China ndio Sababu ya Maduro kutekwa na Marekani, Mchina ni tishio kwa Mmarekani

China ndio Sababu ya Maduro kutekwa na Marekani, Mchina ni tishio kwa Mmarekani

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Namna Marekani alivyocheza karata zake kwa Venezuela ni kama Demu mkali ale vitu vyako alafu kisha hakukatae badae unamuona anajibebisha kwa mwamba mwingine ambaye wewe ni kama mshindani wake wa muda mrefu, unaamua kumteka demu na kuondoka nae kwa nguvu hili awe na wewe kwa lazima.

Screenshot_20260104_155344_Instagram.jpg


Hakuna nchi ambayo ni Tishio kwa Marekani kama China, kitendo cha Venezuela siku ya jana kuarika maofisa kutoka China kwenda kuzungumza na serikali ya Venezuela ni kama Marekani aliona sasa hapa nanyanganywa tonge mdomoni. Ukizingatia China ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani baada ya Marekani. Na kama mazungumzo ya China na Venezuela yangeenda vizuri, basi kwenye biashara ya mafuta China ingeenda kuwa bingwa mara dufu kiuchumi na Marekani angetikisika kidogo. Jambo ambalo Marekani kwa hali yoyote asingekubali itokee.

Ebu tutazame hili Jedwali hapa namna China anavyomfukizia Marekani kimya kimya.


Screenshot_20260104_105920_Instagram.jpg


Ukiangalia pato la Taifa tu, Marekani anamzidi China theluthi tu ya utajiri wake. Kana kwamba China angefanikisha tu baishara ya mafuta na Venezuela basi China ingeeimarika mara dufu ukizidisha na namna China ilivyoteka nchi nyingi kibiashara hususani za Asia na Afrika.

Wese, Mafuta ndio chanzo kikuu, na Mmarekani aliogopa sana Karata ya Mchina, akaamua kuiwai kabla ijaleta madhara. Na ndio maana Rais wa Venezuela ametekwa mara moja tu baada ya kufanya mkutano na viongozi kutoka China, lengo la kwanza ni kuharibu dili la China, lengo la pili ni kuweka utawala wao kwenye kudhibiti mafuta. Na Venezuela ndio nchi yenye kiwango kikubwa cha Akiba ya mafuta duniani.

Marekani akatazama kushoto akamuona Mrusi nae anakodoa macho, hili kumnyamazisha Mrusi waliingia Makubaliano na Urusi akapewa kibali cha kuendelea kumtwanga Ukrein kwa kigezo cha Urusi kutoingilia mambo ya Venezuela ndio lengo la Trump na Putin kukutana. Yani Venezuela na Ukraine zimetumika kama njia za Marekani na Urusi kumalizana Kibingwa. Marekani hakutaka Urusi aingie kwenye anga zake, hivyo akaamua kumuachia Ukrein, huku akicheza karata vizuri kabla ya mchina. Hiyo ndio tunaiita Bargaining Power, nchi zingine zinakabidhiwa kwa makontawa hili wasiingliane kwenye kugawa dozi
 
Back
Top Bottom