji wa mazao na kuimarisha usindikaji wa chakula katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania imeweza kupiga hatua katika ahadi yake ya nchi kuleta maendeleo endelevu, kupunguza umaskini na kuondoa tatizo la uhaba wa chakula.

Mradi huo ambao upo katika kijiji cha Mtego wa Simba, Morogoro, unashirikisha Chuo Kikuu cha Kilimo cha China (CAU) na Taasisi ya Mipango ya Maendeleo Vijijini ya Tanzania (IRDP) ukilenga kuwafunza wakulima wa eneo hilo mbinu za hali ya juu za kilimo na mbinu za kisasa za usindikaji wa mazao, hususan mahindi na soya.

Kupitia ushirikiano huu unaotegemea utafiti wa kilimo, mpango huu sio tu kwamba unasaidia mavuno bora ya mazao, bali pia unaleta minyororo mipya ya thamani kwa jamii za vijijini, hasa usindikaji wa soya kuwa maziwa yenye lishe bora.

Mradi huo ni matokeo ya moja kwa moja ya juhudi za uratibu kati ya Ubalozi wa China nchini Tanzania na Serikali ya Tanzania, ukiashiria kukua kwa moyo wa ushirikiano na kubadilishana ujuzi.

Akipongeza mradi huo kwa kuleta matokeo mazuri katika maisha ya watu wa vijijini, Profesa Provident Dimoso, Naibu Mkuu wa Taaluma, Utafiti na Ushauri katika IRDP, amesema mpango huo una mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa chakula, kukuza kipato cha kaya na kuboresha lishe ya watoto shuleni.

"Kupitia mradi huu, soya husindikwa kuwa maziwa na kusambazwa bila malipo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Juhudi," Prof Dimoso alieleza. "Jambo hili sio tu linaboresha ulaji wao wa lishe bali pia linahimiza mahudhurio ya shule na kukuza ustawi wa jumla."

Katika ushirikiano huu wa kilimo kati ya China na Tanzania, wakulima wadogo wa Tanzania wanapata fursa ya kuwezeshwa kiteknolojia, kupata mbegu bora ambapo katika maeneo yao madogo ya kilimo sasa wanaweza kuvuna mazao mengi zaidi.

Aidha kuna baadhi ya mazao ambayo wakulima hawa awali walikuwa hawalimi, mathalan soya na kokoa. Kupitia ushirikiano huu ambapo wataalamu wa China wanazingatia zaidi wakulima wadogo ili waweze kuwainua, sasa wakulima wengi wameona faida ya kulima mazao haya mapya, ambapo wanapata masoko moja kwa moja nchini China.

Mbali na hapo, wataalamu wa kilimo wa China pia wameingiza mpunga chotara kupitia Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia na Maarifa ya Kilimo Bora nchini Tanzania. Kutokana na muongozo wao wa kiteknolojia, kwa sasa kiwango cha mavuno kimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 kwa eka ikilinganishwa na zamani. Kituo hicho kimetoa mafunzo kwa wakulima na wataalamu wa kilimo wazawa zaidi ya 6,550, na kuwafahamisha watu zaidi wa huko teknolojia ya upandaji wa mpunga.

Wanavijiji wanaonufaika na miradi hii ya kilimo wengi huwa wanaishukuru China, hasa timu zake za wataalamu wa kilimo, kwa kuanzisha teknolojia zinazohitajika sana na ujuzi wa vitendo ambao umeboresha maisha yao kwa kiasi kikubwa.

Mbali na uzalishaji na usindikaji wa chakula, ushirikiano huo baina ya China na Tanzania pia unajikita kwenye masuala makubwa ya kijamii na kiuchumi. Kwa kuzingatia hilo, ndio maana wanakijiji pia wanasisitiza kwamba ni muhimu kupanua mipango hiyo nchi nzima, hasa kwa kuwa inatoa suluhu kwa vitendo kwenye changamoto za lishe zinazowakabili wanawake, vijana na watoto kote Tanzania.
 
Kibaraka wa Uchina, ndani ya dk 30 umeanzisha nyuzi 4 kuhusu China
 
Back
Top Bottom