China na Tanzania zashindwa kuafikiana kwenye ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Ujenzi wakwama

Uhusiano wa CCM na China lazima utalegea pia kikwete na wakazi wa Bagamoyo hawataipenda Serikali ya awamu hii tena kwani imewapora fursa kubwa ya mji wa Bagamoyo kukua na kuwa jiji kubwa Duniani
 
Reactions: BAK
Itakuwa Serikali imestukia kuingizwa kwenye Mkataba wa Kimagungo.

If so, hongera kwa Serikali
Hongera zako uwape pindi wakishinda kesi kwani walitoa pesa zao kuwalipa fidia wananchi na baadhi walilipwa ingawa kuna ufisadi wa kutisha sana
 
Reactions: BAK
Hap hakuna cha disagreement, ilikuwa tu propaganda za amsha popo.
 
Huu mradi ulikuwa ni hatari Kwa taifa letu. Hapa tulikuwa tunaenda kushikiwa Mali na Mchina kama baadhi ya Nchi mfano Sri Lanka, Pakistan , Djibouti na Zambia n.k. hawa wote wameangukia kwenye China's debt trap .
 
Itakuwa Serikali imestukia kuingizwa kwenye Mkataba wa Kimagungo.

If so, hongera kwa Serikali
Mkataba huo ungepelekea nchi kushindwa kulipa halafu tungeingia kwenye China's debt trap. Nchi ambazo zimeanguka under China's debt trap ni Djibouti, Zambia, Pakistan, Sri Lanka
 
Mimi sijui kilichondani ya mkataba,miradi mikubwa ikipendekezwa ingepelekewa wananchi waijadili,harafu ipelekwe bungeni kupewa ruksa.
Sasa tunasema mambo tusiyojua wala kuona.
 
Reactions: BAK
Tuna Bunge DHAIFU ndiyo chanzo cha matatizo yote haya.

Mimi sijui kilichondani ya mkataba,miradi mikubwa ikipendekezwa ingepelekewa wananchi waijadili,harafu ipelekwe bungeni kupewa ruksa.
Sasa tunasema mambo tusiyojua wala kuona.
 
ulikua mradi mzuri sana,ungetoa ajira nyingi sana,tatizo tulitaka wawekezaji waweke dola bilioni kumi hapo kisha ujenzi ukiisha watukabidhi na kuondoka,hiyo biashara haipo
Mradi mzuri Ila madhara yake huyajui wewe . Kawaulize Sri Lanka, Zambia, Pakistan, Djibouti. Hawa wote walidondokea kwenye China's dept trap . Yaani hizi nchi zilikuwa achana na Zambia ambao wamenyanganywa misitu, Shirika la umeme, Shirika la utangazaji. Hizo nchi zote wamenyanganywa Bandari zao na Mchina kwa kipindi cha miaka 100. Hii inaitwa China dept trap
 
Walitaka kutuibia tu.
Walitaka kukuibia? Hopeless kabisa
Si afadhal huo mradi ni tangible
Haya waambie hawa ambao hawawaibii watuoneshe zilipo 3.+ trillion
 
Bora umenisaidia.
 
Nimeshindwa kuelewa JK aliwakaribisha vipi hawa wachina..! Yani Mradi wa Trillion 23...!!! Bajeti yetu ya mwaka mzima

Yaani mradi huu ungekamilika/ ukifanikiwa ingekuwa kama ule wa Mtwara natural gesi, kuuza nchi, pili Dsm Mtwara na Tanga zipo kwani huo wa kazi gani! IDLE ELEPHANT!
 
Hakika ni hela ndefu sana hiyo, na hiyo miradi uliyoitaja bila shaka kabisa ni mhimu sana kwetu.

Lakini pia nakuomba uiangalie bandari hiyo kama biashara inayoweza kuliingizia taifa pesa ndefu sana.

Piga picha tu kichwani mwako huku ukiwa na ramani ya nchi yetu na majirani zetu, hasa wa upande wa magharibi. Achana na hivyo viinchi vidogo dogo; angaza macho yako yakivuka ziwa Tanganyika toka kusini hadi kaskazini, mpaka kule karibu na Afrika ya Kati.

Ni kukosa uwezo tu, na kwa kweli kupanga ni kuchagua. Sasa hivi inabidi tupange hayo uliyoyaweka hapo juu, kwa sababu uwezo hatuna.

Lakini kufanya hivyo haina maana kwamba mradi huo hauna manufaa kwetu. Una manufaa makubwa sana, kwa miundombinu tunayojenga sasa na biashara zetu na majirani zetu pia.

Kama faida hizi unazitambua na huoni umhimu wake, basi tunatofautiana sana kimaono.
 

Mkuu upo sahihi,sio kwamba haina umuhimu ila nachosema mimi ni hv,tuna bandari kubwa kama tatu hv hzo nilizozitaja,kwa nn tusiziboreshe hizo kwanza na kama uhitaji ukiwa ni mkubwa kiasi cha kwamba tunatakiwa kuongeza bandari nyingine,ndipo huko mbeleni tuifikirie hiyo bandari ya Bagamoyo.

Kwa sasa hiyo miradi ya umwagiliaji ikianzishwa,ina matokeo ya haraka sana kwani soko la chakula Africa tu ni zuri,wakulima watapata bei nzuri ya mazao yao kwa usimamizi wa Serikali hivyo uchumi wa nchi utakuwa tu.

Halafu isitoshe,bandari za Dar na Bagamo zipo karibu mno,kwa nn wasiiboreshe kwa kuipanua hii ya Dar kwanza kisha ikizidiwa ndio wafikirie hizo zingine kwa kuwa karibia asilimia kubwa sana ya mizigo ya baharini hupitia bandari hii ya Dar
 
miaka 50 ijayo bandari ya dar itakuwa pafinye sana,Bagamoyo ilikuwa imefocuss miaka 100 mbele sio miaka 5 ijayo
 
Unapozungumzia kuendeleza 'kilimo' moja kwa moja nakuelewa vizuri sana, kwa sababu mimi naamini maendeleo ya nchi yetu yangekuwa tofauti sana wakati huu kama tungeamua toka mwanzo kabisa wa uhuru wetu kuvifanya kilimo na elimu kuwa vipaumbele vya kudumu katika mipango yetu ya maendeleo ya kila mwaka.

Kwa hiyo siwezi kamwe kupinga wazo lako la kilimo cha umwagiliaji kama ulivyoandika. Nashukuru pia kuona kwamba wazo la Bandari ya Bagamoyo hulikatai moja kwa moja, bali ni swala la mipangilio tu na uwezo utakaokuwepo kuuwezesha.

Lakini kumbuka kwamba, habari zilizokuwepo (kama ni kweli), ujenzi huo haukuwa deni. Wawekezaji wangejenga bandari na eneo la biashara na kuliendesha kibiashara ili mtaji wao na faida virudi kwa mda maalum kabla ya kuukabidhi kwetu.

Kwa hiyo huu uwekezaji usingekuwa matumizi ya pesa yetu ya kuelekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji, elimu, n.k.

Lakini katika uwekezaji wa namna hii pia masharti kadhaa lazima yawepo, na nadhani masharti hayo ndio serikali imeyaona kuwa magumu au yasiyokuwa na maslahi kwetu ndio maana ikashindikana kufikia maafikiano.

Bandari yetu ya Dar es Salaam inaweza kutosheleza kwa mahitaji yetu ya ndani (Tanzania) kwa mda; lakini ni bandari finyu ambayo kwa mda mrefu hata mahitaji yetu tu ya ndani itashindwa kuyamudu.
Tanga inafaa sana kuendelezwa, hasa kuitumia kwa mizigo inayoelekea kaskazini, Tanga, Moshi, Arusha, Manyara na hata Mara na Mwanza endapo kama miundo mbinu ingeweza kuimarishwa. Lakini bandari hii nayo ni finyu zaidi. Haiwezi kuingiza na kuhudumia meli kubwa. Labda ule mpango wa Mwambani ufufuliwe tena, lakini hii iliyopo mjini Tanga haina mazingira ya kuifanya kuwa kubwa ya kutosha kuhudumia mizigo mingi.

Kama nilivyoeleza huko mwanzo, Bandari ni biashara kama zilivyo biashara nyinginezo kama ndege, na hata barabara, n.k.

Eneo la ukanda wetu huu wa Afrika, hasahasa Zambia, DRC tunaweza kuwanasa vizuri sana kwa biashara ya bandari zetu kama zitaweza kufanya kazi kibiashara hasa.

Bagamoyo inaweza kukidhi mahitaji yetu na mahitaji ya nchi hizo kama itajengwa kwa malengo hayo.
 
Hatuna haja nna bandari ya Bagamoyo! Hongera Magufuli kwa hili! Hata kama gharama ingekua chini ya milioni mia za kitanzania!! Hapa Jk alikuwa anatengeneza mkeka wake wa kupumzikia! We miss you JK!
Ndiyo maana JK haishi kwenda kumsalimia Magu ikulu. Labda huwa anakwenda kujulia hali ya Bwagamoyo deal!
 


Serikali kwenye hili naisifu huu mradi sio mzuri na tayari tuna bandari Dar na tunajenga bandari nyingine Tanga hakuna ulazima wa kutumia pesa nyingi hivi kwa mradi huu. Mnajua hata kama tungelipa asulimia 5% tu kwa mwaka ni $100M kwa project ya $10M . Hiyo interest tu miaka miwili ingewekezwa airport ya Kia tungepata pesa zaidi kwa watalii kwa uhakika tena. Vilevile tungeweza kujenga reli kuunganisha Arusha, moshi mpaka singida ili kukuza utalii
 
Hao Oman ni kama chambo tu kwenye huo mradi, China angekuja kutudhulumu kama kawaida yao, ingekuja kuwa chini ya hawa Whitedog wa china kwa miaka 200.......
Miaka 100...including exclusive use of it....closing Dar Port as a strategy....who knows if it could be used as their naval base.???
Wachina wanaweza kuinunua Africa yote
 
Miaka 100...including exclusive use of it....closing Dar Port as a strategy....who knows if it could be used as their naval base.???
Wachina wanaweza kuinunua Africa yote
Hii mijamaa inaweza kuinunua Africa reserves of China US$3.23 trillion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…