China-US (Tech War): China wabaini ndege ya jeshi la Marekani ikiangusha vifaa vya kiupelelezi katika bahari ya Kusini ya China

China-US (Tech War): China wabaini ndege ya jeshi la Marekani ikiangusha vifaa vya kiupelelezi katika bahari ya Kusini ya China

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Ndege hiyo ya Marekani ya NAVY, Boeing P–8A Poseidon, ilikuwa ikipita katika anga la kimataifa katika Bahari ya Kusini ya China.

Jeshi la China kwa kutumia vifaa vya teknolojia vyenye uwezo wa kuona mbali viliweza kunasa tukio hilo na kulirekodi kwenye video.

Ni nini ambacho ndege hiyo ya jeshi la Marekani iliangusha kwenye bahari hiyo?

Baada ya jeshi la wanamaji la China, The People's Liberation Army Navy (PLAN) kuviibua vifaa hivyo, wataalamu wa vifaa vya kijeshi wa China waligundua kuwa ni submarine detectors.

Ni vifaa ambavyo vinaweza kutambua submarine mahali ilipo na kutuma taarifa kwa jeshi la Marekani.

Mpaka sasa serikali ya China haijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo wala Marekani pia.

Ikumbukwe mwaka 2023 puto (balloon) lililokuwa limetokea Hainan China lilipaa juu ya anga la Marekani na kunaswa. Lakini baadaye watafiti waligundua halikuwa na madhara yoyote katika kukusanya taarifa na kuzipeleka China
.

Je, huenda Marekani walizutupa hizo submarine detectors eneo hili ili kukilinda kisiwa cha Taiwan dhidi ya submarine za China ikitokea uvamizi wa kijeshi, kama baadhi ya wachambuzi wamekuwa wakisema?

20240628_022704.jpg

CREDIT & VIDEO:
View: https://twitter.com/CGTNOfficial/status/1806214948936360299?t=flEKL5sgwwxTTk_Kms_Y3A&s=19
 
Tatizo tamaa ya Marekani ni China iingie vitani analeta ni kama anaichokoza makusudi
Ndio mkuu, na bora kipindi kile China aliamua kukaa kimya ktk ile ziara ya Peros, huenda angejibu mpaka sasa angekuwa kwenye wakati mgumu sana.

Linapokuja suala la vita US ni mtu mwingine, ana uzoefu mkubwa wa haya mambo.
 
China ni taifa linaloamini katika nguvu ya peace table as a means of conflict resolution tofauti na Marekani

Lakini pia China iko strong kuhakikisha inalinda sovereignty and territorial integrity

China itakuwa one of the greatest soon. Maana Wana tech nzuri Sana.
Elimu ya china imewabadilisha sana
Ni kweli, msisitizo umewekwa kwenye sci-tech

Serikali inasupport kwa kutoa pesa za kutosha kwenye innovation na R&D hasa cutting-edge technology

Matunda wameaanza kuyaona na hawajaridhika
 
Wachina na Wahindi ni Cheap labor kwelikweli, ukiingia maeneo yao ya kazi hadi unawaonea huruma kwakweli. Huko USA jamaa wanafanya kazi kama maboss. Ebu fikiria Uchina mtu wa miaka 36 anaanza kukosa kazi kisa ameshatumikia kazi muda mrefu na kuchoka mwili na akili hivyo hawezi kudeliver kama u30
 
Ndio mkuu, na bora kipindi kile China aliamua kukaa kimya ktk ile ziara ya Peros, huenda angejibu mpaka sasa angekuwa kwenye wakati mgumu sana.

Linapokuja suala la vita US ni mtu mwingine, ana uzoefu mkubwa wa haya mambo.
Nyie watu bana!
Manapenda sana kudanganyana,
Huo uzoefu mkubwa wa mambo hayo ya vita kauonyesha wapi Kwa mafanikio?
Nyie vijana,movie za Hollywood zimewaharibu mno.
Huo uzoefu na uhalisia haviendani kabisa,maana USA amteswa ama kushindwa karibu Kila vita alizopiganq.
 
Ni kanchi kachochezi sana kanavuruga kanakimbia basi.Mmarekani ni mchochezi tu.
 
Back
Top Bottom