China ni kama maji usipoyaoga utayanywa - India yasitisha ununuzi wa drone

China ni kama maji usipoyaoga utayanywa - India yasitisha ununuzi wa drone

def_xcode

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,896
Reaction score
5,181
India ina mgogoro wa mpaka na China. Sasa ilikuwa imeeweka oda ya drone 400 kwenye makampuni yake ya ndani kwa ajili ya usafirishaji wa vifaa kwa majeshi yaliyo mpakani. Sasa imekuja kugundua hizo drone zina vifaa kutoka China.

Inadaiwa uchunguzi wao ulianza hapo awali baada ya drone zao za awali walizoletewa kuna siku moja iligoma kuruka. Ndipo wakaanza kufuatilia shida ni nini wakaja kugundua mchina ameihack. Nyingine ilikuwa inaruka kwenye eneo la Kashmir nayo ikaanguka napo wanadai China alifanya yake.

Sasa wanaogopa kama hizo drone zinaenda kutumika kwenye eneo ambapo China na India wana mgogoro na zikawa na vifaa ndani yakee kutoka China kuna hatari zaidi china atakuwa anaziteremsha anavyotaka.

Hii ikanikumbusha vijana wadogo Efraim Diveroli na David Packouz ambao katika vita vya USA Afghanistan walikula tenda ya dola milioni 300 kusupply risasi kwa jeshi.

Wao badala ya kununua risasi kutoka ulaya kama sheria inavyowataka, wakaamua wanunue risasi toka china kwa sababu ni bei chee, wakawa wanazipack kwenye maboksi kama vile zimetoka huko zinapotakiwa kutoka na kisha kuwasilisha risasi hizo.

Vijana wakawa matajiri sana ila mwisho walikuja kufungwa.
 
Back
Top Bottom